Nilichokoza, sasa sijui nifanyeje....!

Nilijaribu kumchokoza mke wangu kuwa tungeenda kumpima mtoto wetu DNA...! Sasa nakosa sipati usingizi, kila wakati "Mimi nataka nikae na amani bwana..."!. Je, hii inaashiria nini? Ni uzushi, au ni kweli anataka akae na amani? Nifanyeje, hasa ukuzingatia kuwa kwa sasa kupima DNA ni mlolongo mrefu, tena ulio na complications nyingi?

Yaani unajihisi wewe ni mume *****? Nenda ukapime ili uzime huo moto.
 
pole kaka hilo suala si mchezo ila cha msingi nadhani pia ulikua unataka kujua process ya kupima DNA hilo ndo la msingi hiki kitu ni muhimu uende ukacheki asee hapo hata mtoto mdogo atakua anjua kuna kitu kimejificha nenda kapime bila kujishauri
 
Huyo ni mke kweli wa ndoa au ni hawara au nyumba ndogo?? Kama ni mkeo wa ndoa then u must be sick in the head
 
Hivi kama kweli mmekwenda kupima na mtoto akagundulika kuwa vinasaba vyake vinasigana na vya baba nini kitafuatia!? km si mkanganyiko na kasheshe kubwa itakayohitimishwa kwa ndoa kusambaratika. Ndo maana wahenga wanatuasa kuwa makini tunapotafuta wa kuishi nao kinyumba ili kukwepa mitafaruku km hiyo. Hata hivyo kitanda hakizai haramu, na pengine ni a blessing in disguise kwa wale marijali lakini sperm counts zao ni zero.
 
Shukrani kwa wale woote walioweza kuchukua muda wao na kuchangia mawazo yao juu ya huli...! Lakini ieleweke tu kuwa "nilimchokoza", yaani nilimtania tu, kuona reaction yake. Ilikuwa ni namna ya kumsoma mwenzio kisirisiri tu. Lakini inauma kuambiwa kuwa kashamegwa na sasa anataka kuwa na amani, je ni amani ya kujulikana kuwa kasaliti ndio anataka?
 
Hebu tafakari itakapodhihirika kuwa mtoto ni wako itakuwaje? Upimaji wa DNA ninavyojua mbali na process zingine haipungui laki tatu. Je ni muhimu kuifanya hiyo test?
 
Shukrani kwa wale woote walioweza kuchukua muda wao na kuchangia mawazo yao juu ya huli...! Lakini ieleweke tu kuwa "nilimchokoza", yaani nilimtania tu, kuona reaction yake. Ilikuwa ni namna ya kumsoma mwenzio kisirisiri tu. Lakini inauma kuambiwa kuwa kashamegwa na sasa anataka kuwa na amani, je ni amani ya kujulikana kuwa kasaliti ndio anataka?

this is one of the worst cruelty one can do to his/her beloved child; psychologically kupima DNA ni kitendo kibaya sana, omba Mungu majibu yawe kwamba sio mwanao vinginevyo huyo mtoto utakuwa umem-torture sana na wengine huwa wanfikia hatua ya kupoteza mapenzi na baba zao kabisa ... imani inayopatikana kwa mtoto ni kwamba yeye ni mtoto wa haramu na hata kama umemzaa inaonekana ilikuwa ni kwa bahati mbaya tu, hivyo kiuhalisia wewe siyo baba yake!! tafuta habari kuhusu hiyo kitu inayoitwa DNA test, ni mbaya sana!
 
Kwenye hilo, wanawake wako sensitive, Na kwa vile ameonyesha kukubali, anauhakika ni wako. Yaishie hapo mwambie nimekubali wewe kweli ni wangu. Kama angekuwa na wasiwasi, asingetaka muende kupima ! kwa hiyo ulichotaka umeshapa, huhitaji tena ushauri ! Close th chapter, mtafutie zawadi nzuri!
 
Hii kauli yako wala siyo. wanandoa wanawindana kama hujui

Do mbona hatari sana ! Na ukishaangukia kwenye mtego mwenzio anafurahi ama anahuzunika na kuichukulia kuwa ni changamoto kwenu na kwake?

@ Konakali; swali la msingi unao uhakika gani kwamba wewe umetoka maungoni mwa baba yako kama si uthibitisho kuwa umezaliwa ndani ya muungano wao?

Haraka sana muombe radhi mwenzio na usirudie huo upuuzi na ubinafsi wa kujifikiria wewe tu; yaani mpaka mna mtoto kuna kikubwa kipi unachohitaji kumsoma na pia nakuambia kama kweli kamegwa nje ! kwa atitude hii wewe umechangia kama sio kuisabaibisha kabisa; sie tu hapa tumekereka kuwa iwaje mwanandoa afikie hatua kama hiyo; na usituletee habari ya kuwa ni utani; asilimia kubwa ya mambo tufanyayo kwenye mizaha ni tafsiri ya mawazo halisia yaliyojikita vichwani mwetu!

Wacha hii maneno! na ombea mwaao asije kusearch hii archive!
 
Kapime tu upate uhakika,kwani watu wengi tu wamebambikiwa mtoto wa baba mwenza,cha msingi ukikuta sio wako wewe endelea na mkeo,na baba wa mtoto kama anaomshiko zaidi yako,itabidi alete pesa ya matunzo ya mtoto,ila hamna mtoto kwenda kwa baba yake,inshort analipia matunzo ila mtoto anabaki wako,afterall akigraduate chuo,returns utaanza kuziona.na hiyo inakuwa fundisho kwa wife,akicheza nje,asije ndani ya nyumba na masalio ya sperms za jamaa zake.
 
Au huyo mtoto kafanana na bosi wa mkewe au houseboy?ukimchunguza kuku humli kaka, na kitanda hakizai haramu, mandhali bado mtoto anakuita baba ni wako huyo hata upime dna bado ni mwanao, wewe si something ya mama yake basi wewe ni babayake bado aidha halisi au wa kambo bado ni baba
 
Kwenye hilo, wanawake wako sensitive, Na kwa vile ameonyesha kukubali, anauhakika ni wako. Yaishie hapo mwambie nimekubali wewe kweli ni wangu. Kama angekuwa na wasiwasi, asingetaka muende kupima ! kwa hiyo ulichotaka umeshapa, huhitaji tena ushauri ! Close th chapter, mtafutie zawadi nzuri!

Zawadi itakayomfaa ni kumpatia haki yake kisawasawa
 
Kapime tu upate uhakika,kwani watu wengi tu wamebambikiwa mtoto wa baba mwenza,cha msingi ukikuta sio wako wewe endelea na mkeo,na baba wa mtoto kama anaomshiko zaidi yako,itabidi alete pesa ya matunzo ya mtoto,ila hamna mtoto kwenda kwa baba yake,inshort analipia matunzo ila mtoto anabaki wako,afterall akigraduate chuo,returns utaanza kuziona.na hiyo inakuwa fundisho kwa wife,akicheza nje,asije ndani ya nyumba na masalio ya sperms za jamaa zake.

Newmzalendo msaidie kujibu kona kali;

Mnao uhakika gani kuwa mnatokana na sperms za Baba zenu waliowalea! Unajua mnachoshabikia hapa kwa mazingira ya hadithi ya konakali ni matusi kwa mama zetu?

Kwa maneno mengine Konakali kabla hujaenda kuhakiki Kinasaba cha mwanao; anza kwanza kuhakiki cha kwako; usije kuta hii dhambi ni ya ukoo nawe umepatilizwa tu na unataka kumpatisha shida binti wa watu!
 
Back
Top Bottom