Niko njia panda, ushauri tafadhali

Ifike wakati muwe mbaacha ujinga basi mnatudhalilisha sana WANAUME,hapo mpaka umeambiwe umekalia kaa la moto ndipo uinuke???
 
Ipo hivi nilioa single mother mwaka jana mwezi October,anaishi Mwanza na mimi nipo mkoa jirani,mwezi January akaomba aende Mwanza kuona maendeleo ya biashara zake(ana duka la nguo)
Muda wote alishanihakikishia kwamba hana mawasiliano na baba wa mtoto wake,na mtoto anaishi na bibi yake hivyo mawasiliano na pesa ya matumizi yapo kwa bibi yake,
Aliporudi kutoka Mwanza(alikaa wiki moja)nikakagua simu yake na kukuta kama siku tatu mfululizo walikuwa wakiongea na mzazi mwenzake.
Kuongea na mzazi mwenzake kwangu siyo tatizo maana siwezi kujua waliishije mpaka kuzaa pamoja.Ila kilinichonistua ameenda huko ndipo wakawasiliana karibia kila siku, na nilipomuuliza mbona ulisema hamuwasiliana ina maana ulinidanganya? Akasema "alipiga kujua hali ya mtoto wake"
Mimi mtu mzima nikaona huyu hatutafika mbali,bora nimpunguze kabla sijaingia gharama na kupoteza muda.
Nilimuacha kistaarabu sana mpaka leo hajui kama tumeshaachana au laa,kwa sasa siwezi kuoa mwanamke aliyewahi kuolewa au kuzaa na mtu mwingine bora nitafute tu gurunyembe ambalo halijawahi kuolewa wala kuzaa lije liniharibikie mwenyewe.
 
Huuu msemo wa waha huwa una ukweli ndani yake mwanamke aliyeshindwa na mwanaume mwenzio wewe utamuweza.
 
Tulisha waambia, ukitaka kuoa single mother hakikisha baba mtoto wake amekufa na akuonyeshe kaburi lake.
 
Shukran mkuu kwa ushauri
 
Kilichopendwa hapo ni uwezo wako wa kugharamia tu,hakuna mapenzi ya kweli hapo
 
achana nae utalizwa bure chezea wapenda pesa mujini.
 
Wewe ni mpumbavu, endelea kukaa na upumbavu wako
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…