Na Abdallah Bulembo ni msomi aliyebobea au?Habari wana-JF
Mhe. JPM mara nyingi hufanya teuzi mbalimbali akiwa anachagua wasomi,wahadhiri na wanataaluma.
Mfano jana kamteua "nguli wa sheria kuwa mbunge"(kwa mujibu wa gazeti la mwananchi). Nilichogundua ni kuwa anachagua watu wa aina hii kama njia ya kujihami kwa sababu zifuatazo;
1. Hawa wasomi anaowachagua hawawezi kupingana na bosi wao hata ikitokea kakosea mambo.
2. Kuwanyamazìsha watu wasiweze kuhoji pale inapoonekana jambo limekosewa na Mhe. maana utaambiwa mbona akina fulani ni wasomi wamesema mambo yako sawa.
3. Kuonyesha kuwa anajenga serikali ya wasomi ambao wanaamua masuala ya nchi kitaalamu jambo ambalo si kweli tunaona mambo mengine yanaamulia kinyume mfano uvunjaji wa katiba
Mkuu hayo uliyoyaandika mheshimiwa JPM anayajua fika, ndio maana baraza la mawaziri la sasa limejaa PHD na Prof.
Lawama tu siku nzima bila ya kutazama mambo katika jicho positive, sio suluhisho la matatizo tuliyonayo.
Ona sasa! Wewe nawe ndiyo wale wanaofikiri kila asiyewapenda CCM ni UKAWA. Mimi naichukia CCM tu. Sijali hata kama CHAUMMA waongoze taifa hili, lakini si CCM.Halafu maCCM hayo hayo yakakupeni makombo, na hayo makombo ndio aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya UKAWA.
Mkuu, I couldn't agree more. Umemaliza kila kitu. Shukrani kwa haya uliyoyasema. Ubarikiwe.Msomi anaacha kuwa msomi pale anapochagua kufanya au kusimamia jambo nje ya kile alichosomea. Mfano msomi wa kemia akiwa rais kupitia kura huyo sio msomi tena wa kemia bali ni mwanasiasa. Ili ubaki kuwa msomi unatakiwa uwe independent, impartial, unbiased na uonyeshe transparency kwenye kazi zako. Haya yote yanapotea unapojiingiza Kwenye siasa au chama.
Nchi za wenzetu wamewatenga wasomi na siasa kwa kuwaundia taasisi ambazo kazi yake ni kuishauri serikali na vyombo vyote vya maamuzi pasipo kujali chama wala itikadi zao. Sisi hapa NMRI imekuwa ya siasa, Repoa/Twaweza imejaa wasomi-siasa, TANESCO hivyo hivyo, vyuoni maptofesa waliotakiwa waisaidie nchi pasipo upendeleo ndio kwanza wanaandika vimemo wateuliwe nafasi za kisiasa. Usomi sasa ni siasa sio taaluma nyingine. Mhadhiri akiteuliwa nafasi ya kisiasa anashindwa kujuwa kwamba taaluma yake ndio basi tena.
Tutapataje wasomi halisi na makini watakao ongoza maamuzi ya serikali endapo kila kitengo cha maamuzi mkuu wake anateuliwa na rais kutoka chungu cha wasomi? Kwa maneno mengine msomi aliyeteuliwa ukurugenzi wa taasi anapata wapi nguvu ya kuwa unbiased, transparent, impartial, na independent kwenye maamuzi yake na kazi zake? Vyuo vyetu vimegeuka viwanda vya makada sio wasomi.
Mkuu kwenye hilo aupo pekee kuna wapiga mbiu wa CCM wenye shughuli zingine za kupata mlo lakini wanajishughulisha na mambo ya CCM katika muda wao. Kuna baadhi yao pia nimewasikia kwa mara ya kwanza wanadhani kuna sababu ya CCM kukaa benchi kwanza.Suluhisho ni CCM kuondoka madarakani. PERIOD
Usomi wa kukataa kile ulichokiandika kwenye PhD thesis yako?
Sasa mtu mkweli muwazi na mtetea wananchi kama Kabudi anaenda kuingia kwenye serikali ya dikteta uchwara lengo lake likuwa kutesa kupoteza watu kutukana kufirisi uchumi wa nchi kuvunja sharia si ndio maajabu ya wasomi wa Tanzania hawawezi kusema hapana ndio maana mtu kama jaji Agustine akashikishwa koba la CCM na yeye akakubali hii inchi ni vituko
Kagame sio JpmMbona kwa Kagame anachukua wasomi karibia wote, hadi wengine anaazima kutoka UD?
Siwezi kukubaliana na wewe 100% kuna baadhi ya mambo kama mtu hajasomaa huwezi kumkabidhi mradi. Wasomi kuna mabo wanafanya vizuri na mengine wanafanya vibaya sana. Hasa siasa sidhani kama inatekelezeka kwa professionals, hawa wanatakiwa kufundisha wanafunzi vyuo vikuu.Mkuu zamani hata mimi nilikuwa nawaamini wasomi ile mbaya. Lakini nilivyoonza kuona mikataba ya kipuuzi kwenye raslimali zetu, makumpuni kibao kufa mikononi mwa wasomi , basi tokea hapo nawadharau wasomi ile mbaya. Kitu kingine kinachonifanya kuwadharau wasomi wengi, unakuta mtu ni msomi lakini maisha yake yote yanategemea ajira, akikosa ajira hata wazo la kufungua mradi wowote hana. Ukitaka kucheka mkabidhi mradi ausimamie, mpe miezi sita tu huo mradi utakuwa duni au hoi kabisa.
Nani amesema kagame ni JPMKagame sio Jpm