Nikiingia ofisini nasikia usingizi, nifanyeje nisisikie usingizi?

Ndugu zangu wa JF,

Naombeni namna ya kufanya nikiingia ofisini asubuhi saa 2 nikikaa kwenye kiti tu nasikia usingizi wa ajabu mpaka najiuliza ni kwanini.

Sijui nifanyeje?
Acha kabisa kula viporo

Vaa nguo/funga mkanda pia Viatu visivyokubana

Unapokaa ofisini penda kuvua Viatu pia weka kitu kama mpira laini uwe unaukanyaga wakati wafanya kazi zako

Fungua mlango au madirisha ofisini kuruhusu hewa safi kuingia

Unapopata kifungua kinywa, kula kidogo tu, si lazima ushibe! Pendelea kula matunda zaidi na achana na vitafunio vya wanga kama chapati na vitumbua

Mwisho pata muda kuzungukia ofisi nyingine ndani ya jengo unalofanyia kazi hata kwa salam tu. Hii itakusaidia kuua usingizi unaoambatana na miayo mileeefu mpaka unatoa machozi.

Hapa Kazi Tu. Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
Asante mkuu
 
Mimi naona hiyo kazi unayo ifanya mwanzo ulikua ukipata marupurupu sasa hivi hupati.
Ila ninacho kushauri, fanya kazi ukiwa miguu yako ipo kwenye beseni la maji, hiyo ndio dawa ya usingizi ofisini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom