Nilichokiona jana kwenye Wasafi Festival 2018

Madimba jr

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
1,577
3,143
1. Wasanii amabo tulikuwa tunaaminishwa kwamba hawana uwezo ndio wanaweza sana kupiga show na amsha amsha nyingi sana nimeziona kwa Dudu, Dully, Country, Moni, Nikki, Killer, incredible, stereo, Catrina, Makaveli na wengine wengi kifupi wamepokelewa vizuri sana

2. Watu wa mikoani wanapenda sana burudani na hata show za ukweli kama jana ziwe kila Jumamosi watajaa tu

3. Wasafi wamejipanga sana stage imetulia, muzik system imeshiba na hakuna ile ya mic kukata kata

4. Serikali inapenda sana mapinduzi ya burudani na inawapenda sna WCB licha ya figisu wanazopitia baina ya Basata na WCB lakini Naibu waziri Shonza na Mngereza wa Basata wote walikuwepo kutoa sapoti na kula bata Nangwanda

5. Nyimbo za zamani bado zinasound sana na mashabiki wanazipenda kuliko maelezo,ni wakati sasa wasanii wakongwe waamke waache kulialia njaa

6. HipHop ni tam sana kwa stage na zinaamsha sana

7. Dj Ommy Crazy anajua sana tena sana,sema tu ndo anakosa nafasi za kuonyesha uwezo wake,ila anatakiwa apunguze mizuka na kukata kata nyimbo wakati zishachanganya

8. Muziki wa Singeli bado unakubalika sana ukipigwa wahuni wote wanaamka kwa shangwe "viroba tupa kule sasa ni mwendo wa.....#pespi

9. Harmonize ni msanii atakaye chukua nafasi ya Diamond miaka michache ijayo nyimbo zake nzuri sana kwa steji watu wamezipokea kwa hamasa mno na anajua kuimba live.

10. Vijana wa WCB wazuri sana stajini nadhani wamekuwa trianned vyema sana jinsi ya kucheza na audience heko kwa Lavalava,Mbosso,Vanny Boy,Darleen,Konde Boy

11. Navy Kenzo are so good kwa show na ngoma zao haziboi ila wanatakiwa kidogo wapate kujua kucheza na jukwaa wanaweza kujifunza kutoka kwa Chibu D

12. Diamond ni Mzuri sana tena sana kwa kuimba live na sauti yake iko so perfect kwa live Band,ana pumzi sana nashangaa sijui kwa nini hapendagi kuimba Live huyu kijana.

13. Team WCB wameweza na wakiendelea kushikamana tamasha lao litakuwa kubwa sana,kikubwa waboreshe maslahi na wasilewe sifa wakanza ubabaishaji

14. Wanachotakiwa sasa hivi wachukue na wasanii wengine ambao wanaonekana kuside na mahasimu wao,hiinitawasaidia kuonyesha hawana kinyongo na mtu na kuongeza love na kujiongezea mashabiki.




BADO SANAAAAAA

Diamond Show kapiga kuanzia saa 03:30 hadi 05:21
Kapiga ngoma 31 ( 36, 2, 3, 18, 43, 44, 4, 6, 7, 8, 11,13,14,16, 25, 27, 28, 33, 34, 37, 38, 45, 46, 51, 47, 30, 31, 35, 49, 50, 39) kutoka kwenye playlist yake aliyotupostia instagram.

Katumia mfumo wa kupiga playback na band pamoja na wacheza show.

1. Band ilipwaya maana drumer alikuwa juu ya mziki wote drums zinasikika kuliko mziki wote(kisayansi na hisabati za muziki)

2. Wasanii wa Hip Hop bado wamekuwa wageni wa stage( effect ya kubaniwa big stages) hawakujua watu wanataka nini.

3. Kumchukua Dudu baya kutawaangusha Wasafi kwani dudu baya hamna alichofanya. Maneno mengi sana hana kazi wala bazi

4. Moni centrazone na Country boy wameonyesha uzoefu wao wa big stages (fiesta effect)

5. Hawakuwa na stage planner mzuri(kuna gapes kibao stage...kabla ya show na show na stage ipo chini hadi washabiki wanapanda stage.

6. Wasanii wa wasafi hawana uzoefu wa show especially show kubwa...(fiesta effect)

7. Band ya wasafi haina back vocalists wala formation ya band professional.

8.Harmonise anaipa nguvu Theory yangu kuwa akipatikana mastermind kama Ruge akamtengenezea Harmonize channel, Diamond hamuwezi Harmonize...Harmonize alitulia stage akacheza na mashabiki...akawaambukiza ile energy yake bila kuwambia piga keleleeee

9. Navy Kenzo bado wageni wa stage kubwa. Hapo ndio utaona tofauti ya wasanii wa club na wasanii wa big stage kama Country Boy na Moni.

10. Mboso peke yake ndiye alitakiwa kuimba na Band hasa ukizingatia uzoefu wake wa stage kubwa na kuomba kwenye team aliotoka nao Yamoto band na ufundi wake wa kupiga chombo.

11. Mboso, Ray Vanny na Lava Lava walitakiwa kufanya back vocals wakati wa show ya Diamond hiyo ndio definition ya team sio kuwajaza kina Tale na Fela na Salam kwenye stage na watu wengine wasio wasanii. Stage ni Ofisi ya msanii sio ofisi ya manager wala mpiga picha wala baunsa, wala kumpandisha Steve Nyerere na kina Aunt Ezekiel ni format ya zamani ya show iliyotumiwa na Fiesta. Show haikuwa na ubunifu wa stage picture, light wala projection ya picha inayoeleweka.

Stage ilikosa Theme na MC (Jonijoo) alitakiwa kuhost na yule mwanamke mwengine ila asimpe nafasi hata ya kuwa co host... Fela anaingia kila mara na kuwashika wasanii begani huku akiwapa maelekezo fulani maanake anaonyesha stejini yeye ni Boss.


Heko sana Wasafi Festival jana Ntwala kulinoga sana watu wamefaidi na wameridhika na buridani mliyowapatia,ila next year jaribuni kufix ratiba yenu isiendane na msimu wa mvua kwani matamasha haya yatakuwa yanafanyika kwenye outdoor grounds
 
Nmekesha nao kwa TV mpaka asubuhi....they did their best kwa kweli,,,,lkn Harmonize kiboko yule jamaa though ilikuwa ni home ground lkn kwangu huyo ndo alikuwa man of the match
Siku zote nasemaga huyu dogo ....atamuacha Diamond by far......yaani atamfunika .... style ya Mond na Hamo....hazitofautiani sana....but Hamo....yupo vizuri sana kuliko Mond....
 
nilishangazwa sana nimeacha leo kuongea sana juu ya hilo sababu ukimgusa diamond unaambiwa una wivu,harmonise alijitahidi sana,ila tamaduni wameniangusha overrall sound na perfomance zilikuwa hovyo ,PLAYBACK?halafu inaonekana wengi walikuwa wamelewa kabisa,mara mikono juu,dj ommy crazy subiri kidogo,,,ah siyo hiyo ngooma bana...dah hta rayvanny kalipua tu ,warekebishe bana,kama sio liveband basi walazimishe wasanii waimbe na BEAT CHORUS...playback iwe chorus tu ,verse waimbe live.
 
Hizi matamasha zimekaa poasana, tatizo nipale figisu zinapotaka kuvuka mipaka.
 
Hahahhhahahaaaaa
20181125_073606.jpeg
 
Mkuu diamond lile jini alitabiriki konde boy bado kinda sana kwa chibu Ana mengi ya kujifunza bado
Dogo ame-mcover Diamond kwa muda mfupi....2 to 3 yrs to come.....Mungu akitupa maisha tutakuwa tunazungumzia habari nyingine....
 
Ninachosikitika tunatengeneza wanamuziki wengi sana ila tunashindwa kuwatengeneza wakina Ruge wengi ambao ni mastermind, mainnovator magamechanger so sad kwa kweli kwa afya ya industry yao anyway show kwa kuwa ni ya kwanza ilikuwa poa sana
 
Back
Top Bottom