Nikamsikia akimwambia, ‘wewe ndiye mwanamke halisi’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikamsikia akimwambia, ‘wewe ndiye mwanamke halisi’

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Dec 15, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwaka 1990 wakati nafunga ndoa na mume wangu sikutarajia kwamba , ningekuja siku moja kumfumania na mwanamke yeyote. Alianza kunisimulia mama huyu, ambaye hapa ningependa mumfahamu kama mama Sikuzani. Alishusha pumzi na kisha kuendelea na simulizi yake ya mkasa uliompata muongo mmoja uliopita……………………

  Huyu mwanamke alikuwa ni mama wa mtoto mmoja. Hakuwa na ndoa na kazi yake ilikuwa ni kutumwa kufanya kazi za watu pale mtaani na kulipwa kidogo. Kazi kama kuchota maji, kulimia bustani na nyingine za aina hiyo. Alikuwa ni mwanamke ambaye amejipiga mahuru, yaani hakuwa anajali sana kuhusu mwili wake wala nguo.Sifa yake kubwa ni makalio makubwa tu, lakini hakuwa na sura wala kitu kingine ambacho mtu anaweza kusema kwamba, kinaweza kumbabaisha sana mwanaume.

  Mimi ni mwanmke, hivyo sijui mwanaume anavutiwa na kitu gani kwa mwanamke linapokuja suala la kujaamiana. Nakumbuka ilikuwa ni
  Mwaka 2000, nikiwa nimetoka kazini kwenye muda wa saa kumi siku ya jumamosi, niliamua kutoingia ndani kwanza. Niliona nipite hadi kwenye mabanda yangu ya kuku, ili kuona kama kijana anayenisaidia kazi alikuwa amefanya kazi zake vizuri. Nilipofika kwenye banda kubwa nilikuta mlango ukiwa wazi na nilijua ni yule kijana wangu wa kazi. Sikutaka kumsumbua, nilijua yuko kazini, hivyo niliona nikabadilishe nguo na kula kwanza ndio nirudi mabandani.Lakini wakati nataka kugeuza ili nirudi, nilisikia minong'ono.

  Niliamua kurudi nione ni akina nani wanaonong'ona. Nilifika mlangoni na kuchungulia bandani. Niliona nilichokuwa nataka kukiona, lakini hakikuwa nilichokuwa nimekitarajia. Hakuwa mtumishi wetu bali mume wangu wa ndoa. Alikuwa amemkumbatia yule mwanamke mchafu wa mtaa. Alikuwa anamng'ang'aniza kumvua nguo na yule mwanamke alikuwa hataki. Halafu badala ya kunong'ona, yule mwanamke aliongea kwa nguvu. ‘Hebu mheshimu mkeo we baba, ndio nini unataka kufanya. Halafu wewe afisa mzima utatembeaje na mimi. Kwanza siamini..'
  Mume wangu naye aliongea kwa sauti kidogo. ‘wewe ndiye mwanamke halisi, hujipodoi, huna nywele za bandia, hunukii pafyum, unanukia harufu halisi ya mwanamke... Tunaita kuku wa kienyeji, usijali, maofisa wengi wanapenda wanawake kama wewe...' Halafu niliona yule mwanamke akitupa kanga zake pembeni na mume wangu alianza kuhangaika kuvua shati.

  Nilijihisi kama vile nimenaswa na umeme na pumzi zilisimama na nilipotaka kuwakemea nilijikuta nimekwama. Nilipojitahidi kutaka kuwafuata nilijikuta sina nguvu kabisa.
  Bahati nzuri, yule mwanamke alitupa jicho mlangoni na kuniona. Alishtuka sana na kuinama na kukusanya nguo zake. Sijui zilitoka wapi nguvu zile.nilikurupuka na kwenda kumvaa yule mwanamke na kumwangusha chini, halafu nilimpiga hasa, huku mume wangu akiwa amesimama asijue la kufanya. Yule mwanamke alikuwa kipiga mayowe ya kuomba msaada, na ndipo mume wangu alipopata ujasiri wa kunishika ili nisiendelee kumtia adabu yule mwanamke hayawani.

  Nilimgeuzia mume wangu kibao na kuanza kumvurumishia mangumi mfululizo, hakumudu kujibu mapigo zaidi ya kujitahidi kujikinga uso nisimtie ngeu. Kumbe siku zote nilikuwa sijui kwamba nina nguvu kiasi kile. Ilibidi kijana wetu wa kazi ambaye ndio kwanza alikuwa anarudi kutoka mjini alikokuwa ametumwa na mume wangu ili ampe nafasi ya kufanya uibilisi wake aingilie ule ugomvi na kuamua.Yule mwanamke mchafu wa mtaa alishakimbia zake na kutokomea kusikojulikana, na hata kijana wetu wa kazi hakuweza kujua chanzo cha ugomvi wetu.

  Tukio lile lilikuwa ni chungu sana kwangu na sitakuja kulisahau kamwe. Bado niko na mume wangu, lakini tangu siku hiyo, amebadilika sana.

   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Dingi napita tu! Eti mwanamke halisi ni kama maza ama yule aunt wa ofisini kwako?
   
 3. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  huku kwetu kuna watu husema moyo wa mtu ulaya ..............
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu, mimi nilisimuliwa tu, sasa mbona unaniuliza maswali ya kunitega..........................
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Story ndefu sana sijaelewa chochote
   
 6. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  lakini jamani wake zetu nao mbona wanaparamiwaga na ma shamba boy na watembeza mitumba majumbani? halafu hao wapaka rangi kucha ndo usipime kabisa,haya mambo yapo bana na tusihukumu sana.
   
 7. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Bado yupo na mumewe lakini amebdilika kawa kawa je? Mtundu au mpole,mrefu au mfupi ufafanuz plz
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Asee......
  Yaani banda la uani?
  Come to think of it....mwanamke halisi.....!
   
 9. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,016
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa alikuwa na bonge la pointi ila alikosea pa kuitoa tu, lakini kiukweli wanaume tunavumila mengi yanayokera, mfano hayo madawa ya kichwani tu ni balaa, unalala naye usiku kucha, ukiamka asubuhi unajikuta tumbo limejaa gesi tele na mafua kibao...........:A S 465:
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa mama Sikuzani, kabadilika sana kitabia, kawa mwema, mpole na mwenye kujiheshimu sana tofauti na awali.............. baada ya tukio alijieleza kwa mkewe kuwa ni shetani tu alimpitia............ hata hakujua alitendalo!
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi bwana hebu nitumie ka pesa ka juice kwa mpesa wakati nasoma hapa huku nashushia
   
 12. Imany John

  Imany John Verified User

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  mbona kazi
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hebu nenda hapo jirani dukani kwa Mpemba, mwambie akupe Juice na Boflo, nitampitishia hela yake jioni nikirudi kutoka kwa shangazi Bonyokwa
   
 14. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wanaume hawajui wanacho kitaka... natural or not akiamua kukugeuka atageuka tu. Hapo alikua anamwambia yule mama hivo kwa sababu kuna kitu alikitaka kwake!
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwali, niliwahi kusoma sayansi kuhusu wanyama na tendo la kujamiiana. nilisoma kwamba, wanyama wanafanya tendo hilo sio miito ya kimwili bali kwa kukamilisha tendo la kuzaana, na tendo hilo hufanywa pale mnyama jike anapoonesha dalili fulani, na dalili hizo hutofautiana kutoka mnyama mmoja hadi mwingine..... kwa mfano mbwa, anasikia harufu ya mbwa jike anayetaka kuingiliwa kimwili ili apate kuzaa kutokea mbali, na ndio maana mbwa dume huenda umbali mrefu sana kufuata jike linalotoa harufu ya hitaji hilo, mbuzi hupata harufu ya hitaji hilo kupitia kwenye mkojo wa mbuzi jike na ng'ombe dume harufu hiyo huipata kwenye uke wa ng'ombe jike....................

  Je sisi wanaadamu hususan wanawake kimaumbile hawana mabadiliko ya kimwili pale wanapohitaji tendo hilo kwa ajili ya kukamilisha uzao? haiwezekani kwamba moja ya mabadiliko hayo yaweza kuwa ni harufu kama vile wanyama? Je haiwezekani kwamba mama mchafu wa mtaa alikuwa na kichocheo hicho cha harufu kumvutia mwanaume yeyote kwa sababu alikuwa kwenye heat period?..................
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  mwanaume mzinzi haangalii usafi wala uchafu, wote twende kazi!
   
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  hako nako ni ka pweint aisee,tafakari.
   
 18. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  .......Chukua hatua.
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mzee mwenzangu, nime-google ili kujiridhisha, wataalamu wanadai kuna harufu itokayo kwa wanawake walio kwenye heat period inayowavutia wanaume........ haiyumkini ndio maana kuna wababa wanawabaka watoto zao au ndugu zao wa karibu, jibu limeshapatikana ni kumbe ni natural smell aisee..............!!!!!!!!!!

  Hebu Bofya hii link: Men can 'sniff out' ovulating women - Thaindian News
   
 20. F

  Febby Kalage Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hili limeniacha hoi. Ila nadhani hapakuwa na haja ya kumpiga yule mwanamke maana hakupenda kutenda tendo hilo na mpaka akasikika akisema "linda heshima ya mkeo" nadhani hapo aliyepaswa kuadhibiwa ni huyo mwanaume. Anyway jambo la muhimu hapo ni kwamba mmesameheana na kuanza upya, ila chunga mwenzangu huyo mwanaume ni mzinzi, akiona makalio makubwa popote hataweza kustahimili. Huyo ni mlaghai tu na alikuwa anampamba hadi kumuita kuku wa kienyeji ili atimize azima yake lol .:lol:
   
Loading...