Nilichokiona Fiesta Kahama.. Ujinga ujinga tuu

Nilichokiona Fiesta Kahama.. Ujinga ujinga tuu

Sambusa kavu

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2015
Posts
811
Reaction score
1,311
Kwanza nianze kwa kukiri kuwa sina maslahi na upande wowote ule wa hii tasnia ya muziki,bali nikiwa kama mwananchi wa kawaida nilielipa 10,000 siku ya jana kushuhudia Fiesta ya Kahama.Burudani niliyojiwekea akilini kuwa may be ningeipata kwa wasanii waalikwa sikuipata hata kidogo.Shukrani sana kwa Sholo mwamba,man fongo na Msami,hawa tu ndio walinipoza hasira yangu na kunifanya niende kulala kwa Amani..ntajaribu kuchambua kwa kile nilichokiona kwa msanii mmoja mmoja ili angalau wajirekebishe sehemu zingine watakapoenda…

RAYMOND WA WCB
Alikuwa flop of the night..watu walitegemea kuona makubwa sana kutoka kwake lakini show aliyopiga ujinga ujinga tuuu…kwanza jamaa ni very predictable,habadiliki,alichokifanya mwanza ndicho alichokifanya kahama na naamini ndicho atakachofanya na sehemu nyingine pia.wakati wa show ana mistari yake anayopenda kuisema,yaan ni iyo iyo tu tangu kipindi kile yupo kama back vocal artist wa Madee mpaka leo msanii wa kujitegemea bado anaitumia iyoiyo,hajui kuwa wapenda burudani tumeshaijua na tumeikariri pia..kanichekesha Zaidi pale nilipoona kuwa hata nguo alizovaa Mwanza ndizo alizovaa Kahama.

NANDY
Upcomimg artist but alinikosha kwa alichokifanya na live band,alipiga show nzuri,she knows how to dance,ana pumzi na swaga pia anazo

MAUA SAMA
Huyu bora hata angeimba playback tu,alijifanya kuimba live matokeo yake mpaka nikamwonea hururma,full kuboronga mpaka nikamuonea huruma

JUX, CHRISTIAN BELLA,BONGE LA NYAU, BILLNAS
Walipiga show ya kawaida sana,hata billnasi sikutegemea show mbovu vile kutoka kwake

DARASA NA MR BLUE
Walijitahidi kidogo,walipata shangwe na walikuwa wakiimba pamoja na mashabiki

SHOLOMWAMBA
Kuna wakati nilitaka kusinzia,lakini niliamshwa na shangwe za watu pale tu waliposikia ‘ooooiii babaaaaaa’..jamaa alipiga show nzuri sana watu walienjoy na kucheza pamoja,sikuamini kuwa hata wasukuma wanaukubali mziki wa kisingeli namna ilee

JOH MAKINI
Huyu jamaa ni mwamba kweli,alipangwa kuwa msanii wa mwisho kuperform ili awe funga kazi kwa amsha amsha za kihiphop,hali haikuwa ivyo kama waandaaji walivodhani maana alipata shangwe kidogo tu kutoka kwa wananchi,wengi wao walikuwa wameshaondoka na wengi zaidi walikuwa mbali na jukwaa kutokana na kuwepo kwa vumbi jingi sana lililokuwa limetimuliwa na watu kwa kucheza mziki wa msanii(MAN FONGO) aliyetoka jukwaani mda mfupi kabla ya Joh Makini kupanda

MANFONGO
Nawashauri waandaaji wa Fiesta popote waendapo,kama Man fongo atakuwepo basi awe msanii wa mwisho kabisa kuperform,jamaa alipiga bonge la show,uwanja mzima ukawa kama vile tupo Syria,vumbi lilitimka,mpaka watu wakawa hawaonani,ikawa kama vile inanyesha mvua ya mchanga,mwisho watu wakaanza kukimbia mbali na jukwaa,kwa shangwe na hamsha hamsha aliyofanya ilibidi jamaa akatishe show kabla hajamaliza ndipo akapanda Joh Makini

MSAMI BABY
Nikiri tu wazi,kwa kiingilio changu cha sh 10,000 Msami pekee alinifanya nione hela yangu imeenda kihalali..Jamaa alipiga show ya Live,no playback,mchizi ana pumzi,energetic,zile choreograph na madancers wake daaamn…alishangiliwa na uwanja mzima,watu walienjoy mwanzo mwisho..ndo msanii pekee aliyeperform mda mrefu kuliko wengine wooote…kama uongozi wa Fiesta utakuwa unamlipa hela sawa na wasanii wengine basi itakuwa ni unyonyaji wa dhahili kabisa…nadiriki kusema kwa wasanii wanaoweza kupiga liveshow jamaa anaongoza Tanzania nzima..BIG UP KWAKE.
 
Fiesta ni moja ya chanzo cha maambukizi ya ukimwi
tumekusikia tutapeleka ombi kwa waandaaji wagawe mipira wakati wa kuingia uwanjani, sasa sijui tutawaelekezaje vijana maana wakicheza muziki wanabambia na kunawa kwa hiyo wavae vidoleni?
 
Fiesta ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000
Hapo mmetoroka shuleni, mnamuona msanii km ngwea, tid, prof jay, mandojo na domokaya
Hapo mchozi yanawatoka kwa furaha

Siku hizi ujinga tu huko
 
tumekusikia tutapeleka ombi kwa waandaaji wagawe mipira wakati wa kuingia uwanjani, sasa sijui tutawaelekezaje vijana maana wakicheza muziki wanabambia na kunawa kwa hiyo wavae vidoleni?
1472318098039.jpg
sio utani....... Ila km waona ni utani waambie wavae km huyo bibi
Sio vidoleni tu
 
daah kaazi kweli kweli, kichwa cha habari kimewaponda,
Halafu content imesifia wasanii wengi, na wengi huwa wape
 
Nasikitika kama Jux hajaperform vizuri maana ngoma ya WIVU ni Rnb ya mwaka hapa bongo , na itachukua muda sana wasanii kuifunika hii rnb
 
Hahahaa! Watu wa mikoani bhana... utasikia, "Oh, hiyo Singeli itabamba huko huko kwa Wanaume wa Dar... muziki gani huu!" Hadi sasa ishadhihirika Wasukuma mnashikwa mmoja baada ya mwingine... tunasubiri feedback kutoka kwa "wagumu" wa A-City sasa!!
 
Hapo wasanii nnao wafahamu hawazidi watatu, kweli nimezeeka sasa
 
Mambo kama haya wakati nipo kijana ndio nilikuwa muhudhuliaji mzuri ila niliacha baada ya kuwa Kila show unayoenda hakuna kitu kigeni
 
chid benz watamuweka lini..? hili jamaa napenda linavyofloo na ile besi yake dah!
 
Back
Top Bottom