Moniel
JF-Expert Member
- Nov 17, 2020
- 228
- 553
Mimi ni graduate katika moja ya chuo maarufu hapa Tanzania mwaka huu, Nina miaka 24, nimesomea bachelor of Accounting and Finance
Kutokana na changamoto kadhaa ya ugumu wa ajira na maisha kiujumla nimeamua niwe dereva bodaboda, nilinunua used kutoka kwa hela niliyoipata kwa kusave nikiwa chuo (boom) niliamua kuisafirisha Hadi nyumbani Kanda ya Kati ili niweze kusukuma maisha, ninakaa kwa wazazi baba yangu mzazi na mama yangu wa kambo, kwani mama mzazi alishafariki.
Leo nimeonana na rafiki zangu tuliosoma pamoja, nmekua nikiogopa Hata kufanya kazi hii kwani wengi wanafahamu Mimi nilikua Nina uwezo mkubwa Sana darasani wengine wamekua wakinikejeli kwa mafumbo na misemo ya hovyo mfano "kweli kusoma sio kupata kazi" kila nikikutana na wazee barabarani wananiuliza "umepangiwa wapi," "siku hizi unakazi gani" yaani wanaamimini kwa vyovyote vile nitakua nimepata kazi tu, dah😞
Kazi hii ya bodaboda inaanza kuwa ngumu Sana kwangu, mfano Leo Kuna wadada wamenikuta kijiweni nimepaki , wanabaki kushangaa tu, "yule si Fulani" Yani unaamua kuzuga na kuondoka unaekt Kuna sehem unawahi.
Juzi Kuna abiria kaja ana dharau kweli, we "boda nimesema huku" Hata anavyonielekeza kwake anaelekeza kwa dharau, ukimuuliza wapi anakaa kimya mdada ana nyodo hatari
Kingine kinachoniumiza kichwa ni Hali ya hapa nyumbani, maisha yamekua ni magumu Sana, sometimes najitegemea kwa chakula kwa kula mgahawani, naogopa Hata kumwambia yule mama Kama Kuna msosi alipika, naweza kaa na njaa tu kisa kuogopa kuuliza, Mana sipendi Sana.
Nilinunua kitanda na godoro nilipokua chuo na kuvisafirisha Hadi home ili nije nipange lakini Bei ya pango ni kubwa mno sh 40 kwa mwezi nimeshindwa kulipa kwa miezi 3 120k Kwan hela nayopata inaishia kwenye chakula tu.
Rafiki zangu tuliosoma nao wakafeli Wana maisha mazuri wengi wameoa na wamejenga,m wapo mbali kimaendeleo sana
Nafikiria kivipi nitaweza pata hela nipambane na haya maisha ya mtaani
Kwa yeyote mwenye connection ya kazi yoyote halali mkoa wowote naomba anisaidie, nitaifanya kwa uaminifu na upendo kwani huku napokaa jamii inashindwa kunielewa.