Nilichogundua teuzi za Rais Magufuli

Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,733
1,645
Habari wana-JF
Mhe. JPM mara nyingi hufanya teuzi mbalimbali akiwa anachagua wasomi,wahadhiri na wanataaluma.

Mfano jana kamteua "nguli wa sheria kuwa mbunge"(kwa mujibu wa gazeti la mwananchi). Nilichogundua ni kuwa anachagua watu wa aina hii kama njia ya kujihami kwa sababu zifuatazo;

1. Hawa wasomi anaowachagua hawawezi kupingana na bosi wao hata ikitokea kakosea mambo.

2. Kuwanyamazìsha watu wasiweze kuhoji pale inapoonekana jambo limekosewa na Mhe. maana utaambiwa mbona akina fulani ni wasomi wamesema mambo yako sawa.

3. Kuonyesha kuwa anajenga serikali ya wasomi ambao wanaamua masuala ya nchi kitaalamu jambo ambalo si kweli tunaona mambo mengine yanaamulia kinyume mfano uvunjaji wa katiba
 
Mkuu zamani hata mimi nilikuwa nawaamini wasomi ile mbaya. Lakini nilivyoonza kuona mikataba ya kipuuzi kwenye raslimali zetu, makumpuni kibao kufa mikononi mwa wasomi , basi tokea hapo nawadharau wasomi ile mbaya. Kitu kingine kinachonifanya kuwadharau wasomi wengi, unakuta mtu ni msomi lakini maisha yake yote yanategemea ajira, akikosa ajira hata wazo la kufungua mradi wowote hana. Ukitaka kucheka mkabidhi mradi ausimamie, mpe miezi sita tu huo mradi utakuwa duni au hoi kabisa.
 
Habari wana-JF
Mhe. JPM mara nyingi hufanya teuzi mbalimbali akiwa anachagua wasomi,wahadhiri na wanataaluma.

Mfano jana kamteua "nguli wa sheria kuwa mbunge"(kwa mujibu wa gazeti la mwananchi). Nilichogundua ni kuwa anachagua watu wa aina hii kama njia ya kujihami kwa sababu zifuatazo;

1. Hawa wasomi anaowachagua hawawezi kupingana na bosi wao hata ikitokea kakosea mambo.

2. Kuwanyamazìsha watu wasiweze kuhoji pale inapoonekana jambo limekosewa na Mhe. maana utaambiwa mbona akina fulani ni wasomi wamesema mambo yako sawa.

3. Kuonyesha kuwa anajenga serikali ya wasomi ambao wanaamua masuala ya nchi kitaalamu jambo ambalo si kweli tunaona mambo mengine yanaamulia kinyume mfano uvunjaji wa katiba
Mkuu katika mambo yaliyochangia katika kuchelewesha maendeleo yetu ni siasa kuchanganyika na taaluma.

Unakuta mbunge msomi yupo ndani ya ukumbi wa mkutano akiwa na diwani au mwenyekiti wa serikali za mitaa ambaye ni darasa la saba. Zamani hali hii ilizoeleka kwa sababu wasomi wenye shahada kubwa walikuwa ni wachache.

Kama unao watu wenye PHD kwenye fani mbalimbali, kwa nini usiwape uhuru wa kuuweka ubunifu wao kwa vitendo kupitia vyeo vya uwaziri, unaibu na ukatibu mkuu wa wizara?.

Kwanini uendelee kuwa na rundo kubwa la watu wenye elimu za kawaida kwenye vyeo vya juu wakati unaweza kuwatumia wanataaluma waliopo nchini?. Na wanasomeshwa kwa fedha nyingi ili ujuzi wao uwe na tija kwa taifa lao.

Wewe mleta mada umemezwa na tabia ya malalamiko na kujiona mnyonge kwenye kila jambo. Achana na hiyo inferiority complex, waache wanataaluma wachape kazi.
 
Hawa wazee wangu wasomi, huwa nawaoneaga huluma sana siku wanapokutana na mkasi live wa utumbuaji majipu.
Utasikia kuanzia leo namsimamisha kazi Dkt.......... au Prof .........., kwa kutolizishwa na utendaji wake..
 
Habari wana-JF
Mhe. JPM mara nyingi hufanya teuzi mbalimbali akiwa anachagua wasomi,wahadhiri na wanataaluma.

Mfano jana kamteua "nguli wa sheria kuwa mbunge"(kwa mujibu wa gazeti la mwananchi). Nilichogundua ni kuwa anachagua watu wa aina hii kama njia ya kujihami kwa sababu zifuatazo;

1. Hawa wasomi anaowachagua hawawezi kupingana na bosi wao hata ikitokea kakosea mambo.

2. Kuwanyamazìsha watu wasiweze kuhoji pale inapoonekana jambo limekosewa na Mhe. maana utaambiwa mbona akina fulani ni wasomi wamesema mambo yako sawa.

3. Kuonyesha kuwa anajenga serikali ya wasomi ambao wanaamua masuala ya nchi kitaalamu jambo ambalo si kweli tunaona mambo mengine yanaamulia kinyume mfano uvunjaji wa katiba
Nahisi upo sahihi kbs
 
Mkuu katika mambo yaliyochangia katika kuchelewesha maendeleo yetu ni siasa kuchanganyika na taaluma.

Unakuta mbunge msomi yupo ndani ya ukumbi wa mkutano akiwa na diwani au mwenyekiti wa serikali za mitaa ambaye ni darasa la saba. Zamani hali hii ilizoeleka kwa sababu wasomi wenye shahada kubwa walikuwa ni wachache.

Kama unao watu wenye PHD kwenye fani mbalimbali, kwa nini usiwape uhuru wa kuuweka ubunifu wao kwa vitendo kupitia vyeo vya uwaziri, unaibu na ukatibu mkuu wa wizara?.

Kwanini uendelee kuwa na rundo kubwa la watu wenye elimu za kawaida kwenye vyeo vya juu wakati unaweza kuwatumia wanataaluma waliopo nchini?. Na wanasomeshwa kwa fedha nyingi ili ujuzi wao uwe na tija kwa taifa lao.

Wewe mleta mada umemezwa na tabia ya malalamiko na kujiona mnyonge kwenye kila jambo. Achana na hiyo inferiority complex, waache wanataaluma wachape kazi.
Usomi wa kukataa kile ulichokiandika kwenye PhD thesis yako?

Nchi yetu haijawahi kuwa na tatizo la wasomi kuwepo serikalini. Tatizo kubwa ni maCCM kutoheshimu na kufanyia kazi mawazo ya wasomi (haswa walio vyuoni). Siasa na siyo taaluma ndiyo inaendesha nchi hii. Kibaya zaidi maCCM yanatumia 'njaa' za wasomi kuwatumia wasomi wenye maslahi na matumbo yao kuliko kutumia bongo zao kwa manufaa ya taifa.
 
Back
Top Bottom