Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

happy amos

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
251
434
Siku zote nimekua nikilalamika humu mme/mwenzangu kutohudumia nyumbani na kuhamishia nguvu kwao ila nilichokiona mpaka nimemuonea huruma.

Iko hivi mimi na mwenzangu tulikua tunaishi pamoja tangu mwaka Jana mwaka huu wazazi wakaamua wakamilishe taratibu zote ikabaki ndoa tu sasa katika maisha na mwenzangu wajibu wake ndani umekua mdogo maendeleo hakuna hafanyi.

Nimeenda kwao likizo nimechoka mwili na roho nimepoteza ndoto za kua na maisha mazuri kabisa jamaa ukoo mzima iwe shangazi, mjomba,Dada zake hata walioolewa yeye ndio anawahudumia.

Nimemuonea huruma maana sio ombi nilazima familia ile dada zake wavae aanunulie nguo kila siku ikifika mwisho wa mwezi hela zote zinaenda kwao ikifika tarehe 10 mshahara umeisha nilikua nachukia namuona hana akili za maendeleo lakini kwa hali nilivyoiona hata yeye hana jinsi.

Jamani nishauri nifanyeje tue na maendeleo na sisi? Sababu kipato changu ni lak 3 binafsi mwenzangu yeye anapokea mil 1.4_5 lakini majukumu ni mengi kwao hawezi kufanya chochote.

Nifanyeje jamani?
 
Dhaaa........huo nao ni upofu, yaani mtu umesota kusoma umepata kazi kisha unaanza kununulia nguo dada zako, hii ndio akili gani sasa. Jambo analopaswa kufanya ni moja tu. Aachanr na familia na ashughulike kwa kiasi tu na baba na mama yake pekee kwa kiwasaidia makazi bora chakula wapambane wenyewe. Hao ndugu wapambane na hali zao tu. Hiyo lazima kuwasaidia imewekwa na nani. Otherwise mtayumba sana na huyo mwanaume asiye na msimamo
 
Kupanga ni kuchagua hata sisi hatujatoka kwny familia nzuri ila unafanya kitu kutokana na uwezo wako...mm huwa natoa msaada kwa watt ambao wazazi wao wamefariki haswa linapokuja suala la ada huwa kama ndugu tunachangia kwa anayeweza.

Issue ya kumnunulia shangazi mpk chupi sitikuja kufanya mpk nakufa kila mtu apambane na maisha yake tu
 
Kama mnaishi karibu na nyumbani ni bora kwanza kufikiria kuishi mbali na nyumbani, ikiwezekana hata kuhama kanda hio ambayo ni karibu na kwao na kuhamia kanda nyingine kabisa.

Halafu ahakikishe anaseti bajeti ya si chini ya laki nne tu kwa mwezi kuwatumia wazee wake kijijini, hapo atapata maendeleo.

Vinginevyo atasumbuka na watu sana, siku akiyumba kiuchumi hao hao watageuka kumcheka tena.
Dunia ya sasa inabidi kuishi kwa akili sana hasa na ndugu.
 
Dhaaa........huo nao ni upofu, yaani mtu umesota kusoma umepata kazi kisha unaanza kununulia nguo dada zako, hii ndio akili gani sasa. Jambo analopaswa kufanya ni moja tu. Aachanr na familia na ashughulike kwa kiasi tu na baba na mama yake pekee kwa kiwasaidia makazi bora chakula wapambane wenyewe. Hao ndugu wapambane na hali zao tu. Hiyo lazima kuwasaidia imewekwa na nani. Otherwise mtayumba sana na huyo mwanaume asiye na msimamo
Hapo aachane kuwahudumia hao dada zake maana hao wanaweza jimudu kama kuna watoto wa kiume awatafutie mtaji au shuguli za kufanya baada ya hapo kila mtu afanye yake ukiendekeza ndugu lazima ufe masikini
 
Kupanga ni kuchagua hata sisi hatujatoka kwny familia nzuri ila unafanya kitu kutokana na uwezo wako...mm huwa natoa msaada kwa watt ambao wazazi wao wamefariki haswa linapokuja suala la ada huwa kama ndugu tunachangia kwa anayeweza.

Issue ya kumnunulia shangazi mpk chupi sitikuja kufanya mpk nakufa kila mtu apambane na maisha yake tu
Nilichogundua jamaa hana jinsi hata ya kujitetea kila kitu anakubali,,, kuna dada zake wametoka kwa wame zao wamekuja kusalimia wakamwambia hatuna nauli ya kurudi wala hatuna cm za mawasiliano jamaa katoa hela kawapa......na nguo kawaliwanunulia. , jamaa hana cha kujitetea
 
Shida haziishi dada yangu.Kuweni na mipango.Mfanye mambo yenu ya maendeleo pamoja na kusaidia wengine.Msisahau kuweka akiba pia.

Kupanga ni kuchagua.

Uko sahihi kabisa.....maisha yao hayatakiwi kusimama...
 
Nilichogundua jamaa hana jinsi hata ya kujitetea kila kitu anakubali,,, kuna dada zake wametoka kwa wake zao wamekuja kusalimia wakamwambia hatuna nauli ya kurudi wala hatuna cm za mawasiliano jamaa katoa hela kawapa......na nguo kama kawaliwanunulia. , jamaa hana cha kujitetea

Aaah...kwingine akaze sura sasa...simu?!
 
Shida haziishi dada yangu.Kuweni na mipango.Mfanye mambo yenu ya maendeleo pamoja na kusaidia wengine.Msisahau kuweka akiba pia.

Kupanga ni kuchagua.
Sasa nifanyeje? maana mwenzangu yeye dizain kama anawaogopa wazazi
 
Ulicho kiona ndio maisha halisi ya familia ya Mme wako

Unacho paswa kujua nikuombe tu naomba jifunze kuwekeza vitu vidogo vidogo kutokana na mshara wako

Hii itakusaidia kufikia uchumi wa kawaida

Ukianza kuwekeza kwa pesa kidogo unaweza kufikia malengo

Swali utakalo jiuliza nawekezaje?

Hapa nikuombe kama uko tayari kujifunza kuwekeza basi useme unapenda kuwekeza kwenye nini ili upate ushauri sawa na wazo lako
 
Nafikiri una machaguo mawili tuu
1. Umuache
Hii ni kama unahisi huwezi kuprosper nae kiuchumi kwa mawazo yako yanavo kutuma juu ya mzigo alio nao.

2. Usimuache

Kwa kuwa umeona hali halisi ya ukweni , kaa naye ongea naye kwa kirefu na kwa kutoa mapendekezo juu ya nn mkifanye ili maisha yenu yawe sawa pasipo kuathiri harakati za kuwasaidia hao ndugu zake, coz hujui hao wamemtoa wapi na wamemsaidiaje hadi kufika hapo alipo na kukukutana na ww hivyo huwezi ukamwambia aache kuwasaidia,
Namna nzuri ni kupanga mipango ya kuanzisha kitu ambacho kitakuwa kinawasaidia hao ndugu zake kujisimamia ( kama unampenda kweli huyo jamaa ako ) Pasipo kumtegemea jamaa ako .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom