Nikki Mbishi atarudi kumjibu P the MC?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,141
2,000
Kwa washabiki wa HipHop watakuwa wanaijua ile ngoma inaitwa Futi Sita aliyotoa P the Mc kumdiss Nikki Mbishi, baada ya Nikki kuanza chokochoko kwenye ngoma yake ya Welcome to Gambosh

Ngoma ya P the Mc imekonga nyoyo za wapenda HipHop na imefanya kuwa na kitu kama ‘teams’ hivi, yaani wanaomkubali Nikki Mbishi na wanaomkubali P the MC

Watu wengi wamezungumza kuhusu ngoma ile wengine wakimuambia Nikki asijibu ile ngoma ili isije ikatokea akakosea akajishushia huku wengine wakisubiri kwa hamu majibu ya Nikki Mbishi. Hivi karibuni Nikki alisema kuwa ile Ngoma haikumdiss bali imemuelezea tu kwa hiyo hana cha kujibu

Tukumbuke Nikki Mbishi ni mmoja kati ya wasanii wanaopenda kudiss watu haswa, ila wasipomjibu huamia kwingine, na kwa hivi karibuni wengi wakawa hawamjibu kabisa au wanamjibu kwa lugha ya kujificha sana, aidha aliyejibizana naye alikuwa Wakazi

Kwa kuwa mambo ya kudiss ni kawaida kwenye ulimwengu wa HipHop hivi kweli niki atajibu futi sita au atakubali kuzikwa. Unadhani akija kujibu anaweza kuifunika Futi sita?

Nikki Mbishi ni mmoja kati ya wasanii wanaodiss watu kwenye nyimbo zao. Kwa muda mrefu Nikki Mbishi hakupata mpinzani halisi wa kujibu ‘diss tracks’. Kwa wanaofuatilia Hiphop nchini watatambua alipoanza kumdiss Nikki wa Pili, ila hakujibiwa

Nikki Mbishi alimdiss Bonta kwenye wimbo wa Undisputed, aliwavamia Weusi kwa ujumla, alijibiwa na Lord Eyez kwa mstari mdogo baadae wote wakawa kimya. Mchezo wa kudiss ulienda kwa kina Nehi wa Mitego, Babu Tale hao wote hawakujibu ngoma hizo za Nikki Mbishi

Kati ya watu wa mwanzo kutoa ngoma kumjibu Nikki ni Wakazi ambaye kwenye wimbo wa Contorvesial alizungumza kidogo, na Nikki alijibu ile ngoma kwenye ‘where is my crown at’

Hivi karibuni Nikki Mbishi alitoa ngoma ya Welcome to Gamboshi ambayo alitoa mstari wa kukera kwa kijana wa Kiwalani, P the Mc,
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
16,071
2,000
Interview yake wakati anaitambulisha bengazi alishatoa rai mapema kwa kuweka vigezo vya mtu anayestahili kujibiwa.

So hiyo track ya mawenge ilikuja baada ya hiyo interview ya nikki kupita. Nacho kiona jamaa kafanya kile alichoahidi.
 

Niache Nteseke

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
467
500
Juzi usiku Ijumaa nafkiri ni So So fresh kama skosei niliskia ngoma 1 hivi ni kama Nikki ilikuwa ni ngoma flani ya kuimba hivi kama anamuimbia mchumba I think.

Sikuwahi kuiskia before ni mpya au ya zamani wadau...?
 

Alisina

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
3,741
2,000
P the Mc anauwezo wa kawaida..


Hafikii hata robo ya uwezo wa geezmabovu.
 

Ollachuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
14,708
2,000
Huyu Nikk mziki umemshinda..muda unazidi kwenda kazi kutoa track za kudiss mziki haujamlipa bado. Wanaomsapoti hawanunui kazi zake, wao ni kumsifia mitandaoni na ku download bure nyimbo zake.
 

kajamaa kadogo

JF-Expert Member
Nov 2, 2018
1,332
2,000
Huyu Nikk mziki umemshinda..muda unazidi kwenda kazi kutoa track za kudiss mziki haujamlipa bado. Wanaomsapoti hawanunui kazi zake, wao ni kumsifia mitandaoni na ku download bure nyimbo zake.
verse nikki mbishi

Watoto wengine ni mafala ile mbaya wana ndoto kama zile za watoto wa kala jeremaya

Unjuneering song
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom