Nikupigie goti kwani nakuomba nini

Nikupigie goti kwani nakuomba nini

Kwema wakuu.

Mke wangu mtarajiwa nimemwambia siku nakuvisha pete ya uchumba utapiga goti, kanijibu nikupigie goti kwani nakuomba nini? Hii imekaaje! Noamba kuwakilisha.
Nipe namba zake nimpe madini, asiwe hivyo
 
Kumpigia magoti mwanamke ni ishara ya kushindwa totally, kuvikana vikana pete ni umama, NB mwanaume kama umempenda mwanamke kamchukue mambo ya mahari,pete,sherehe waachie vijana wa daslamu. yaani kijana bado unajitafuta unataka ufanye sherehe ya nini sasa?
 
Ila Gen Z sijui mnafikiriaje, hata siwaelewi. Yani kujua hapo kuwa huna waifu material Hadi uambiwe na mtu?
 
Kuvalishana pete ni utamaduni wa wazungu ambao hauwezi kufanya kazi kwenye mazingira ya kiafrika ila unalazimishwa tu.
Sitafanya huo ujinga, nitapeleka wazazi wangu na washenga tutoe mahari tujitambulishe kisha nimepeleke mke nyumbani wamjue,
Mambo mengine kama pete, ndoa za kanisani na sherehe hayana msingi ni kufuata mkumbo
unataka wambea tukose cha kusimulia, sio vizuri bwana
 
unataka wambea tukose cha kusimulia, sio vizuri bwana
Hapana mkuu,
Mambo mengi vijana wanafanya ni kufuata mkumbo ila ukija kwenye uhalisia sio lazima kufanya
Wenye uwezo wakifanya sio tatizo ila changamoto ni pale ambapo watu wapo chini ya uwezo kisha wanalazimisha na michango mikubwa juu yake
Meaningless 💯
 
Haya ndo madhara ya kukopi utamaduni wa watu usioendana na mazingira yetu, kwani pete lazima mkuu? Kuna watu wanaenda kuvalishana pete Kanisani ambapo hakuna maswali ya nani anapiga goti au kama ni lazima sana valishaneni mkiwa wote mmesimama kuna wanaofanya hivyo na mambo yanaenda tu.
Hata hivyo ni kweli bebi wako akupigie goti anaomba nini mkuu? Huwezi kupiga goti wakati huna unachoomba.
 
swali zuri... mpe jibu la kwanini apige goti, au hata wewe hujui umekariri tu
 
Kwema wakuu.

Mke wangu mtarajiwa nimemwambia siku nakuvisha pete ya uchumba utapiga goti, kanijibu nikupigie goti kwani nakuomba nini? Hii imekaaje! Noamba kuwakilisha.
Maafa yamekuwepo tangu enzi na enzi pengine mara baada ya maisha kuanza kjwepo hapa nchini. Kumbukumbu zinaonesha maafa ya mwanzo hapa afrika ni yale yaliyoandikwa katika vitabu vitukufu ambapo dunia ilipelekewa moto na gharika wakati wa enzi za nabii Nuhu. Gharika hilo lilisababisha mafuriko na maji kujaa katika uso wa afrika ambapo nabii nuhu aliweza kunusurika pamoja na kizazi chale kwa kujiandaa kutengeneza meli au merikebi.
 
Back
Top Bottom