Nilichokiona uwanja wa taifa mechi ya Yanga na Ashanti

sungura1980

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
1,909
Reaction score
1,225
Napenda kuwapongeza wachezaji,wanachama na mashabiki wa Yanga kwa ushindi wa kishindo wa goli 5 kwa 1.

1: Ukaguzi wa tiketi na rushwa.
Kuna wakati niliwahi kwenda kuangalia mechi kati ya Yanga na Simba,basi nikakata tiketi ya 15,000 lakini pale jukwaani nilipokaa,asilimia kubwa ya walionizunguka ni wale waliokuwa na tiketi za 3,000 na kinachofanyika wanatoa hongo ya sh 1,000 kwa maaskari then wanaruhusiwa kukaa jukwaa la 15,000.Hivyo hivyo na jana ndio utaratibu uliokuwa ukifanyika,waziwazi kabisa!Hivi hili TFF hili hamlifahamu?

2: Usafi wa viti na vyoo!
Nimekuwa nikijiuliza maswali bila kupata majibu,hivi zile hela zinazokatwa kila mechi kwa ajili ya uwanja zinafanya kazi gani?Nimekuwa nikihudhuria mechi pale taifa mara nyingi sana lakini kila siku mambo ni yale yale,viti vichafu,vyoo vichafu sana kupindukia.Jamani hela tunayotoa kama viingilio ni kubwa sana hizo huduma za usafi zifanyike,na kama kuna watu wanachukua hizo hela za usafi wakati usafi haufanyiki wawajibishwe.

Najua wahusika wamo humu JF,wayafanyie hayo kazi.Pia wale waliokuwa uwanjani jana na wale wenye uzoefu na uwanja wa taifa karibu tuchangie!
 
Usafi ni Tabia! vinginevyo itakuwa kumshutisha Punda kunywa Maji. TFF pamoja na wenye mamlaka na uwanja huo Wajitambue!!
 
Warudishe utaratibu wa zamani. Ticket ikaguliwe tena sehemu ya kukaa. Vinginevyo kwa nini kuweka viwango?
 
Pale sehemu ya kukaa ndo kunako hongo,ulishakaguliwa getini vzr na tiketi inachanwa kipande ili isiweze kutumika tena.Sasa pale kwenye kukaa kuna askari na nadhani wengine ni viongozi wa vilabu husika na TFF,hapo ndo mtu anaonyesha tiketi ya 5000 mathlani na sehemu yenyewe ni ya watu wenye tiketi za 15,000.anatoa 1000 au 2000 then anaruhusiwa kukaa
 
Pale sehemu ya kukaa
ndo kunako hongo,ulishakaguliwa getini vzr na tiketi inachanwa kipande
ili isiweze kutumika tena.Sasa pale kwenye kukaa kuna askari na nadhani
wengine ni viongozi wa vilabu husika na TFF,hapo ndo mtu anaonyesha
tiketi ya 5000 mathlani na sehemu yenyewe ni ya watu wenye tiketi za
15,000.anatoa 1000 au 2000 then anaruhusiwa kukaa

Na hiyo hatimaye hupelekea sehemu ambayo unahisi ni ya gharama ambayo wanaweza kukaa watu wastarabu, ukawaona wahuni wamekaa na kurusha chupa uwanjani, kisa walihonga 1000 tu kwa maaskari!
 
Jamal Malinzi na wagombea wengine watuambia wakichaguliwa watatatua vipi kero hizi,
kwani wengi wao ni member wa JF
 
Last edited by a moderator:
Jamal malinZI na wagombea wengine watuambia wakichaguliwa watatatua vipi kero hizi,
kwani wengi wao ni member wa JF
 
Last edited by a moderator:
Napenda kuwapongeza wachezaji,wanachama na mashabiki wa Yanga kwa ushindi wa kishindo wa goli 5 kwa 1.

1: Ukaguzi wa tiketi na rushwa.
Kuna wakati niliwahi kwenda kuangalia mechi kati ya Yanga na Simba,basi nikakata tiketi ya 15,000 lakini pale jukwaani nilipokaa,asilimia kubwa ya walionizunguka ni wale waliokuwa na tiketi za 3,000 na kinachofanyika wanatoa hongo ya sh 1,000 kwa maaskari then wanaruhusiwa kukaa jukwaa la 15,000.Hivyo hivyo na jana ndio utaratibu uliokuwa ukifanyika,waziwazi kabisa!Hivi hili TFF hili hamlifahamu?

2: Usafi wa viti na vyoo!
Nimekuwa nikijiuliza maswali bila kupata majibu,hivi zile hela zinazokatwa kila mechi kwa ajili ya uwanja zinafanya kazi gani?Nimekuwa nikihudhuria mechi pale taifa mara nyingi sana lakini kila siku mambo ni yale yale,viti vichafu,vyoo vichafu sana kupindukia.Jamani hela tunayotoa kama viingilio ni kubwa sana hizo huduma za usafi zifanyike,na kama kuna watu wanachukua hizo hela za usafi wakati usafi haufanyiki wawajibishwe.

Najua wahusika wamo humu JF,wayafanyie hayo kazi.Pia wale waliokuwa uwanjani jana na wale wenye uzoefu na uwanja wa taifa karibu tuchangie!

ya ngoswe mwachie ngoswe..
 
ya ngoswe mwachie ngoswe..

Mkuu hivi ni kweli kuwa Simba waligoma kuingia uwanjani Mboka Manyema mpaka walipoahidiwa droo?

flat,550x550,075,f.jpg

Simbakoko SC

VS

Rhino

furious_rhinoceros_angry_rhino_comic_design_mousepad-re03fd88baa574579ba5e22b9ea0e0ed3_x74vi_8byvr_512.jpg
 
ya ngoswe mwachie ngoswe..

Hatuwezi kuwaacha tusilalamike,unalipa kiingilio ukitegemea utakuta viti visafi na huduma kama za vyoo pia ni nzuri.Hata baa/hoteleni huwa nikikuta vyoo vichafu au huduma yoyote hairidhishi basi huwa namwita meneja na kumpa taarifa
 
Napenda kuwapongeza wachezaji,wanachama na mashabiki wa Yanga kwa ushindi wa kishindo wa goli 5 kwa 1.

1: Ukaguzi wa tiketi na rushwa.
Kuna wakati niliwahi kwenda kuangalia mechi kati ya Yanga na Simba,basi nikakata tiketi ya 15,000 lakini pale jukwaani nilipokaa,asilimia kubwa ya walionizunguka ni wale waliokuwa na tiketi za 3,000 na kinachofanyika wanatoa hongo ya sh 1,000 kwa maaskari then wanaruhusiwa kukaa jukwaa la 15,000.Hivyo hivyo na jana ndio utaratibu uliokuwa ukifanyika,waziwazi kabisa!Hivi hili TFF hili hamlifahamu?

2: Usafi wa viti na vyoo!
Nimekuwa nikijiuliza maswali bila kupata majibu,hivi zile hela zinazokatwa kila mechi kwa ajili ya uwanja zinafanya kazi gani?Nimekuwa nikihudhuria mechi pale taifa mara nyingi sana lakini kila siku mambo ni yale yale,viti vichafu,vyoo vichafu sana kupindukia.Jamani hela tunayotoa kama viingilio ni kubwa sana hizo huduma za usafi zifanyike,na kama kuna watu wanachukua hizo hela za usafi wakati usafi haufanyiki wawajibishwe.

Najua wahusika wamo humu JF,wayafanyie hayo kazi.Pia wale waliokuwa uwanjani jana na wale wenye uzoefu na uwanja wa taifa karibu tuchangie!

Toba jamani....nawapa pole nyie mnaoshabiki mpira wa kibongo mpaka leo hii 2013 bila ya kuwa na maendeleo yeyote. Mpira wa kibongo ukisema uufuatilie haki ya nani utajiua kwa hasira. Si mashabiki wala wachezaji kila mmoja ni msanii na ndiyo maana hakuna maendeleo yeyote ya mpira hapa Bongo, ni upuuzi tu uliokithiri, kila mtu toka wachezaji, viongozi, na mashabaiki wanachakachua mpira wa kibongo. Nasema, kwa mtajii huu....hatutaendelea ng'ooooooooo!
 
Napenda kuwapongeza wachezaji,wanachama na mashabiki wa Yanga kwa ushindi wa kishindo wa goli 5 kwa 1.

1: Ukaguzi wa tiketi na rushwa.

2: Usafi wa viti na vyoo!

Najua wahusika wamo humu JF,wayafanyie hayo kazi.Pia wale waliokuwa uwanjani jana na wale wenye uzoefu na uwanja wa taifa karibu tuchangie!
sungura1980

Ushahuri tu ndugu yangu Next time ukienda kaa kw ambali kidogo na jaribu kurecord Video na ukishindwa hata picha hao wanopokea Rushwa live na uje ubandike hapa live tuone kama hatua hazijachukuliwa.

Kuhusu Vyoo hivyo hivyo video na Picha ukilete hapa naamini wikiend ijayo ukienda tena utakuta kila kitu safi.

Ni hayo tu ndugu yangu!
 
We unataka tukale wapi?? Mxxxxx!!!

Picha za vyoo nitaleta siku nikienda tena ingawa sina hamu tena kwa kweli,lakini za hao wanaopokea rushwa sileti ng'o,nayapenda meno na kucha zangu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom