Nilighairi ndoa baada ya baba mkwe kunisingizia nimemuibia elfu sabini

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,778
Habari wakuu,
Nimekumbuka hili tukio lililotokea miezi mitatu iliyopita baada ya kukuta missed calls zake mbili kwenye simu yangu jioni hii

Ilitokea kipindi nilipokuwa kwenye harakati za kumuolea mke wangu Mwa J mke wa pili ili mke mdogo amfunze Mwa J namna ya kuishi na mume. Yule binti alikuwa mzaliwa wa Tanga

Sintosahau siku hiyo ambayo mida ya saa nne asubuhi, baba mkwe aliniaga pale kwake na kuniacha nikiwa sebuleni natazama runinga na kwenda kuwapokea watu wake muhimu ili waje wanione. Mida ya saa tano hivi, baba mkwe aliwasili akiwa na mijibaba mitatu, ndipo wanafamilia wengine walipokuja. Shamla shamla za hapa na pale zilitaradadi mpaka mida ya saa kumi hivi

Muda huo baba mkwe alimvuta mkewe nje na kwenda kumnong'oneza, niliisikia sauti ya mkewe ikisema, "Mume wangu acha, utatutia aibu jamani, ona majirani walivyojazana! Nitakuwa mgeni wa nani mimi". Kwa akili yangu nilijua itakuwa baba mkwe amezimua kiasi cha kufanya fujo kwenye masufuria ya ukoko huko nje, kumbe sikuwa sahihi

Niliskia sauti yake ikipaza na kusema, "Hapana mke wangu, wacha nilipasue dongo, kama mbwai, mbwai tu. Humu ndani tulikuwa wawili tu, mimi na yeye. Kabla sijaondoka niliacha elfu sabini ndani ya foronya (mto), kwani mimi ninaweza nikajiibia, mke wangu". Nilibaki mahala pale nimetulia huku nikibubujikwa na machozi ya lasha lasha. Niliamua kufunga virago vyangu, kisha kuvaa yale mavazi yangu ya heshima ya tenge lenye maua ya njano (sheti), tai yangu ya kijani, suruali yangu nyeusi, moka za bluu na neck tai ya bluu

Baada ya hapo nikapambana kwenye boda boda yangu iliyokuwa ikivutwa kwa nyuma na kiganja cha kulia cha baba mkwe kisha kutokomea kwenda kumalizia hasira zangu kwa Mwa J

Uliwahi kumbwa na aibu gani ukweni ambayo hutokuja kuisahau?
images%20(1).jpg
 
Back
Top Bottom