Niko safarini kwenda Iringa

Magu

Senior Member
Jun 13, 2011
156
56
Wadau niko safarini kwenda Iringa nimeanza safari saa sita na nusu mchana.

Nimepanda basi lenye majina mawili kwa gari moja, ubavuni limeandikwa Budget na mbele linaitwa Upendo.

Gari limechakaa ile mbaya bodi yake, hapa kwenye dashi bodi usiombe ni kama uko ktk gari lililotupwa dampo, linatoa mlio kama magari ya zamani SISU au Leyland Dafu kwenye injini.

Tuombeeni tufike salama
 
hayo magari nayafaham sana bora ungepanda abood. Lakini Mungu akujalie ufike salama.
 
hayo magari nayafaham sana bora ungepanda abood. Lakini Mungu akujalie ufike salama.

Abood za Iringa na Mbeya ni mabovu kweli kweli, mabasi machovu huondolewa kwenye rute ya Dar - Moro na kupelekwa mikoani.
 
Je umefika salama. baridi Je.

Wakuu nawashukuru kwa sala zenu nilifika salama saa nne usiku tukiwa tumeanza safari saa sita na nusu mchana, hivyo ni takribani masaa 10 ya safari ngumu, lakini ni 450 KM tu toka Dar, baridi la ukweli.

Nauri ni 15 000 kwa kweli haina mlingano, mana kwa ubovu huo wa basi tulipaswa labda abiria ndo tulipwe usumbufu.
 
Back
Top Bottom