Nilichokigundua katika Upilato wa TCU ni kwamba.....

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Wengi wa Wanafunzi ama waliopo au hata wale waliomaliza kusoma Vyuo Vikuu na sasa wapo Makazini ni kwamba hawakupitia mfumo wa Elimu uliozoeleka ambao ni wa kumaliza Form Four kisha kwenda Form Six kisha kufaulu vyema na kujiunga Vyuo Vikuu na kwamba wengi wa waliotajwa katika Orodha ya Kipilato ya TCU ni wale ambao walifeli Form Four kisha wakaenda kujiunga na Vyuo hivi vidogo vidogo ambapo kuna waliofanya Kozi mbalimbali kwa ngazi ya Certificate na Diploma ili wakishamaliza miaka yao mitatu basi wawe na Sifa za kujiunga Chuo Kikuu.

Nimeligundua hili baada ya kuipitia kwa umakini sana hiyo Orodha na kwa bahati nzuri kuna Wanafunzi kadhaa wa Vyuo vyetu hivi vidogo vilivyo chini ya NACTE ambao nawajua walipitia hizi Kozi ndogo ndogo za hapa na pale kisha wakapata Certificates na Diplomas zao ambazo walizitumia kuombea kusoma Degree huko Vyuo Vikuu.

Kwa mtazamo wangu hapa nadhani wa kulaumiwa siyo hawa Wanafunzi bali ni TCU wenyewe na hasa hasa ile Central Admission System yao na kama ikiwezekana nadhani ipo haja ya hawa Wanafunzi wote waliopilatiwa na TCU waende Mahakamani wakaifungulie Kesi TCU kwani kiukweli Kitendo chao walichokifanya kimewachanganya na kuwaharibu Wanataaluma wengi psychologically na ni hatari sana.

Na kinachonishangaza hata Waziri husika amekaa kimya mno wakati nilijua kama Mdau namba moja angelitolea hili ufafanuzi mzuri sana kutokana na kwamba kuendelea Kwake kuwa Kimya si tu kutawaathiri hao Wanafunzi au Wazazi / Tegemezi wao bali kimsingi hii kitu itaathiri kwa kiasi kikubwa hizo Taasisi nyingi za kutoa Elimu ya Juu nchini ( Vyuo Vikuu ) na si kitu kizuri kwa afya ya Kitaaluma kwa nchi yetu.

Nilichokiandika hapa ni mtazamo wangu tu ila nitafurahi pia ukikosolewa kwa hoja ili wote tuweze kufaidika Kimaarifa na pia tuweze kuwasaidia wale ambao sasa hawajui nini cha kufanya. Hii ni kitu Nyeti hivyo nawaomba tuijadili kwa Unyeti wake ili hata watakaokuja humu wapate na watoke na kitu.

Nitawashukuruni na karibuni katika kulijadili hili intellectually zaidi ILA niwatie tu moyo wale wote waliopatwa na hii kadhia kuwa wasiogope wala kukata tamaa Mwenyezi Mungu yupo na haki yao itapatikana na zile ndoto zao za wao pia kuwa Wasomi wa nchi hii zitatimia cha msingi wawe na subira.
 
Hivi mkuu Gentamycine haya ni mapya kwako?
Watu walipokuwa wanalalamikia hii mifumo ninyi mlikuwa mnawatetea sana watawala (Mlijitoa Ufahamu).

Nakumbuka wewe bwana mdogo ulidiriki hadi kutoa kashfa kwa vyuo hivi vidogo na kuwaita MAPOPOMA. Leo nashangaa huu Huruma wako kwa hawa wanafunzi uliowaita MAPOPOMA umetoka wapi?
 
Hivi mkuu Gentamycine haya ni mapya kwako?
Watu walipokuwa wanalalamikia hii mifumo ninyi mlikuwa mnawatetea sana watawala (Mlijitoa Ufahamu).

Nakumbuka wewe bwana mdogo ulidiriki hadi kutoa kashfa kwa vyuo hivi vidogo na kuwaita MAPOPOMA. Leo nashangaa huu Huruma wako kwa hawa wanafunzi uliowaita MAPOPOMA umetoka wapi?
Mkuu,nami imebidi nishangae kwa bandiko hili na kujiuliza mara 3 kama kweli huyu ni Genta,maana hata uandishi si "Genta style". Hata hivyo ubinadamu unakamilishwa na kuwa na "guilty consience".
 
Back
Top Bottom