Nilichofanya leo Mlimani City

Nilichofanya leo Mlimani City

monaco

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
2,184
Reaction score
1,779
Habari wadau.

Leo majira ya Saa 8 mchana, nikiwa Maeneo ya Mlimani city napata mahitaji yangu Mara akatokea jamaa mmoja mwenye asili ya Asia, akiwa na kavaa nguo nyeusi juu mpaka chini na viatu na ndevu ndefu, begi mgongoni na camera mkononi.

Nikiwa pale maeneo ya game lango la kuingilia Game kulia kuna duka la nguo, mara akatokea huyo jamaa akaanza kupiga Picha Eneo la game kwa mbele, kisha akapiga Kwenye roof, pale Kwenye varanda ambayo watu wanapita kwa Juu kuna security camera jamaa akaipiga, kisha akapiga na sehemu za Dari.... Mi namiangalia tuu,kisha akaingia duka la nguo lililo karibu pale.

Nikaondoka kwenda kumwambia Askari pale Kwenye duka la nguo,akasema nae amemuona Ila anamcheki kwanza.

Jamaa kaingia Kwenye Duka la nguo kaangalia nguo za watoto 2kisha kazirudisha, mimi bado namiangalia tu. Akatoka akaingia game ndani, ndipo nami nikaenda kwa Askari wa Pale mlangoni game nikamueleza tukio zima, nikamwambia jamaa mwenyewe ameingia humu ndani.

Akaniambia nae amemuona akiingia ndani, nikamwambia namtilia Shaka kwanini apige Picha Maeneo hayo nilioyataja awali? Akamuita mwenzake kwa Radio call akaja nikamweleza.

Jamaa akawa anatoka pale pale akamsimamisha na kumuhoji maswali yafuatayo:

Tafsiri ya kiswahili chini;

Kwanini unapiga Picha humu?
Umepata wapi idhini ya kupiga Picha?
Nioneshe hizo Picha - Askari akaziona kama nilivyomwambia, akakuta na nyingine za ndani.... akamwamuru a delete zote.

Jamaa akafuta na kusema alikuwa analinganisha duka hili la Hapa Tanzania na Afrika kusini, kwa sababu yanafanana.

Una kibali? Hapana.

Mwisho Askari akamwachia.

Mimi nikamfuata Askari nikamuuliza kwanini umemuachia? Akanijibu Kama angekuwa na Silaha ndo wangebidi wamkamate. So wakamwambia aondoke haraka eneo lile.

Jamaa akatoka akaelekea mpaka pale Exim Bank, halafu akaanza kutembea kama mtu mwingine kuelekea Bureau de Change, nilivomuona tuu, nikatoa simu yangu fasta nikaenda kwa mbele pale Bureau de Change kama nakuja anapotokea nikawa nampiga picha kwa ubavu, na kwa nyuma na huku kama tunapishana vile, akaingia Toilet.

Nami nimo nikaenda huko huko, kufika tukafika pamoja tukakuta wanachomelea Ila watu wanamaliza tuu haja zao, akaniuliza nikamjibu you can proceed, then nikaondoka...

Hivyo tuwe waangalizi wa nchi yetu.

ImageUploadedByJamiiForums1447178113.846668.jpg ImageUploadedByJamiiForums1447178149.333934.jpg ImageUploadedByJamiiForums1447178170.987055.jpg ImageUploadedByJamiiForums1447178203.772295.jpg ImageUploadedByJamiiForums1447178225.201820.jpg
 
safi sana,bila shaka kitengo cha IT pale makumbusho,watakuwa wamezipakua hizo picha kwa matumizi ya baadae.
 
hao askar gani? wa security au polisi? maana wewe ndo umeonesha kujali zaidi ya hao askari

Sio Polisi ni security wa Mlimani city,ningeenda Polisi nisingefanikiwa kumfuatilia!
 
Back
Top Bottom