Niko njia panda msaada

Yani we ni mjinga ndo maana hata mwanamke kaweza kukuletea mchepuko nyumbani kwako kashakuona ni Fala huna maamuzi yoyote mbele yake.

Kwa tukio hilo ulitakiwa uwe tayari umeshachukua maamuzi ya kuachana nae kuomba ushauri ni kama vile unatafuta suluhisho ili uendelee kuishi nae acha ufala we jamaa, na hiyo safari unayomsindikiza kwao akajifungue bado tu unaiongelea na wakati mimba siyo yako?

Acha undezi acha udhaifu wa kiduanzi unampa mwanamke umuhimu kuliko hata nafsi yako? Kiazi kweli
 
Pole mkuu... usikute mkeo anatokea kanda ya kati.
 
Pole sana kiongozi, hakika Una busara na hekima ya Hali ya juu. Tafuta ushahidi wa kutosha. Mpeleke akajifungue, baada ya wiki nenda kwao na ushahidi wote Kisha mchakato wa talaka uanze. Huyu huwezi kuishi nae kama mke tena kwenye ulimwengu huu.
 
kama unampenda mchane ukweli na uwe tayari kusamehe,, kama ulishashtuka kitambo kuwa ulishikiwa akili kumuoa piga chini,, ni bora kuanza moja
 
Katoe nakala ya hiyo kadi ya kiliniki,mpeleke kwao,usimpe matumizi wala usimfuate.
Ataliamsha yeye na baadae wewe piga kimya.
 
Umemshauri vizuri Sana hakika
 
Mbaya sana hii.
Huyo si mke tena,ona njia sahihi ya kumumtaliki.
Tunza ushahidi!
 
Hivi kweli,ikiwa ni wewe. Namba 4 hapo. Unaweza? Hiyo ni zaidi ya dhalau. Bora achepuke tu utasamehe,japo kauli kupenda,haipo. Huko ni kujitia uzuzu bure tu. Mpaka anamzalia mtu,ni ile unaambiwa,nipo kwake kimwili tu. Sasa,huyo wa nini?

Hii simpo. Mpaka anajifungua,bado siku chache sana. Hizo zivumilie. Kikubwa tunza hiyo namba.
Kwao,ikifika siku,mpeleke tu. Nauli toa,lakini usimuache na chochote. Na hapo hapo,kama wazazi wapo,ongea nao,na ushahidi uliopo wape. Akizaa poa. Akijifungua,sawa. Kadi ya kliniki haipo mbali,ukitaka ipige kopi,uende nayo ukweni. Mwambie atoe origino. Akigoma,toa kopi.
Mahakama ina uwezo wa kuziomba kampuni za mitandao kutoa mawasiliano ya mtu na mtu. Wambie hilo wasiwe na wasiwasi,utaghalamia. Ye mwenyewe ataamua.

Akikataa,thibitisha. Akikubali,achana nae. Ukute ulikuwa unaogea taulo alilojifutia mwenzio.
 
Daa!! Kuna wanaume aise mna roho hili nalo ni jambo la kuja kuuliza huku aise,,, chukua maamuz ww,, na hiyo ndo tkert yake huko hom kwao,, kwanza piga pcha hiyo card ya mtt Ili uwe na ushahid,, peleka kwao siku akitaka kulud mwambie aende Kwa mme wake wa watt hao,, wambie na wazaz wake hapo hapo
 
MTU Kama analeta fiction story ili apate attention ya watu anakuwa anakosea.

MTU unatumia akili yako na muda ili kutoa ushauri kumbe MTU hayupo serious anadai hii story ya kutunga.

Hii ndo sababu MTU anaamua kukaa kimya hata kwa mwenye uhitaji wa kweli.

Guys we need to be serious na tuitumie hii platform in building each other .
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…