Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Wanajamvi, nimeshtushwa sana,kusikia ni mgombe mmoja tuu amepitishwa na NEC kuwania kiti kilichokuwa cha Mh. Lisu.
Awali ya yote bila kujali yuko chama gani, ninampongeza.
Pili, nimesikitika na kujiuliza kulikoni, na je, ndivyo walipenda iwe kwa Wananchi wa jimbo hilo? Na je, ndivyo tulivyozoea ktk chaguzi zetu za vyama vingi? Na je, ni nani wa kulaumu au kunungunikiwa endapo wananchi wa jimbo hilo hawakutaka iwe hivyo?
Juzi, Mh .Rais wetu akiwa Bahi,aliendesha mchango wa kujenga shule. Kwa mliokuwepo au mlioona ktk luninga,aliita watu mbalimbali kupita mbele wachangie. Hata Bodyguard wake alichangia.
Pia, pa kusikitisha ni pa alipoita viongozo wa Vyama vya upinzani waende mbele kuchangia. Hakuna aliyejitokeza licha ya kuwepo ndani ya mkutano ule!!
Kwa tafsiri ya karibu ni kuwa Mh, Raisi wetu anatambua kisheria uwepo wa vyama vya upinzani!
Pia, anatambua uwepo wa viongozi wa upinzani ndani ya ujenzi wa Taifa hili.
Swali la kujiuliza, viongozi hao hupatikanaje? Jibu ni kwa njia ya chaguzi zenye fursa sawa na utashi na upendo wa walioko madarakani.
Ni kweli, viongozi hawa wanachaguliwa na wananchi kwa taratibu za kikatiba kwa kuhusisha vyama vyote. Uzalendo ni pamoja na kujumuisha Taifa kuwa kitu kimoja siyo katika kutoa michango tuu ya ujenzi wa maendeleo, bali hata zile haki sawa za msingi za kuchagua na kuchaguliwa. Sasa basi,
Ni nani anapaswa kuweka mazingira ya ushindani sawa katika haya?
Kwa maoni yangu, ningekuwa Rais, nisingekubali haya yatokee machoni pangu kwa vile, umma utakuwa unanitegemea kama Mzalendo no 1 na baba wa wanafamilia wote.