Msandawe Halisi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 647
- 351
Ni mtoto ambaye alizaliwa kwenye ndoa. Nilihisi mapema toka siku ambayo amezaliwa, ila sikufanya chochote. Mtoto alizaliwa wa kike na ndio uzao wetu wa kwanza. Ukweli mtoto hakufanana na mimi kabisa wala mama yake. Nimemgundua baba wa mtoto wangu mwaka huu, kwa kweli wamefanana copy and paste.Ila wadogo zake 3 ni wa kwangu kabisa.Nimemsomesha mtoto sasa yupo chuo kikuu mwaka wa kwanza.
Baada ya mtoto kuzaliwa niliamini mtoto sio wangu siku hiyo hiyo namuona, nilimuomba Mungu anipe ustamilivi na ujasiri kushinda nafsi ya kumkataa, ukweli nilimpenda sana na mpaka leo nampenda sana, ananiita baba mimi namwita mwanangu, ila vijembe nilipigwa sana na ndugu jamaa na marafiki ila nilijiandaa kushinda kila kitu, sikuwahi kumuuliza mke wangu, ila mke wangu anahisi najua kila kitu.