Nilichogundua kuhusu Arusha

Hivi ardhi ni ya serikali au mchaga??
 
Sema stendi ya moshi inaizidi ile ya arusha hapo tutakuelewa tu kwasababu stendi ya moshi ni kubwa kidogo ukilinganisha na ile ya arusha. Yaani ina segment mbili za magari ya ndani ya mkoa na mabasi ya mikoani. Lakini.siyo kuleta blah blah na dharau zako kuishusha stendi ya msamvu
 

Kweli stendi ya mabasi ya mikoani imepitwa na wakati. Sisi wakazi wa Jiji hili tunaishauri halmashauri ichukue uwanja uliokuwa wa manyesho ya biashara kusherehekea miaka 10 ya Azimio la Arusha ulioko Sakina na kuufanya stendi ili kuondoa msongamano wa magari katikati ya Jiji. Hicho kitakuwa kitega uchumi kizuri cha Jiji letu kwani kuna eneo kubwa hata kwa maduka ili wafanyabiashara wadogo wote wahamie hapo. Tatizo ni kuwa CCM walinyakua eneo hilo ingawa serikali ililinunua kwa fedha za kodi kutoka kwa wenyeji kwa ajili ya maonyesho hayo. Ni wakati muafaka Ba
raza la madiwani kupeleka maombi kwa rais afute hati ya CCM ili eneo lirejee serikalini kwa manufaa ya umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…