Kazi haina assurance yoyote Mkuu datz y. Ushauri ni mimi nibaki kwenye hiyo kazi ambayo haina malipo zaidi ya chakula cha mchana/hakimu hadi ajisikie siku hiyo kukupa chcht so poa. Wazo jingine nikujikita kwenye kilimo kwa mzazi mwenzangu alipo, ila kipengele ni namna jinsia ke vile hawajui kukaa na mwanaume anamlisha, kitu ilinishinda mara ya mwisho hadi kugombana nikaondoka. Hapo ndo akili yangu inastuck kufanya maamuzi sababu naona yapo 50/50 hadi kufikia kuomba mawazo zaidi hapa.Ushauri juu ya kipi? Be precise
Kazi umepata japo tempo, tumia connection hiyo kupata sehemu ya kudumu.
Na hiki ndo kinaniwazisha, kulelewa na mshikaji si shida ila haisound good kabisa, kulelewa na mwanamke ni kujishusha mamaee๐๐Nenda Njombe kamsaidie mzazi mwenzako kulima mahindi. Mwanaume kamili huwezi kulelewa na mwanaume mwenzako. Bora ukajifanye zoba kwa mzazi mwenzako, ili maisha yaendelee.
Sawa mkuu nashukuru kwa mchango wakoNenda Njombe ukalime bwana mdogo, kwa mazingira uliyopo sasa sioni NURU mbeleni zaidi ya kujipa matumaini hewa. DAR ES SALAAM ni mji unaopumbaza sana watu na kuwapotezea muda haswa ukiwa hauna uhakika wa kipato endelevu...
Kila la kheri
Maamuzi ya busara na ya kiutu uzima ni haya tu ya kwenda Njombe. Sijui ni kwa nini vijana huwa mnawachukulia wanawake kama watu wabaya sana.Na hiki ndo kinaniwazisha, kulelewa na mshikaji si shida ila haisound good kabisa, kulelewa na mwanamke ni kujishusha mamaee๐๐
Maisha mtegoni.
Maamuzi ya busara sana yanatakiwa mkuu
She so Sweet kiasi kwamba mwenyewe sioni ugumu kwenda tatizo lipo kwenye malumbano, leo ananipigia akinieleza kuna pahali ananiombea kazi ili nisogee alipo (kuna watu watakuja kusema ataliwa na boss wako) nasubiri mrejesho wake.Maamuzi ya busara na ya kiutu uzima ni haya tu ya kwenda Njombe. Sijui ni kwa nini vijana huwa mnawachukulia wanawake kama watu wabaya sana.
Wanawake ukiwajulia, hata wawe pilipili kiasi gani! bado ni rahisi sana kuishi nao.
Huko huendi kukaa tu unaenda kufanya kazi.Na hiki ndo kinaniwazisha, kulelewa na mshikaji si shida ila haisound good kabisa, kulelewa na mwanamke ni kujishusha mamaee๐๐
Maisha mtegoni.
Maamuzi ya busara sana yanatakiwa mkuu
Endelea kukaa kwa jamaa, usitoke wala usisogeze mguu.Nipo kwa mshikaji wangu-haonyeshi kunichoka kulingana na hali yangu ananisaport sana kwa kila namna. Kuna muda hadi nasikia aibu hapa ndipo mawazo yanapoanza kwamba nikiondoka ataona nimedharau jitihada zake
Moyo na fikra naona 50/50 NAWAZA sipati majibu; kwamba nikibaki, je nitabaki kwa msela hadi lini(ye tayari maisha yake yana unafuu sana)pesa ya kodi, kula na other basic needs anaweza ku afford..Sikiliza moyo wako unavyokuambia.
Nmejibu kulingana na kile walicho changia mkuu, mimi kwangu naona 50/50 No More#Nimesoma reply zako zinaonesha unataka kurudi kwa mshangazi ukalelewe, yani wale wanaokupa ushauri unaoambatana na kurudi ndio unawaona wanakushauri vizuri bila shaka unasumbuliwa na genye na upwiru wa kummiss huyo unaemuita mzazi mwenzio
Komaa town mzee wanawake sio wa kutegemea kabisa komaa ujenge kwako komaa upate kitu cha kufanya town mishe nyingi jichanganye acha kufungwa na mawazo ya kuajiriwa na elimu ulionayo
Usirudi kwa huyo mshangazi utakuta maumivu hakuna mwanamke anaemtafutia ugali mwanaume halafu akawa mwaminifu hakunaaa
Tafadhali sana! Usimchukulie kama kahaba! Ukiwasikiliza hao utakesha, kikubwa ni kuziba masikio na kusonga mbele. Kwa Njombe, ukiamua kuacha u-mjini hutatamani kuajiriwa tena. Kule kilimo ndimo mwake, sema Sisi wengine tumezeeka sasa lakini huko ndiko kwa kupiga kazi. Mahindi, viazi mviringo, maharage n.kShe so Sweet kiasi kwamba mwenyewe sioni ugumu kwenda tatizo lipo kwenye malumbano, leo ananipigia akinieleza kuna pahali ananiombea kazi ili nisogee alipo (kuna watu watakuja kusema ataliwa na boss wako) nasubiri mrejesho wake.
In short yule ni mke wa kuoa ndugu na ikitokea nimefeli kufanya hivyo basi ni sababu zilizo nje ya uwezo wangu, we turn 8-9 years now, tulipoendana skuli tukaja kukutana kwa mara ya kwanza kimwili 2018โค๏ธโ๐ฉน
Ndivyo navyowaza au nilivyowaza ila nikawa NAWAZA kumdissapoint tena mshikaji ataniona jau kinoma.Mkuu asilimia kubwa ya hizi taasisi za serikali ukienda kujitolea bila barua rasmi ya mkataba, wataishia kukutumia tu kusafisha ma-file yao na kukimbizana na makaratasi yao ambayo wao wenyewe yamewachosha kuyafanyia kazi. Umeshasikia tetesi kabisa kwamba wanataka watu wenye Diploma, wewe huna, unategemea nini? You are literally wasting your youth energy on a dead end job kwa matumaini ya miujiza.
Serikali wakitaka kuajiri wanafuata taratibu na budget yao. Hiyo elfu tano unayoichukulia leo poa, itakufanya uwe stagnant kwa miezi mingine sita ijayo, halafu mwisho wa siku unaachwa hewani.
Huyo mshikaji wako hatokuonyesha tabia yoyote ya tofauti kwa sababu pengine ni mtu muungwana sana, lakini don't abuse his hospitality mzee. Kila mtu ana maisha yake na ana mambo yake ya siri anayotaka kufanya kwenye geto lake. Unazidi kujishusha thamani ukikaa hapo Dar bila ramani kuliko ukienda Njombe kupambana na mzazi mwenzako.
Mzazi mwenzako kavuna gunia 13 za mahindi kwenye heka moja tu! Huoni kuwa huo ni ushahidi tosha kwamba hiyo ardhi aliyopo ina baraka zake kiaina?. Huyo mwanamke ameshkutengenezea njia, wewe kama dume la familia nenda kamsaidie, kama msimu uliopita amepata gunia 13 peke yake, mkienda wawili mkaongeza nguvu na akili mkabarikiwa kuvuna gunia 50 au 100 si mtatoboa?
Huko Njombe ndiko kuna fursa yako ya haraka kwa sasa mzee, mchezo wa kilimo ukiujua vizuri unaleta hela ya haraka kuliko kuendelea kubaki bila ramani, matokeo yake unazidi kujilemaza tu.