Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Jumapili iliyopita nilihudhuria misa takatifu katika Kanisa katoliki la Mt.Anoarite,Makuburi Dar es Salaam. Ni misa ya kuanzia saa tano na robo asubuhi. Katika misa hiyo ya kuadhimisha sikukuu ya Watakatifu Petro na Paulo,wanakwaya wa Kwaya ya Mt.Kizito walitumia, pamoja na ngoma na kinanda, vuvuzela kunogesha uimbaji wao. Vuvuzela lilitumika mwanzo hadi mwisho wa misa katika uimbaji.
Kiukweli,sijawahi kushuhudia vuvuzela kanisani (kanisa katoliki) wakati wa misa. Nikiri kuwa vuvuzela lilichagiza vyema uimbaji na kuufanya ujae baraka zaidi. Hongereni wanakwaya ya Mt.Kizito kwa ubunifu huu. Nilibarikiwa sana kwa misa nzima na uimbaji wenu. Vuvuzela liko juu...