Nilifundishwa: Imani inahusika katika mahusiano ya kweli

Nilifundishwa: Imani inahusika katika mahusiano ya kweli

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,969
Salamu wana Jamiiforums
Kunawakati nakumbuka tulikuwa kwenye mafundisho ya mahusiano. Ningependa nishirikiane na ninyi mafundisho ambayo yamebaki kwenye akili yangu kila siku.

Ilikuwa mwaka 2004 nilikuwa kwenye mafundisho ya vijana na mahusiano tulifundishwa kuwa imani inahisu sana katika mahusiano. Mkufunzi kutoka Uganda alieleza kwa kina umuhimu wa kuwa na mahusiano na mtu mwenye imani inayofanana.

Alieleza kuwa imani ndio inayofanya familia kuwa imara. Pia hupunguza matatizo mengi sana katika mahusiano.

Ni muhimu sana kuwa na mtu mnaoendana katika imami ili kuimarisha mahusiano na kuwafanya watoto wenu wawe katika msimamo mmoja na kuwa katika mtazamo mmoja.

Alieleza chanzo kikubwa cha watoto kuwa katika tabia ambazo haziendani na jamii ni moja wapo ya wazazi kutokuwa na imani moja.

Ni hayo tu.
 
Ninataka kushea na ninyi japo imani sio kila kitu.
 
Hata mimi nishawahi elezwa hili, pia niliambiwa KE na ME wasitoke katika jamii ambazo zina tofauti kubwa sana ya kipato/ kiuchumi.
 
Hata mimi nishawahi elezwa hili, pia niliambiwa KE na ME wasitoke katika jamii ambazo zina tofauti kubwa sana ya kipato/ kiuchumi.

Watu wanasema mapenzi hayana fomula lakini kuna kanuni za msingi kabisa ni lazima uzifuate ili muishi kwa amani.
 
Back
Top Bottom