Nilikuwa nasikia tetesi kwamba Zantel Imefilisika na huenda ikauzwa

mzeelapa

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
1,118
404
Nilikuwa nasikia tetesi kwamba Zantel Imefilisika na huenda ikauzwa. Mimi ni mtumiaji wa Simu na Modem ya Zantel. Sasa hivi niko safarini Iringa lakini kwa wiki ya tatu sasa mtandao wa Zantel hauko hewani, imeshafungwa? Au ndio imekufa kifo cha mende? Hela zetu zilizoko huko zimeyeyuka. Nijuzeni maeneo mengine kama bado iko hewani.
 
pole mkuu, hiyo kitu wamenunua tigo. ingawa wanafichaficha kutokana na maslahi ya kibiashara. hususani huko visiwani wanahofia watu kuwakimbia.
 
Ilishauzwa/ubia! Sijui kwann wana ficha ficha.. Mustakabali wa mifwedha watu waliyoweka Ezy pesa sijui inakuwaje
 
Haijafichwa sema nyie mnategemea sana taarifa za kidaku na ni kwamba wale etisalat wameuza hisa zao zote kwa milcom wamiliki wa Tigo.sio kwamba Tigo imeinunua zantel na brand name itabaki kama ilivyo so ni sister companies operating independently
 
Umecheza na lugha, lakini nimekuelewa. Nilipeleka simu yangu kwa fundi akapata net work lakini kuna kitu amefanya kwa kupitia mtandao wa Tigo. Nadhani kuna kitu kimeunganishwa kati ya Tigo na Zantel.
 
Back
Top Bottom