Niko njia panda,naombeni ushauri

jombaa nimeshangaa sana kumpa title la wife material huyo mdada,wife material anakupangia jambo nawe unafuata.Nina mashaka na hiyo ndoa ambayo unaifikiria baina yenu,lazima uanaume wako utakuwa na mapungufu yaani unaburuzwa kiivyo.Hata hivyo kwa ushauri wng,fanya maisha yako na usiruhusu hisia(mapenzi/kupenda) zikatawala uhalisia(umepangwa kwa muda/goma lako kwa sasa linatumika na mwingine huo)
 
Wapendwa Wana JF,

Nimekuwa katika uhusiano na dada mmoja mzuri sana, na kulingana na nilivyo mtathimini anaonekana ni wife material, I admit to say that from my heart. Tatizo lililopo ni kuwa tunaishi mikoa mbali mbali. Mimi naishi mkoani kagera, na yeye anaishi mkoa wa Katavi.

Toka tufahamiane tumekuwa na mawasiliano active muda wote, though mikwaruzo ya mara chache chache sana hutokea na immediately we resolve it and become one thing again.

USHAURI:
Kwa kuwa tumeadhimia kuweka mambo yetu hadharani kwa wanafamilia mwishoni mwaka huu (december, 2016), huyu mpenzi wangu ameniomba na kushauri kuwa ni vema tusiwe na mawasiliano kwa muda wa miezi mitano toka sasa hadi mwezi september, 2016 ili ibaki miezi mitatu...then ndio tuanze mawasiliano motomoto kuelekea december kukamiliasha mambo muhimu ya kutuunganisha rasmi.

Kasisitiza kuwa ili kufanikisha hilo kila mmoja am-block mwenzake kwenye simu na kusiwe na mawasiliano hadi tarehe 1 semptember, 2016. Mimi nilishangazwa na kauli ile, kwa haraka ili kupima upepo nione itakuaje. Nilipomkubalia tu, basi akani-block kweli hadi muda huu naandika huu uzi.

1. Wadada kweli mnaweza fanya hivyo kwa mtu unayempenda kwa dhati - kutowasiliana nae for 5 months?
2. Inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia huko katavi na mimi nisijue kinachoendelea?

Nipo njia panda...nishaurini....nielekeee upande wa kulia kumfuata atakavyo yeye au mimi niamue kufuata njia nyingine upande wa kushoto?

NB: Naombeni ushauri sahihi hasa kwa watalaam wa mambo ya mahusiano yenye muelekeo wa ndoa.

KARIBUNI.

Pole sana kiongozi upo njia panda ya wapi maana hata mimi umeniacha njia panda aiseee.....maana ndio naiskia leo kitu kama hiki.
 
Dah...mimi sina cha kuchangia ila kumbuka usemi huu:
"ukiona manyoya...!!!"
Kama wewe ni mwanaume kamili jibu unalo.
...tupiamo kapicha kake basi...!
 
sikuwa hewani muda mrefu nimekaribishwa na hiki kituko cha huyo mdada hadi nimecheka sana.wadada msitufanyie hivyo maana nyie mkifanyiwa mnalia sana mpaka dunia inajua mnaonewa.
 
jombaa nimeshangaa sana kumpa title la wife material huyo mdada,wife material anakupangia jambo nawe unafuata.Nina mashaka na hiyo ndoa ambayo unaifikiria baina yenu,lazima uanaume wako utakuwa na mapungufu yaani unaburuzwa kiivyo.Hata hivyo kwa ushauri wng,fanya maisha yako na usiruhusu hisia(mapenzi/kupenda) zikatawala uhalisia(umepangwa kwa muda/goma lako kwa sasa linatumika na mwingine huo)
Samahani, umeoa? Kama hujaoa subiri uone au waombe waloooa wakusimlie tunavyoburuzwa
 
Nimeoa naishi kwenye ndoa mwaka 4 sasa,suala la kuburuzwa kwng sijaliona kwng kwa kuwa najua mbinu ninazoishi na mwenza wng!
 
Mdau usipoteze muda aise kama wanawake wapo wengi sana hapo ninavyoona ameamua kukupotezea aise kimbia fasta
 
mahusiano bila mawasiliano yamekufa.....someone else is keeping her busy...nimekumbuka mistari ya wimbo flani...who is loving ma baibe and taking care of her I need to know right now.....pole mkuu ila kiukweli ushaliwa.....
 
Hii
Wapendwa Wana JF,

Nimekuwa katika uhusiano na dada mmoja mzuri sana, na kulingana na nilivyo mtathimini anaonekana ni wife material, I admit to say that from my heart. Tatizo lililopo ni kuwa tunaishi mikoa mbali mbali. Mimi naishi mkoani kagera, na yeye anaishi mkoa wa Katavi.

Toka tufahamiane tumekuwa na mawasiliano active muda wote, though mikwaruzo ya mara chache chache sana hutokea na immediately we resolve it and become one thing again.

USHAURI:
Kwa kuwa tumeadhimia kuweka mambo yetu hadharani kwa wanafamilia mwishoni mwaka huu (december, 2016), huyu mpenzi wangu ameniomba na kushauri kuwa ni vema tusiwe na mawasiliano kwa muda wa miezi mitano toka sasa hadi mwezi september, 2016 ili ibaki miezi mitatu...then ndio tuanze mawasiliano motomoto kuelekea december kukamiliasha mambo muhimu ya kutuunganisha rasmi.

Kasisitiza kuwa ili kufanikisha hilo kila mmoja am-block mwenzake kwenye simu na kusiwe na mawasiliano hadi tarehe 1 semptember, 2016. Mimi nilishangazwa na kauli ile, kwa haraka ili kupima upepo nione itakuaje. Nilipomkubalia tu, basi akani-block kweli hadi muda huu naandika huu uzi.

1. Wadada kweli mnaweza fanya hivyo kwa mtu unayempenda kwa dhati - kutowasiliana nae for 5 months?
2. Inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia huko katavi na mimi nisijue kinachoendelea?

Nipo njia panda...nishaurini....nielekeee upande wa kulia kumfuata atakavyo yeye au mimi niamue kufuata njia nyingine upande wa kushoto?

NB: Naombeni ushauri sahihi hasa kwa watalaam wa mambo ya mahusiano yenye muelekeo wa ndoa.

KARIBUNI.
inanikumbusha zamani nilibahatika kukamata njiwa mzuri sana kwa mtego, wakati nikiwa kwenye harakati za kumpapasa manyoya yake laini na mazuri ghafla akachomoka na kuruka nikabakiwa na manyoya ya mkiani mkononi. Pole sana.
 
Hii mpya. Pole sana. Bt kwa mwenye akili timamu ajiongeze..
Mnacheza bongo muvi ama?
 
Back
Top Bottom