Nikiamua kuacha kazi, mfuko wa PSPF watanipa stahiki yangu?

Pesa yake ya PSSSF ndo italipa madeni hayo na kama pesa haitoshi unatafutwa ulipe deni lako.
Ili uwe pensionable lazima uwe umechangia kwa muda usiopungua miezi 180 (miaka 15)
Kwa miaka yako 10 bado haujawa pensionable

Haipo hiyoo...
Watu kibao wameacha Kazi na halijatokea hilo.

Acha kuongea nadharia, vitendo vinatokea maofisini na tunaviona.

#YNWA
 
Kwa sasa hivi ni ngumu sana maana sheria zimebadilika sana. Kuna mambo 3

1. Acha kazi halafu subiri pesa zako hadi ufikishe miaka 60 ndio ukachukue.

2. Fanya kazi kufikisha miaka 15 ili uwe peshanable kisheria kabisa. ( unapata kiinua mgongo na pensheni kabisa)

3. Acha kazi kisha anza kuchangia kwa hiari hadi ufikishe miaka 60.

Vinginevyo ni ngumu sana.
Hili ndio jibu sahihi kabisa na ushauri mujaraab
 
Ndio.

Tz watu hatuna desturi ya kuweka akiba na kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ingekuwa tunawekeza sioni sababu ya mtu kufanya kazi mpaka unafikisha miaka 60 au 65 unashindwa hata kula hela yako vizuri.
Mm binafsi naona saa zngn mshahara hautosh alafu muda wa kufanya mambo mengine unakuwa mdogo kikubwa ss watumish wenye high income ni wachache sana yaani mwez mzm unafukuzia 450k na wengine ht hy haifiki mishahara imekopewa utakuta 250k maisha yote ndn ya utumish sasa jiulize unakuja kupata hela kubwa ukiwa na miaka 60-65 tofaut na hapo ni mikopo tu benk
 
Ngoja nikupe ushauri kama mtumishi mwezio......

1. Nenda NMB chukua mkopo wa Maximum value, yaani ule wa juu kabisa kulingana na mshahara wako.

2. NMB wakishakupa mkopo, nenda tena kwenye financial institute zile za kuacha Kadi nako kombaa mzigo mkubwa hasaaa.

Halafu mwisho wa siku potea.

Potea kama miezi 3 - 6 halafu Rudi kachukue barua yako ya kufukuzwa Kazi (utaikuta tayari kwenye faili).

Ila hakikisha huko uendako hufeli na unakujua vizuri.

Maana ukifeli huko SIJUI KAMA UTAKUWA TENA NA PAKUKIMBILIA.

#YNWA
Duuuh
 
Habari wakuu,

Naomba ushauri mimi ni mwalimu idara ya elimu msingi nimekuwa kazini kwa kipindi cha miaka 10 sasa. Nataka kutafuta Channel zingine za maisha nikiwa na maana ya kuresign mwenyewe. Nachouliza kwa kipindi hicho nilichotumikia kwenye mfuko wa PSPF watanipa stahiki yangu au laah?
Huo mfuko kwanza haupo,Kuna Psssf na nssf.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Kwa sasa hivi ni ngumu sana maana sheria zimebadilika sana. Kuna mambo 3

1. Acha kazi halafu subiri pesa zako hadi ufikishe miaka 60 ndio ukachukue.

2. Fanya kazi kufikisha miaka 15 ili uwe peshanable kisheria kabisa. ( unapata kiinua mgongo na pensheni kabisa)

3. Acha kazi kisha anza kuchangia kwa hiari hadi ufikishe miaka 60.

Vinginevyo ni ngumu sana.
Naomba ufafanuzi hiyo namba 2 ina maana ukishafikisha zaidi ya miaka 15 kazini je ukiacha kazi unaweza kulipwa kiinua mgongo na pensheni au
 
Yes, unalipwa mafao yako na kiinua mgongo pamoja na pension ya kila mwezi kama wastaafu wengine.
Unalipwa kiasi chote sasa vp ukifikisha muda wa kustaafu si utakuja kukosa hy hela uliyochukua mwanzo au sijaelewa?
 
Yes, unalipwa mafao yako na kiinua mgongo pamoja na pension ya kila mwezi kama wastaafu wengine.
Naomba kufahamu mahesabu ya kupata kiinua mgongo kwa mtu anayestaafu 2026 na pension yake ya kila mwezi inakuwaje? Mfano wakati anastaafu gross yake ni kama 2m hivi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom