Nikimwangalia Magufuli na Polepole nakosa imani na watanzania

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,528
Magufuli alitumia mwingi jukwaani wakati wa kampeni kunajinasibu kuwa yeye atakuwa rais wa wanyonge, mpenda haki na kwamba ataleta ajira kwa vijana kwa kuanzisha viwanda, lakini tangu ameingia madarakani hakuna alilolifanya zaidi ya kuumiza hao wanyonge aliokuwa anawatetea, sasa hivi anatenda ambayo hakuyahubiri na hali ya Mtanzania inazidi kuwa mbaya.

Mwingine ni huyu ni mwanasiasa kijana (ingawaje muonekano sio) huyu wakati wa katiba alijipambanua vyema, alijibu hoja kisomi na kiueledi zaidi, kila alipokuwa anazungumza kwenye vyombo vya habari kila Mtanzania alitega sikio kumsikiliza na hoja zake zilikuwa na mshiko kweli kweli, lakini leo hii hana jipya, ule uwezo wa kujibu hoja haupo tena, amebaki kuulizia madada wa watu.

Ni nani amewaloga wanasiasa hawa ambao kipindi hicho walijipambanua vyema.
 
Pole Pole kama asivyojulikana ni kijana au mzee ndivyo hivyo hivyo asivyojulikana msimamo wake. Sura inasadifu akili mkuu.
 
Mahakama ya Mafisadi ipo au haipo?

Viwanja visivyoendelezwa vimechukuliwa havijachukuliwa?

Ajira zinatangazwa hazitangazwi?

Elimu bure hadi sekondari inapatikana au la?

Mikopo elimu ya juu inapatikana au la?

Bei ya mazao kwa wakulima imeboreka au vipi?

Madawa ya msingi katika zahanati na hospitali yapo au la?

Miradi ya barabara na miundo mbinu inajengwa au haijengwi?

Kero ya usafiri hasa kwa Dar imetatuliwa au vipi?

Usafiri wa Anga twiga yuko angani au ?

Rushwa na ubadhirifu vimepungua au?

TULIAHIDI TUNATEKELEZA 2020 NI MAGUFULI TENA....!!

[HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG]
 
Mikopo ipi hii mnayotoa nusu nusu au hii ambayo asilimia inayopewa mikopo na asilia isiyopewa kubwa ni isiyopewa, Elimu bure ipi mkuu hii hii tunayoishuhudia ambayo shule zimebadilika zimekuwa kama sehemu za kuchangia michango ya harusi, Madawa yapi muhimu mkuu mama zetu kutembea na mikoba iliyojaa vifaa wakati wa kwenda kujifungua utadhani wanaenda kufungua famasi au hii ambayo nchi nzima chanjo za watoto zimegeuka kuwa kama maji ya uzima,Bara Bara zipi mkuu hizi jk alizitafutia hela au ni nyingine mmeongeza mpya mkuu,Kero ipi ya usafiri kwani mwendokasi ni Serekali hii ilijenga mkuu au ndio umeshalewa viroba, Bombadier imeweza kuleta impact gani kwa uchumi wetu au faida yake nini? au ndio kututia hasara ya ile iliyoenda kukamatwa huko Canada, Rushwa ipi imepungua mkuu trafiki wanachukua kweupe siku hizi bora enzi za jk tulikuwa tunawavizia kwa camera. Ujinga ni kutokuwa na akili na kusifia vitu bila hata aibu. Jinga Kabisa wewe.
 
Punguza jazba....
Mikopo nusunusu kwa fani gani?
Umesikia wanafunzi wakigoma kwa sababu ya mikopo??

Shule ipi inayokusanya michango ?itaje ili ishukiwe leo hii hii!!

Mama mjamzito kutembea na mkoba ni sahihi...hivi akiwa njiani akajifungua nani wa kumsaidia kama hana hata gloves?

by the way nitajie aina ya dawa anazobeba huyo mama uliyemsema kiasi cha kumfananisha na pharmacy.

Barabara zilitafutiwa fedha na JK...hiyo ni sahihi...na wala sio dhambi..kwani serikali ya CCM inafanya mambo kwa uendelevu...hata Baada ya Magufuli ataingia mwanaccm mwingine wa kumalizia ya Magufuli na kuanzisha mapya.
N.B ujenzi wa reli unaanza hivi karibuni...flyovers zinaendelea kujengwa kama tulivyoahidi.

Hujui faida ya AirTz kurudi hewani...unanichekesha sana!!
 
Mikopo ipi hii mnayotoa nusu nusu au hii ambayo asilimia inayopewa mikopo na asilia isiyopewa kubwa ni isiyopewa, Elimu bure ipi mkuu hii hii tunayoishuhudia ambayo shule zimebadilika zimekuwa kama sehemu za kuchangia michango ya harusi, Madawa yapi muhimu mkuu mama zetu kutembea na mikoba iliyojaa vifaa wakati wa kwenda kujifungua utadhani wanaenda kufungua famasi au hii ambayo nchi nzima chanjo za watoto zimegeuka kuwa kama maji ya uzima,Bara Bara zipi mkuu hizi jk alizitafutia hela au ni nyingine mmeongeza mpya mkuu,Kero ipi ya usafiri kwani mwendokasi ni Serekali hii ilijenga mkuu au ndio umeshalewa viroba, Bombadier imeweza kuleta impact gani kwa uchumi wetu au faida yake nini? au ndio kututia hasara ya ile iliyoenda kukamatwa huko Canada, Rushwa ipi imepungua mkuu trafiki wanachukua kweupe siku hizi bora enzi za jk tulikuwa tunawavizia kwa camera. Ujinga ni kutokuwa na akili na kusifia vitu bila hata aibu. Jinga Kabisa wewe.
Mmmh aisee!hivi unaishi Tanzania kweli mkuu,were you expecting kutia mimba halafu ukachukue mtoto hospitali tu,kupeleka shule mtoto halafu akute yunifom,daftari,kalamu,mwalimu,kiti na chakula darasani? Siasa sawa lakini mambo mengine ni aibu mno ! Mwanaume kupenda kitonga! Najua utasema unalipa kodi lakini una TIN number au ni hivi vi VAT ndo unataka vikuendeshee maisha! Wajibika maisha ni hayahaya na nchi yetu ndo hii hii.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kutia mimba mbona mkuu mwenyewe alibariki hilo suala au umesahau aliposema "Fyatueni tu" watasoma bure?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa wengi n wachumia matumbo.. si unaona jinsi lisu na mbowe na chadema wengi walivokua wanadai eti ssm na lowasa n mafisad halafu baadae wakaja kumsafisha bila aibu, sasa we wafate wanasiasa uone kama hutakufa maskn
 
Back
Top Bottom