Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,020
- 156,480
teheee...aisee we mdau sijakuona kitambo.
mimi nina visa viwili, kimoja hakifai hata kuweka humu,mwenye kiu nacho ani PM
hiki cha pili cha kawaida: kuna mmama fulani alikua rafiki yake mama, alikua anapenda kuja home...
basi mimi kila akija nilikua namfuata mama namnong'oneza nakumwambia "mama mimi nikikua nataka nimuoe huyu mama" hapo nilikua na miaka kama 6,...majuzi nimekutana na yule maza, ni mtu mzima kinoma...akanitania...akanambia wewe si ulisema utanioa? hahahaaa...
I was a litle girl nina 6 years kuna uncle wetu alikuwa apenda sana kuja kwetu sasa kuna siku mama alinunua kabati wakati linaingizwa ndani yule uncle akawa anasaidia nkamwambia aache asijipendekeze kwenye kabati letu akenda mwambia mama nlichapwa nkaambiwa nimuombe radhi
True story niikumbukayo katika hili , nakumbuka nikiwa na 6 yrs.
Kuna magari yalikua yakiitwa Factor films yakipita kila mkoa ama wilaya kwa mwezi mara 1 yakionesha sinema, na hiyo ndiyo siku ya mgao wetu tr. 23 monthly!
Baba alishanipa warning mapema kua sitakiwi kwenda sinema siku hiyo kwakua mapema ya hiyo siku nilionekana nina symptoms za malaria.
Warning ya Baba haikufanya kazi mi nikaenda, niliporudi alinipa kichapo cha haja.
Baada kichapo nikamfata Maa nikamuuliza "hivi mama , huyu baba ni ndg yetu?"
akaniuliza , "kwanini ? " nikamwambia kanichapa akaniuliza tena "kwa hiyo unataka tumfanyaje?" nikajibu
"kwanza leo asile kwetu, usimpe chakula chetu alafu tumfukuze kwetu"