Niko kwenye Jeshi la akiba la wanajeshi wa Tanzania, Utaninyimaje haki ya uraia EX-POLICE wako?

Mkuu lukosi nakuelewa, lakin uliwahi kujiuliza kwanini maisha ya watanzania/wafanyakazi wengi hadi sasa ni duni?
 
Bwana Lukosi!

Mimi sitakutukana kwenye comment hii kwani kama ni matusi umeyapata mengi kwenye uzi huu na umeyavumilia sana Naomba nijibu haya maswali kwa ufasaha ili na mimi nisiwe mmojawapo wa kukutukana tena ila ukipuuzia basi tegemea nondo za kutosha kwenye kila uzi utakao tuma.

SWALI 1. Jana nilikutumia link jana JK Alikuwa uk anaongea na Diaspora wenzako kwanini huku mwambia huko huko unakuja kusemea kwenye keyboard?

SWALI 2. Nakubaliana na wewe kuwa ulikuwa mvivu na hukuwa mzalendo wa nchi yako ndio maana ukaamua kwenda kutafuta maisha mbele Je umefanikiwa kiasi gani au umeshindwa kufanikiwa kiasi ukilinganisha na maisha uliyo ya kimbia ya bongo?? 2B. Kama umefanikiwa unataka kurudi ili iweje? nakama hujafanikiwa kwanini usiwe wazi tuu kuwa yamekushinda na umeamua kurudi nyumbani? Maisha ya polisi kwa sasa ni mazuri sana WP wa kawaida anamiliki gari zaidi ya moja yakutembelea, biashara na na maisha yao mazuri tuu rushwa ya kumwaga kwanini hukuvumilia kama wao mkuu wangu haya ya rambirambi yangetoka wapi leo?

SWALI 3. JK kupitia chama chako ccm aliwaambia nyie madiaspora kuwa mliikimbia nchi ikiwa na njaa kali leo mmeona pamebadilika mnangangania kurudi bakini huko huko je wewe kwanini kama unaipenda Tanganyika kwanini usiukane uraia wa UK Na kama unaupenda wa UK Kwanini usiukane wa Tanganyika kwanini unangangania uraia pacha???

Nasubiria majibu mkuu ila usije na majibu mepesi ya kiccm pls.

Mimi naongea ukweli

Zamani polisi walikuwa duni sana

Nakumbuka mkuu wa kituo alinichukia sana kwa sababu nilikuwa polisi wa kwanza kununua baiskeli mpya PHOENIX .
Baisskeli yenye we nilikopa kwa MZee Ally Kessy
 
Msingechukua uraia wa nje na kubaki na wenu tu ila mgeomba resident permit na mgeishi vizuri tu kwani hata Mohammed Al Fayed anaishi kwa permit na passport yake ni Egyptian mpaka leo na anamiliki biashara nyingi tu ingawa aliomba kwa kuhonga akavuruga kila kitu, huo ni mtazamo wangu tu.
 
Mimi naongea ukweli

Zamani polisi walikuwa duni sana

Nakumbuka mkuu wa kituo alinichukia sana kwa sababu nilikuwa polisi wa kwanza kununua baiskeli mpya PHOENIX .
Baisskeli yenye we nilikopa kwa MZee Ally Kessy

Lukosi, naweza kuwa mtu wa kwanza kukupa ushauri ama kuna waliotangulia kukupa ushauri. Ni vizuri kuongea lakini hekima inatakiwa hasa katika kuchagua maneno ya kuongea.

Kauli zako zinaweza kukuponza kama si leo basi hata huko mbeleni na ukichukulia kwamba mitandao hii inasomwa sehemu mbalimbali duniani.

Hatufahamiani lakini naona nitoe ushauri huu kwako, kesho na keshokutwa utanikumbuka.
 
Mbona unakuwa mwoga kiasi hicho?

Kwa hiyo ulitaka niseme askari walikuwa na maisha bora enzi hizo?

Unajua kuwa nimelala sana kwenye vile vinyum,ba vya bati? mshahara ulikuwa hata hautoshi kununua watoto nguo ya sikukuu wewe ulitaka nisemeje.

Leo polisi walau wanalipwa vizuri lakini sio zamani

Kama una ndugu yeyote polisi wa zamani muulize akuambie...
 
Haujui ulisemalo,

Hata wanamgambo tu wanapewa mafunzo ya kivita, sembuse polisi?

Ulitaka nibaki polisi niwe fukara?

Nilikuwa nalipwa shs 7,250 wakati matumizi yangu yalikuwa shs 35,000, sasa hapo sijui mkate na siagi ungepatikana vipi?

Mazingira ya mishahara kwa wafanyakazi wa serikali yamebaki vilevile. Mbona hujiulizi wanaishije sasa? Waulize basi ccm kipenzi chako wanaendeshaje serikali inayolipa wafanyakazi wake kibaguzi...wachache, hasa wanasiasa mfano wabunge wanalipwa pesa nyingi huku walimu wakilia na mishahara isiyokidhi mahitahitaji yao ya mwezi. Ukipata jibu, tafadhari nishirikishe.

For your info, ccm imeteka kila kitu na kwa kiburi walichonacho wanataka hata kile kinachoonekana ni haki ya walio wengi iombwe kwa kupiga magoti. Msemo lahisi kwao ni huu hapa...'jeshi ni letu, tume ya uchaguzi ni yetu, polisi ni yetu...' Sasa hata bunge la katiba mpya ni lao.

Watanzania nje ya uccm wao (ambao nizaidi ya milion 40 wanapaswa wapige magoti kuwaomba haki zao ikiwemo hiyo ya kwako. Uzuri milioni hizo za watanzania ni wapole kama kondoo... wanasubili ni lini ssm iwape hiyo haki kwa amani. Hiyo haki atapata mjuu wako sio wewe chini ya utawala huu wa ccm.
 
Uzalendo ktk nch yako ni kitu cha mhimu sana,ss wew uliamua kuacha kisa mshahara na kumbuka ww ulikua mzalendo wa nch yako,ss uraia gani unao hitaji hapa wa tz au wa tanganyk
 
Mbona unakuwa mwoga kiasi hicho?

Kwa hiyo ulitaka niseme askari walikuwa na maisha bora enzi hizo?

Unajua kuwa nimelala sana kwenye vile vinyum,ba vya bati? mshahara ulikuwa hata hautoshi kununua watoto nguo ya sikukuu wewe ulitaka nisemeje.

Leo polisi walau wanalipwa vizuri lakini sio zamani

Kama una ndugu yeyote polisi wa zamani muulize akuambie...

Mimi ni mtumishi ama ni mfanyakazi serikalini hapa Tanzania. Sina woga bali nimekupa ushauri tu ndugu yangu baada ya kupitia makala zako nyingi na kukusoma vizuri kwenye Google na Youtube. Angalia unachoongea na kuandika mitandaoni. Unaweza ukawa vizuri kipesa lakini Public Relation ni muhimu sana kwa leo na kesho.
 
Chris, 2yrs ago, ulikuwa mstari wa mbele kumtukana Amiri Jeshi mkuu, je hako kakiapo chako kalikuwa wapi? Napenda sana Uraia pacha, lakini sio huu unaoshabikiwa na CCM
 
Chris Lukosi nadhani mlifundishwa uzalendo kama first priority subject. Hata hivyo sasa hivi uandikapo thread hii kuna mchakato wa katiba mpya ambayo itakuja na jibu la suala lako

Ahsante kwa kuendelea kuipenda nchi yako ya kuzaliwa, ndio uzalendo

Alifundishwa uzalendo lakini alishindwa kuishi kizalendo katika nchi yake na aliamua kwenda kuishi utumwani hivyo yeye ni mtumwa na si mzalendo tenda na hana haki ya kuendelea kujivunia nchi yake kama anajidai ndio maana unaona anasema anahofu hata ya kuwekeza katika iliyokuwa nchi yake.

Wasitafute kubadioishwa kwa katiba iki kuhalalaisha usaliti waliokwishakuufanya kwa katiba iliyokuwa inatuongoza naikiyokuwa inakataza uraia wa nchi mbili kwanza ningekuwa na mamlaka ningalisema ikiwa katiba mpya itaruhusu uraia wa nchi mbiki basi wale waliokuwa na uraia wa nchi nchi nyingine kabla ya katiba hiyo hawataruhusiwa kuomba uraia wa nchi waliyoikataa mpaka kwanza wastakiwe kwa kuvunja katiba ioiyokuwepo na waadhib7we.
 
Alifundishwa uzalendo lakini alishindwa kuishi kizalendo katika nchi yake na aliamua kwenda kuishi utumwani hivyo yeye ni mtumwa na si mzalendo tenda na hana haki ya kuendelea kujivunia nchi yake kama anajidai ndio maana unaona anasema anahofu hata ya kuwekeza katika iliyokuwa nchi yake. Wasitafute kubadioishwa kwa katiba iki kuhalalaisha usaliti waliokwishakuufanya kwa katiba iliyokuwa inatuongoza naikiyokuwa inakataza uraia wa nchi mbili kwanza ningekuwa na mamlaka ningalisema ikiwa katiba mpya itaruhusu uraia wa nchi mbiki basi wale waliokuwa na uraia wa nchi nchi nyingine kabla ya katiba hiyo hawataruhusiwa kuomba uraia wa nchi waliyoikataa mpaka kwanza wastakiwe kwa kuvunja katiba ioiyokuwepo na waadhib7we
Wewe lazima ufe masikini tuu...
 
Chris, 2yrs ago, ulikuwa mstari wa mbele kumtukana Amiri Jeshi mkuu, je hako kakiapo chako kalikuwa wapi? Napenda sana Uraia pacha, lakini sio huu unaoshabikiwa na CCM
Video zangu zote zipo mitandaoni na hotuba zangu ziko hapa JF

Hata siku moja sijawahi kutukana kiongozi yeyote kuanzia katibu kata mpaka Rais. N a hiyo ni moja ya sababu niliyohama chadema kwa sababu hamna siasa zaidi ya kutukana viongozi tu.
 
Mimi ni mtumishi ama ni mfanyakazi serikalini hapa Tanzania. Sina woga bali nimekupa ushauri tu ndugu yangu baada ya kupitia makala zako nyingi na kukusoma vizuri kwenye Google na Youtube. Angalia unachoongea na kuandika mitandaoni. Unaweza ukawa vizuri kipesa lakini Public Relation ni muhimu sana kwa leo na kesho.
Mkuu nimekusoma,

Najua uunachoongelea na nitafuata ushauri wako...
 
Haujui ulisemalo,

Hata wanamgambo tu wanapewa mafunzo ya kivita, sembuse polisi?

Ulitaka nibaki polisi niwe fukara?

Nilikuwa nalipwa shs 7,250 wakati matumizi yangu yalikuwa shs 35,000, sasa hapo sijui mkate na siagi ungepatikana vipi?

Kwa mshahara huo, heri yako Chris uliamua kuondoka, wenzako waliobaki ndio wanatukamua huku Uswahilini kwa kesi za kubambikia na kulazimisha rushwa.
 
Back
Top Bottom