Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,557
Wanabodi,



Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa! Ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere! Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!

Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea.


Ni kama Mwalimu kabisa!

Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.

Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga! akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga"

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?

Paskali
Update
nasikitika kusema hukumfahamu Nyerere. Endelea kumtafiti umjue vizuri
Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.

Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere! Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!




 
Polepole siyo mtu mstaarabu. Hawezi kushirikiana. Ili ushirikiane inatakiwa kukubali mtazamo wa wengine hata kama hukubaliani nao, kama vile ambavyo wao wanakubaliana na wewe hata wasipokubaliana nawe. Ukiona mtazamo wao ni mbaya sana basi unaacha kushirikiana nao mazima.

Sasa anaonekana kama mtu mgomvi tu. Unashikilia habari ya awamu ya 5 vs 6 ili iweje? Jambo lisilo na faida yoyote kwa nchi! Ni ugomvi na kukosa ustaarabu.

Mtu kama huyu akiwa rais ni rahisi nchi kuingia vitani, hawezi kucompromise.
 
Paskali kabla ya Polepole kuendelea kutupigia kelele aseme kwanza kwanini alitaka watu wanyamaze walipokuwa wakinyoosha nchi na sasa kwa nini yeye hataki kunyamaza wenzake wanapofungua nchi?

Haki ya kuongea anaitoa wapi ilihali wao hawakutaka wengine wapate haki hiyo alipokuwa akizunguka na Vee Eiteh?
 
Polepole siyo mtu mstaarabu. Hawezi kushirikiana. Ili ushirikiane inatakiwa kukubali mtazamo wa wengine hata kama hukubaliani nao, kama vile ambavyo wao wanakubaliana na wewe hata wasipokubaliana nawe. Ukiona mtazamo wao ni mbaya sana basi unaacha kushirikiana nao mazima.

Sasa anaonekana kama mtu mgomvi tu. Unashikilia habari ya awamu ya 5 vs 6 ili iweje? Jambo lisilo na faida yoyote kwa nchi! Ni ugomvi na kukosa ustaarabu.

Mtu kama huyu akiwa rais ni rahisi nchi kuingia vitani, hawezi kucompromise.
Ukishirikiana nao automatically umekubaliana nao. Polepole hawezi kuwa sehemu ya mafisadi.
 
Back
Top Bottom