Nilijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura mwaka 2015. Je, mwaka 2020 jina langu litakuwepo?

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,930
Habarini ndugu zangu,

Mwenye kujua nilijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura mwaka 2015, ila mwaka huu sikwenda kwenye kufanya uhakiki wa mpiga kura kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu.

Je, mwaka huu October nikienda na kitambulisho changu (ambacho bado ninacho) maeneo nilikojiandikisha mwaka 2015, jina langu nitalikuta au ndio sina tena sifa za kupiga kura?
 
Ndio, Jina lipo kwa taarifa hizo hizo za mwaka 2015.
 
Hapo ndo mtego mwingine kwa upinzani maana kama walikua wameususia ule uchaguzi. Hope zitatumika taarifa za kujiandikisha awali
 
Hapo ndo mtego mwingine kwa upinzani maana kama walikua wameususia ule uchaguzi. Hope zitatumika taarifa za kujiandikisha awali

Uchaguzi waliosusia hauko chini y NEC na hata ule wa Zanzibar Marudio 2016 March pia walitumia daftari lile lile ila walipiga kura upya

Tatizo ni kwamba hata wakati wa uboreshaji wa daftar miezi kadhaa iliyopita walizunguka nchi nzima ila ilikua almost kimya kimya(Japokua matangazo yalikuwepo)

Ninachowalaumu upinzani ni kushindwa kuwahabarisha watu wengi zaidi kujiandikisha. Na wengi walipitwa sijui wanategemea muujiza gani
 
Ile haikua kimya kimya sema wapinziani waliipotezea ni kama waliona watatoa kiki ya bure. Ukiwa unafatilia vitu mtaani kwako ule uboreshaji hauwezi kukupita. Wengi waliusubiria kwa hamu ili kupata kitambulisho kile wapate urahisi wa kukipata cha NIDA.

Kuna sehemu watu hawakujitokeza kabisa japo matangazo yalipita mitaan kila siku. Waandikishaji walikua wanasinzia vituon hakukua na folen kabisa.

Hio aya ya mwisho tayari wameshajibu wataingia barabaran kuandamana.

Kwa busara NEC inaweza tumia vitambulisho hivi. Kama taarifa zipo ni kuchapisha tu majina kisha wananchi wataenda vituon kuhakiki kabla ya siku ya kupiga kura

Back
Top Bottom