Nikifa Nitaitwa Hayati au Marehemu???

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
Jamani nisaidieni hapa naonaga watu wakibishanaga kwamba haya maneno ni tofauti................mimi naona nikifa nitakua Maiti tu, full stop.................
 
Hata mimi nilitoka kubishana kuhusu hili siku chache zilizopita, ukweli mimi sijui, lakini nahisi ukifa utaitwa maiti, ukishazikwa hapo utakua marehemu. Hii hayati watatusaidia wana JF
 
Jamani nisaidieni hapa naonaga watu wakibishanaga kwamba haya maneno ni tofauti................mimi naona nikifa nitakua Maiti tu, full stop.................

Ukifa unakuwa mzoga na unaoza tu full stop
 
Jamani nisaidieni hapa naonaga watu wakibishanaga kwamba haya maneno ni tofauti................mimi naona nikifa nitakua Maiti tu, full stop.................

Vyovyote utakavyoitwa! utakuwa umetoweka kwenye uso wa dunia hii!
La kujiuliza ni Je Kuna maisha baada ya kifo! Ufanye nini sasa ili baada ya kifo uweze kupata raha tere ......km zipo na si shida .......km zipo!
 
kifo (kama ilivyo ngono) kina nafasi ya pekee katika jamii zote duniani na ndio maana katika jamii zote duniani kifo (kama ngono) kina majina mengi.mfano kwa kiswahili tunasema fulani ametutoka,hatuko naye tena,mola kamuita,amefariki etc,kwa kiingereza has passed away,has gone to glory,is no longer with us etc ,hali kadhalika na ngono kulalana,tendo la ndoa,kut....,ku do,kulamba ,kudinya etc.Kutokana na hili hata kitendo cha kufariki nacho katika jamii kinakuwa na majina tofauti mfano kwa kihaya wanasema ta nanka yafa au ta nanka yatahya.hali kadhalika title ya aliyefariki katika jamii hutofautiana wahaya wana 'omubure nanka' na 'omugenzi nanka' na hapa katika kiswahili ndo inakuja tofauti ya marehemu na hayati, mfano Shk Karume
(RIP) na Mwl Nyerere ni hayati,bishanga nikipigwa chepe nitaitwa marehemu tu,you see the difference?simple,it is based on the status ya aliyefariki katika jamii kabla ya kifo chake.
yote kwa yote nawatakieni maisha marefu!
 
Kama una jambo la kukumbukwa/umeacha jina duniani utaitwa hayati mf hayati baba wa taifa nk,
kama ni mtu wa kawaida kabla hujazikwa utaitwa maiti badae ukishazikwa utaitwa marehemu,
 
kifo (kama ilivyo ngono) kina nafasi ya pekee katika jamii zote duniani na ndio maana katika jamii zote duniani kifo (kama ngono) kina majina mengi.mfano kwa kiswahili tunasema fulani ametutoka,hatuko naye tena,mola kamuita,amefariki etc,kwa kiingereza has passed away,has gone to glory,is no longer with us etc ,hali kadhalika na ngono kulalana,tendo la ndoa,kut....,ku do,kulamba ,kudinya etc.Kutokana na hili hata kitendo cha kufariki nacho katika jamii kinakuwa na majina tofauti mfano kwa kihaya wanasema ta nanka yafa au ta nanka yatahya.hali kadhalika title ya aliyefariki katika jamii hutofautiana wahaya wana 'omubure nanka' na 'omugenzi nanka' na hapa katika kiswahili ndo inakuja tofauti ya marehemu na hayati, mfano Shk Karume
(RIP) na Mwl Nyerere ni hayati,bishanga nikipigwa chepe nitaitwa marehemu tu,you see the difference?simple,it is based on the status ya aliyefariki katika jamii kabla ya kifo chake.
yote kwa yote nawatakieni maisha marefu!
Sie waislam hatuna kuitana Hayati...hayati ni uzima.
Tunaitana Marhuum...ina maana mtu mwenye kurehemewa...anaehitaji kuombewa na kuhurumiwa zaid...simwajua hatujui...kama ni mwema anaraha ndani ya kabr...au anpata adhab ndan ya kabr.

Hayo majina mengine yanaitwa kutokana na mazingira ya mtu...ukiwa mlevi usitegemee utaitwa marhuum...labda utaitwa Mfu!.
 
Hivi mbona kiswahili kigumu?ukiwa fisadi ukifa uanitwa hayati, ila ukiwa masikini ni marehemu.chukua chako mapema uwe hayati
 
Back
Top Bottom