Niko Safarini Samunge Loliondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niko Safarini Samunge Loliondo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIBURUDISHO, Jul 26, 2011.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  WanaJF wenzangu habari za jioni,natumai mu wazima woote.Mwenzenu kwa kipindi kirefu nimekuwa nikisimuliwa na kusikia kwenye vyombo vya habari juu ya tiba inayotolewa na mch,mstaafu Mwaisapile.Hatimaye leo hii nimeamua kwenda mwenyewe kujionea inakopatikana tiba hiyo.Ni safari iliyotugharimu muda wa masaa 14 toka Mwanza mjini hadi ilipotimu saa moja kamili ndio tulikuwa tunawasili kijijini Samunge.Hali tuliyoikuta ni foleni ya magari saba mbele yetu na huduma ilikuwa imesitishwa hadi kesho asubuhi.Kwa wenyeji wetu Wasonjo wakiwa wanajishughulisha na biashara za chakula na malazi.Kwa wingi wa utitili wa vibanda nilivyoviona kabla haujafahamishwa hapa ndipo anapopatikana mch,Mwaisapile unawezasema uko kwenye machimbo ya dhahabu.Hadi hivi sasa ninavyopost hii thread niko ndani ya kibanda cha Msonjo mmoja mchoma nyama ya mbuzi nikisubilia ya kwangu iive!!!!!!! Jamani kama kuna mtu alisahau kitu chake chochote Samunge aniagize nami nitamletea AKSANTENI SANA.
   
 2. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole,cc 2meshtuka dawa haiponyi ni usanii kama wa karata tatu
   
 3. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Salimia wasonjo, walanguzi wale bado hawajamaliza mifugo yao!?? mkuu! angalia pia huko njiani haswa karibu na Oldonyo kuna wamasai wanarushia magari mawe wale haswa wakati wa kiza
   
 4. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, ungerudi tu unajisumbua bure kama umefuata dawa hamna kitu, kama umekwenda kutembea sawa wasalimie wasonjo
   
 5. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Powa bos, tayari nimekwishaonyeshwa guest bubu iliyojengwa na makaratasi ya nailon na kitanda cha miti tayari mwanaume nimekwishajilalia nimelipa sh elfu tano Nawashukuru airtel wanaonisababisha naungana nanyi kama nipo town taratibu channeli ya Aljazeezra inanifariji kupitia kwenye simu yangu.Usiku mwema nitakaloliona huku sitasitakuwajulisheni.
   
 6. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wako wapi waliojisifia tiba ya babu? Watz tulipewa matumaini ya mwisho wa matatizo yetu. Lakini sasa wale walioacha tiba zao kwa imani ya tiba ya babu, mpaka sasa bado wanaendelea na dawa zao za kawaida. Kama kweli dawa inatibu mbona waliotumia dawa, wengi wanaendelea na dawa zao? Ghalama zote za Loliondo zimekwenda bure.!!
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Du kweli huko ni soo,gest nyumba ni ya makaratasi ya nairon kwa hiyo wa nje anamuona wa ndani na wandani anamuona wa nje?
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Aisee wasonjo na ile dizaini yao ya kuchoma nyama ni kiboko, ila niliacha kula pale msonjo alipopenga KAMASI km mita tano toka kwenye nyama halafu akajifuta kwa mikono daaaaaaaaaaah wasonjooooooooooooooooooo
   
 9. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  haha haaaaaaa mbavu iseee, lol umenitia kinyaa afu ukanichekesha vilevile, aaah loliondooooooo! :)
   
 10. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  loliondo ni fake pastor.hahah walioenda kukamua vikombe huko
  halafu wakadhani wamepona kumbeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!
  sasaaa inakuja hatari pande ya pili wengine waliacha dozi madhara yanakuwa makubwa zaidi

  off point:wakati nasoma kibosho girls miaka hiyooo palitokea
  kijana mmoja anaitwa gerald
  akadai katokewa na bikira maria, watu maelfu na mamia
  walikuwa wanamiminika pande hizo kupata maji ya baraka.
  sijui aliishiaga wapi kijana yule manake na yeye alipotelea kama babu wa loliondo
  .of course namwonaga town lakini ile huduma kwishnehi
  my point here watu tusikurupukie mambo.unaskia jambo
  bila kutafakari unakimbilia.na inawezekana hiyo ya loliondo inauwa taratiiibu
  yaani madhara yanaweza kuibuka huko mbeleni
  ndo hapo kutakuwa na kilio cha mbwa midomo juu
   
 11. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Mbona hujatuambia unaenda kutibiwa ugonjwa gani????????????
   
 12. AlP0L0

  AlP0L0 JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 3,473
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Poleni sana mliokunywa kikombe cha mauti huko loliondo, shetani amemdanganya Babu
   
 13. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kwakweli pole yao. sasa mchungaji mstaafu yupo anaendeleza tiba au?
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Watu wanazidi kupukutika tu
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  because of infidelity

  so do you
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Acheni saundi jamani!
  Babu yupo, sasa hivi anatibu zaidi watu wa nje na Ng'ambo!
  Habari zake zinazidi kuvuma kila pahala duniani!
  Mimi naamini kabisa kuwa dawa yake inatibu, maana nina ndugu kibao waliotibiwa, na sasa wanaendelea kuishi maisha ya kawaida kabisa bila matatizo ya awali!
  Sijasikia aliyekufa kati ya jamaa karibia 200 ninaowajua ambao walimeza kikombe!

  Tuache propaganda za hisia na kufurahisha wasomaji!
   
 17. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  PJ jana nimekaa sehemu Mdada mmoja akawa ananisimuliwa shosti yake kapona NGOMA.

  Do you know any one aliyepona Ngoma?
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Siyo kumjua tu, ni kwamba niko nae sehemu moja ya kibarua!
  Na bahati nzuri ni MTU muwazi toka enzi hizo akiwa na ngoma hadi sasa yuko Neg- na anaendelea kuonyesha hadharani dokomenti zake!
  Dawa ya babu inafanya kazi!
  Shida ya hapa JF hata ukiona tukio LIVE na kuja kuripoti hapa watu watakwambia LETE SOURCE!
  Ndiyo maana jamaa mmoja kawauliza wanaotaka SOURCE kuwa wanataka TOMATO, au CHILLY SOURCE!
   
 19. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Dawa ya Mzee Mwasapile inawaponya wenye imani zao na waliofuta masharti.
   
 20. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kwamba kuna waliopona na ambao hawajapona. Nawafahamu wengi tu! Mimi nadhani wale ambao hawajapona wakarudie dozi. Mchungaji alitaka watu wapige kikombe kimoja bila kurudia ili kupunguza msongamano.
   
Loading...