Nikiwa kama kijana ninasikitika na kuumia kwa kutokuwa na kipato cha kutosha kuendesha maisha. Nahisi kudharaulika na kila mtu

Kudharauliwa ni vita ndogo kwenye maisha ukikubali wanao kudharauliwa wakushinde hautaweza vita kubwa za maisha.
Dharau ndo zinaleta hasira ya mafanikio usipo dharauliwa huwez kuwa na hasira na maisha

Hama mtaa kafanyie Kaz sehem usipo julikna ukikaa mtaani kwenu kutoboa ni ngumu
 
Jipe moyo na uskate tamaa utakuja kufanikiwa.
Wanao kudharau leo, kesho watakusalimia kwa heshima.
 
Ulichokosea ni kurudi mkoa ulio zaliwa au ulipokulia ni vema ukahama mkoa uende mkoa mwingine tafuta pesa kidogo ufanye survey then kajipange uishi uko kwanza itakupa ujasiri wa kupambana na maisha maana hakuna anayekujuana atakama yupo ni mmojammoja sana ile hofu na aibu itakutoka machoni pako embu jitaidi kopa ata ndugu zako ukaanze maisha mbele ya safari omba kazi pale zikitokea usijipe stress sana Kwa elimu uliyokuwa nayo Ila angalia unataka nn maishani bidaboda kama ukitulia inaweza kukupa pesa ya kuishi na kukukutanisha na michongo Mingi sana.
Zingatio usiamie mkoa wa jirani nenda mbali na mkoa wako vuka ata mikoa mi3 mbele au nyuma
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa kusave Pesa za boom na kununua Boda.

Pili unatakiwa kutambua kuwa unasoma ili kuondoa ujinga. Husomi ili uajiriwe. Ajira huwa inakufata wewe ukishajua thamani ya elimu yako.

Mkuu kama umefanikiwa kununua bodaboda utashindwaje kutumia hiyo bado kukuingizia kipato

Kama umeshindwa kuthamini na kuzarau kazi ambayo ikilitumia vizuri unapata Pesa. Je kazi ya mtu utaipenda.

Thamini kwanza kile ulichonacho hayo makubwa yatakuja tu. Pia kama unaona hapo nyumbani kuna kikwazo hamia Mkoa mwingine.

La mwisho. Unapofanya shughuli nyumbani inakuwa ngumu kuchanganyikana na watu. Na kupata kazi inakuwa ngumu pia.
Ushauri wangu. Hama hapo nenda sehemu nyingine au Mkoa mwingine kapige kazi mkuu.
 
Nenda shule yoyote ya private hasa za Dar kama wewe ni kipanga kweli na una first class degree watakuchuwa. Ili mradi uwe unaweza kuwapa wanafunzi ujuzi ulio nao kichwani kwa sababu unaweza kuta wewe ni domo zege hata kuongea huwezi. Wanafunzi wakikuelewa unaweza kuwa unafundisha hata shule tatu kwa mwezi ukichukuwa hata laki 5 tuu kila shule ni 1.5m net na hicho ni kiwango cha chini kabisa. Kama huna pa kufikia Dar nitafute nikupe hifadhi ya mwezi 1. Baada ya hapo utakuwa unanilipa 150,000.kwa mwezi chumba chenye kitanda na godoro na meza ya kusomea na kiti. Umeme na maji utajilipia. Wewe umemaliza chuo ukarudi kijijini kwani ulipokuwa chuo ulishindwa nini kutafuta marafiki wanaokaa mjini ukaenda kujibanza kwao utafute chanel huko mjini. Shida nyingine mnazipanda wenyewe na kuziwekea mbolea zistawi halafu mnakuja hapa jukwaani kulalamika.
 
Law degree,graduated same year as you, mama wa kambo as you, unemployed, nmejitolea sana kwny firms nmeambulia chakula tu, Baba yangu mzazi sasa na sio mama wa kambo, Baba mzazi tu yeye ndio kaanza kunidharau na kuonyesha nje nje, sio mimi tu bali hadi hako ka degree kangu ka sheria, nmemaliza degree ya sheria miaka mi4 kwa mkopo so probably unaweza ona probability ya mimi kwenda law school kulipa 1.7 M kwa mkupuo mmoja sina tena, na Biashara yangu ya kiosk cha vinywaji nliofungua kwa kudunduiza Boom inaelekea kufa this month.. Bro tupambane, nafkri tunapitia magumu kwa sabab maalumu.. tutashinda
 
Never give up....
 
Bado una umri mdogo acha kukata tamaa kijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…