Carleen
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 8,592
- 29,545
Hi guys,
Hope mpo salama,
Nakumbuka ilikuwa jumapili moja hivi tulivu sikuwa sawa kiafya hivyo nilikuwa nimeamua niende hospitali moja ya kidini nikapime ili nijue kinachonisumbua,
Hivyo nikafika hospitali vizuri, nikafuata utaratibu wa registration na kupanga foleni ya kumuona daktari..!!
Nilivyoingia kwa daktari nikamuelezea vile nilivyokuwa naumwa huku yeye akiniuliza maswali na ku take notes kwa faili langu,
Baada ya hapo akanishauri kuhusu kupima HIV kwa hiari, moyo ukashtuka kidogo sababu sikuwahi pima hichi kitu hapo kwanza na huku pia nikiihofia sindano vile ni muoga nikamjibu tu haraka haraka nipo tayari ili asione kama sijiamini..!!
Basi nikaelekea maabara kwa ajili ya vipimo mbalimbali, to cut a long story short kimuhemuhe kikawa kuitwa kwa daktari kwa ajili ya majibu.!!
Nikaingia chumba cha daktari akanichangamkia vizuri tu kama mwanzo, akanipa majibu ya hasa kilichonipeleka pale,
Alivyomaliza akaanza sasa kunipa nasaha, alirudia mambo yaleyale ambayo mengi tulikwisha fundishwa shuleni, kwenye seminars na matamasha ila ukweli sikuwa na amani hata kidogo sababu sikujiamini, mapigo ya moyo yakaongezeka alivyoanza kuniuliza personal matters, kama wewe ni wa ngapi kwenu? Unaishi na nani, umesomea nini, upo kwenye mahusiano? and stuffs like that..!!
Nilipotaka kuzimia ni pale aliponiita jina langu na kuniuliza 'umeokoka'..?? Nikawaza nitasemaje nimeokoka wakati nishasema nipo kwenye mahusiano, na maana yake navunja amri ya 6 ya Mwenyezi MUNGU? Nikajibu tu Hapana, akauliza tena umenambia upo kwenye mahusiano wakati unakutana na mwenzio huwa mnakumbuka kutumia kinga??
Nikawaza kimoyo moyo looqh' salale nimekwisha, mwanaume mwenyewe ndo wa kwanza, nikajifanya kumuamini na kumpenda maana tulianza kwa kutumia kinga baadaye eti tukazoeana tukaacha, nikamjibu daktari huwa tunatumia ila si mara zote, akauliza 'mlipima ama huwa mna utaratibu wa kupima'?
Nikajibu Hapana hatukufanya hivyo, nikatamani kumuambia 'anavyoonekana innocent hata wewe ungekuwa kwa nafasi yangu usingekumbuka hilo'..
Basii daktari alianza kunihubiria mule ndani mpaka nikalia machozi, 'hivi unajua ni kiasi gani familia yako inakutegemea, uliwahi jiuliza ni nini kusudi la MUNGU kukuweka mahali ulipo sasa'.!? Aliongea mbaba wa watu mpaka nikahisi kutetemeka,
Alinishauri kuhusu kuokoka na kumtegemea MUNGU katika maisha yangu na hasa katika kuiishi ile kweli yake, akaniambia ni mapema sijachelewa nitubu naye atanirehemu.!! Hayo maneno yalinimaliza nguvu nikajua tu haya majibu nitayopewa hapa Leo ndo kwisha habari yangu..!!
Nikaanza kuwaza nikasema nikipewa majibu nipo salaama Leo sitaki tena mazoea na yule Kaka yaani anikome na namba zake nafuta, Nikaanza mtukana kaka wa watu kimoyomoyo, nikasema ole wangu nikipona leo sintokaa kurudia,
Akamaliza mazungumzo akaniambia niache kulia napaswa kubadilika akanipa majibu yangu, Sikuamini, nikasema 'ahsante MUNGU' mpaka akacheka, nikasema from now nishaacha mtu huko aliko sitaki ujinga tena, akaniandikia dawa akanielekeza chumba cha dawa, nikamshukuru, nikamtakia kazi njema nikatoka kuelekea chumba cha dawa,
Wakati nimempa file nurse wa chumba cha dawa ndo nakumbuka hivii nina simu kwa mkoba?? Nikatoa simu, nakuta missed calls na msgs za kutosha moja venye imeseviwa jina tamu inaniuliza 'honey umeshapata huduma nije kukufuata, ndo natoka job'..!!
Wooiiii, nikapokea dawa zangu nikarudi kukaa kwenye benchi ndo nikajiskia kuzidiwa kabisa na kudeka kukaongezeka nikisubiri kuja kuchukuliwa..!! Sijawahi kukumbuka kama nilimtukana na kumblock yule Kaka siku ile,😂😂
Mpaka Leo sijawahi jua ni kwanini yule Baba alinihubiria kiasi kile kiukweli, MUNGU ambariki tu popote alipo na anisamehe mimi mkosefu..
Happy weekend guys..!!