Poapoa mkuu kila la kheri na Mungu akutangulie ktk harakat zako zisizoenda kinyume na matakwa yakeMuhimu sana Mkuu,nimesogea nyuma zaidi Iringa town hapa.
Naomba nifafanue na kama kuna sehemu utahitaji ufafanuzi zaidi usisite kuniuliza.Nina swali mkuu. Biashara ya kukusanya vigogo na kuuza kwa wachina inahitaji minimum mtaji wa sh.ngapi? Wewe ulianza na mtaji wa sh.ngapi? Ulipata hasara au ni kwamba mtaji ulirudi bila faida yoyote?
@Baraka21Naomba nifafanue na kama kuna sehemu utahitaji ufafanuzi zaidi usisite kuniuliza.
Hii biashara mtaji wake hutegemeana na mambo yafuatayo;
1: Upatikanaji wa miti.
Hapa itategemea miti umeipataje,je alie kuuzia ni mtu anaekujua au kakuuzia bei za kigeni.
2: Umbali ulikopita hiyo miti mpaka kufika kiwandani.
Miti ikiwa mbali sana gharama za usafurishaji huongezeka.
3: Kiasi cha miti.
Miti ikiwa mingi gharama za yule mkataji,hapa namaanisha mtu wa Chainsaw zitaongezeka na usafirishaji pia.
Ila bei ya kawaida ni 50,0000= kwa wastani wa kujaza safu mbili zilizo jaa haswaa!!
4: Barabara & msimu wa mvua.
Msimu wa mvua barabara nyingi za porini huwa haziingiliki kwa urahisi,so jiandae kupakia mzigo nusu nusu wao wanaita "Kushant". Hapo gharama lazima iongezeke.
Pia msimu kama huu wa kiangazi barabara nyingibza porini zinapitika kwa urahisi,hali inayopelekea viwandani kwa wachina kuwa na influx ya mzigo kutoka pori. So hii ina affect soko,kuna time imefikia mchina hapimi mzingo tena,anakukadilia tu pesa kulingana na mzigo.
Kuhusu mtaji ambao nilianza nao mimi.
Mimi sikwenda na pesa hata na mia ya mtaji kwasababu nilikua napita tu pale nimetoka zangu Mbeya,Chunya huko kusaka pesa ila sijaambulia kitu.
So kuna namna nikiweza kudeal na wenyeji wangu mapema tu nikawa nmepata almost 850K,na ikatosha katika gharama zote kwa ujumla .
Hivyo naweza kusema mimi mtaji wangu ulikua ni 850,000/=
Na nilipata 547,000/= tu,HASARA.
Kwa hiyo Mafinga umeondoka na 850,000+547,000 au 850,000-547,000?Shukrani kwako pia,tuko pamoja.
Acha roho mbaya we papaiNyie ndo wezi wenyewe mtu usiyemjua kumkaribisha nyumbani ni hzi sio enzi za kina Yesu huko sijui Ibrahim
Dah, mpambanaji pole sana. Mungu atatuvusha tu wote tunapitia hiyo hali.Ni 850-547= 303,000/= HASARA.
Na hii ni ile awamu ya kwanza kabisa nilipoanza,kwa sasa hali imekua mbaya zaidi.
Kwa nn mkuuWakuu kama mna mpango wa kufanya biashara ya Vigogo Mafinga (vile tunapaleka kiwandani kwa wachina) nawashauri mwende kwa taadhari kubwa, mara ya pili hii napigwa KO.
Asante sana ndugu,naamini hatutobaki hivi siku zote ni LAZIMA hali itabadilika na unafuu utapatikana.Dah, mpambanaji pole sana. Mungu atatuvusha tu wote tunapitia hiyo hali.