Niko tayari kupokea kadi ya CCM endapo ntajibiwa

Jilanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
255
40
Natanguliza heshima mbele!

Nipo tayari kupokea Kadi ya CCM na kuwa mwanaharakati endapo tu ntapatiwa majibu ya kuridhisha juu ya Swali lifuatalo.

Utangulizi.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vigezo vingi sana vya kisheria pale mtu anapotaka kuanzisha kampuni.

Yaani hatua 13 za kisheri (Legal Procedures) na zifanyike kwa muda usiopungua siku 28 ndipo kampuni litakuwa limekidhi vigezo na uhalali wa kuanzishwa!

Swali:
Je kama kweli Serikali kupitia kitengo cha Brela wako makini, waliwezaje kusajili kampuni hewa ya Richmond ambayo ilidumu kwa miaka zaidi ya mitatu huku serikali wakiwalipa 153M kwa siku?
 
Ondoa majungu yako hatukutaki kwenye chama chetu nenda kaandamane huko na wehu wenzako.
 
Kaka kuwa mpole tu huwezi pata kadi yao maana hakuna anayetaka kusoma au kurudia kusoma swali alielewe akujibu ni moto mkali tena wa gas .
 
Msubirie Nape atakuja na majibu mepesi kwa swali gumu kama hili. Nakwambia wapo tayari wakukose kwenye chama chao kuliko kukupa majibu ya ukweli kwa swali lako! Magamba bwana, we acha tu....
 
Kwani we ni nina mbona kuna wa TZ wengi ambao sio wanachama wa chama chochote na tunaishi.
 
We huna shida na kadi ya CCM vinginevyo usingeuliza swali gumu namna hiyo!
 
Swali:
Je kama kweli Serikali kupitia kitengo cha Brela wako makini, waliwezaje kusajili kampuni hewa ya Richmond ambayo ilidumu kwa miaka zaidi ya mitatu huku serikali wakiwalipa 153M kwa siku?

Tena kampuni hiyo ilisajiliwa siku ya tarehe 1/05 i.e MEI MOSI ambayo ni siku ya mapumziko (public holiday)
 
Natanguliza heshima mbele!

Nipo tayari kupokea Kadi ya CCM na kuwa mwanaharakati endapo tu ntapatiwa majibu ya kuridhisha juu ya Swali lifuatalo.

Utangulizi.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vigezo vingi sana vya kisheria pale mtu anapotaka kuanzisha kampuni.

Yaani hatua 13 za kisheri (Legal Procedures) na zifanyike kwa muda usiopungua siku 28 ndipo kampuni litakuwa limekidhi vigezo na uhalali wa kuanzishwa!

Swali:
Je kama kweli Serikali kupitia kitengo cha Brela wako makini, waliwezaje kusajili kampuni hewa ya Richmond ambayo ilidumu kwa miaka zaidi ya mitatu huku serikali wakiwalipa 153M kwa siku?

Pia viongozi wetu wakipunguza vigezo ili tu richmond ikidhi vigezo ambavyo haikuwanavyo kwaali ya kuchukua tenda
 
Ondoa majungu yako hatukutaki kwenye chama chetu nenda kaandamane huko na wehu wenzako.

kwani ni chama gani kina majungu na wavivu wa kufikiria? Wameishia kuwa wambea tu kama wanawake golikipa wanaokaa kuanzia asubuhi mpaka jioni wakipiga umbea pasipokujua wala kutimiza wajibu wao. Huku wakitoa kipaombele cha kuwangia upinzani ndo wachezi pasipokufikiria na kujua kiini na chanzo cha tatizo ili wapate kutatua angalia sasa hata kwenda ntwara wanaogopa na kuishia kuropoka kwenye media tu
 
Back
Top Bottom