Nikiacha Muziki nataka kuwa Waziri-Diamond

Carbondioxide

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
733
195
Diamond Platnumz amesema akiachana na Muziki anataka kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa zaidi kwa vijana.

Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM,Diamond alisema kama akiingia kwenye Siasa basi nia yake ni kuwa Waziri wa Michezo.

"Kwa sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye Siasa baadaye akimaliza mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo",alisema.

"Kile nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukiniambia sijui kuhusu mpira,movie mimi naweza kabisa nikiwa Waziri nikavifanya navikawa na maendeleo.In kitu ambacho naweza siyo nasema kuwa mbunge ila mimi nataka ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye Siasa basi.Na kuwa Waziri wa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na kuboresha vitu",alisema.

Diamond ambaye hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye Siasa kupitia chama gani,mwaka jana katika kampeni za uchaguzi mkuu uliomuingiza rais Magufuli kwenye za CCM na kutengeneza wimbo pamoja na video.
Source.Bongo5.com
 
Watanzania bana ukitoa ndoto za malengo yako wataanza kukuponda sasa nauliza kosa lake ni kusema malengo yake ama kuna mengine?
 
Kumbe anataka kuwa mwanasiasa, ni jambo jema maana na yeye ndo ndoto zake hizo.
 
Inawezekana kabisa kwa Tz,hakuna nchi rahisi kuongoza kama hii yetu tena hata jengo jeupe unaliweza maana pale Dom wapo kibao ambao hata hawajui wao ni akina nani.
 
nchi hii iko huru ko kila mmoja anawaza alitakalo na anafanya alipendalo ko acha nae afuate ndoto zake BUT asitegemee atafka huko kwa ujuz wa kutung mashair wakt watqzania 2naitaj m2 mchapakaz na ambae anaweza jtolea kwa hali au mali kuisaidia nchi ye2
 
hahahhahaha...anataka kuwa waziri moja kwa moja....hahahahahahah....yaani nchi hii bana...
 
akiacha mziki kwanza akasome halafu ndio aje kwenye siasa, ulimwengu wakisomi tunaokwenda nao otherwise atakua mzigo tu kwenye serekali
 
Tatizo hawa jamaa wakisikia Joseph Mbilinyi kawa mbunge vipindi viwili wanadhani ubunge ni sawa na fiesta. Pia wamemsika Joseph Haule wanaendelea kufikiria hivyo, ukweli ni kwamba hawa jamaa ni wasanii lakini ni namba nyingine!
Hebu msome Prof. Jay hapa alafu ndio utajua ametokea mbali kiasi gani na anaelekea wapi.
Japo hatukatishani tamaa!
j.jpg

Hapa wote ni wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano la 11 kushoto Mh. CECIL MWAMBE (Mbunge wa NDANDA) na kulia Mh. Mussa Rashid Ntimizi (Mbunge wa IGALULA) pamoja na mimi Mbunge wa Mikumi...
Sisi wote watatu tulisoma pamoja A-LEVEL mwaka 1995-1997 kwenye shule ya LUTENGANO HIGH SCHOOL iko Tukuyu MBEYA...
Mungu ni mwema sana , Mdogo mdogo Tutafika!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom