Sitanii bali namaanisha hicho nilichokiandika. Ni muhimu sana kuongeza bei ya mafuta kwa gari ambazo si za abiria na mizigo. Hayo uliyoyasema yatafuata baadaye kwani utekelezaji wake si wa leo au kesho. Pia si lazima tuanze na bei hiyo niliyopendekeza. Hata kiwango cha shilingi 5,000/= kwa LITA MOJA ya mafuta kwa gari zisizo za abiria au mizigo kinaweza kuwa kizuri kuanza nacho na kupima matokeo yake ndani ya miezi sita.
Zumbukuku, wala sijakurupa. Ni lazima tukubali ukweli kuwa tumeelemewa kwa sasa kama taifa katika mambo mengi. Hapa sizungumzii kupandisha bei ya mafuta kwa ujumla wake. Kinachozungumziwa ni kupandisha bei ya mafuta kwa magari ambayo kazi yake si kubeba abiria wala mizigo. Hapa kuna tofauti kubwa sana. Na moja ya faida kuu ni watu kutumia muda mfupi zaidi kwenda sehemu zao mbalimbali za kuzalisha mali. Uamuzi huu utailazimisha serikali kuu na serikali za mitaa kufanya kazi ya ziada ili kuboresha usafiri wa umma.
kinachopendekezwa hapa ni kupandisha bei ya mafuta hayo kwa gari zisizo za abiria. Hii maana yake ni kuwa bei ya mafuta haitabadilika ila kama unatumia gari ambalo kazi yake si kubeba abiria wala mizigo itabidi ulipe shilingi 12,000 tu kwa kila lita ya mafuta utakayo nunua na kwa daladala na taxi wao wataendelea kununua mafuta kwa bei ya sasa. Hii itasaidia kupunguza sana magari binafsi na ya serikali katika barabara zetu hivyo kumaliza tatizo la foleni hapa nchini. Pia itatoa fursa nzuri ya kuwa na usafiri bora na wa uhakika wa umma.
Unless uwe unatania au unataka kuongeza posts tu,hili wazo lako SolarPower ni la kichekechea zaidi. Inajulikana wazi kabisa kuwa tatizo la foleni Tz ni barabara zake kuwa ndogo au finyu,kiwango/ubora duni, chache na sababu nyingine kibao. Barabara ziboreshwe na zipitike kwa urahisi,channels ziongezwe na wadau wali-suggest uwepo wa flyovers inapobidi. Nway kwa vile umetoa wazo,basi ngoja tulichukulie kama wazo tu!!
Hayo magari ya abiria yenyewe yako wapi sijui wewe uko mikoa gani kati ya ulioitaja, ukiwa barabara ya uhuru utaona watu wengi wanatembea kwa miguu, nenda morogoro road hali ni hiyo hiyo, vituo vya buguruni na ubungo kwa barabara ya mandela hali ndo mbaya zaidi,nenda kilwa road pia nyerere road kuanzia tazara kuelekea gongo la mboto, sijataja barabara ndogo kama za tabata, shekilango, bagamoyo ya zamani,si kwamba watu hawana hela ya nauli ndo maana wanatembea kwa miguu ni ukosekanaji wa magari ya abiria ndo maana inakuwa.
Labda ungeeleza wakishanunua kwa bei ya juu halafu ndo inakuwaje hiyo hela inaenda wapi au lengo ni kuondoa magari ya binafsi barabarani?
Sidhani kama unaupa ubongo wako muda wa kufikria vizuri! Una uhakika gani kwamba hayo magari unayosema ya abiria (daladala na taxi) hawatachakachua na kuwapelekea mafuta hao wenye magari ya starehe? Wazo lako halina tija!!
MWANZO NILISHTUKA NIKAJARIBU KUFIKIRIA HUYU MTOA MADA ALIKUWA ANAFIKIRIA KUTUMIA NINI KUFIKIRIA LAKINI BAADAYE NIKAMUWEKA KATIKA KUNDI LA SWALI LA PRETA. Kwa ujumla na hiki kitu kimekuwa kila siku twasema dawa pekee ya kuondoa foleni si kupandasha mafuta kama huyo mtu alivyofikisha ujumbe wako nia ni kufufua barabara na kuzianzisha mpya katika lengo la kupunguza foleni
:tonguez:Hivi nitakuwa na akili sawa sawa,ninunue mafuta TShs 12,000/= wakati jirani yangu ana taxi au dala dala ambalo anaweza akanunua yeye alafu akanifaulishia? Jaribu kubuni upya.
Hivi hapo si ndiyo unatengenezea ulaji hao wenye taxi? Mafuta watanunua sh 2000 kwa lita halafu watawauzia wenye magari kwa elfu 3 - faida ya bwerereeee!
Hii idea yako kwa kweli haiingii akilini hata kidogo samahani sana kwa hilo. Laiti usafiri wa umma ungekuwa mzuri na wa kuridhisha basi wengi wetu tungeziwacha gari nyumabani kwa hiari yetu.
ukishangaa ya musa utayaona .....
kwa sababu hivi vituo vya mafuta ni charity na si biashara? hawa wanaomiliki vituo vya mafuta ni wafanya biashara, wanahitaji biashara ikue na wanaajiri watumishi wanaohudumia, unapotaka kupunguza idadi ya magari kwa kuweka bei hiyo ujiandae kupunguza na waajiriwa wa vituo hivi na (inawezekana) ujiandae wimbi la uhalifu mtaani kwa kukosa ajira nk.
dawa ya kupunguza foleni ni kujenga miundombinu ya uhakika yenye kiwango bora na kukidhi mahitaji husika, upanuzi wa barabara ni muhimu, alkadhalika kuwe na njia mbadala za kutoha na si "ku-relay" na barabara moja!!
bila kusahau barabara za juu n.k
hata usafiri wa treni ambao kwetu bado ni ndoto ya mchana....
vilevile kwa barabara za ndani mijini(mfano jamhuri, samora, uhindini, mosque n.k) kuacha kupaki magari kando kando ya barabara na kusababisha ufinyu wa barabara unaoleta msongamano usio na sababu.....
nyingine unaweza kuongezea, ila hiyo solution yako mmmmh umetokota mjomba.....:A S tongue:
sijasema mafuta yapande bali ni kwa gari zisizo za abiria tu. Hivyo kama una taxi au daladala bado utaendelea kununua mafuta kwa bei ya sasa.
Hawataweza kuchakachua kama tukitunga sheria zenye adhabu kali na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria hizo. Kwa mfano ukipatikana na hatia yoyote katika mpango huu adhabu inakuwa ni kifungo kisichopungua miaka 12 pamoja na faini ya shilingi milioni 15 na viboko 36 .
Naomba usome POST YANGU NAMBA 41 HApo juu.
Mkuu, bila kupunguza idadi ya magari binafsi katika barabara zetu tusahau kutatua tatizo la foleni hapa nchini. Unachopendekeza ni sawa lakini ni suluhisho la muda tu hilo. Dawa ni kupunguza idadi ya magari binafsi katika barabara zetu pamoja na kuhakikisha kuwa barabara zetu zote zinapitika muda wote na zina ubora unaotakiwa. Mbali na kupandisha bei ya mafuta kwa magari ambayo si ya abiria, njia mbadala inayoweza kutumika katika kutatua tatizo la foleni ni kuanzisha KODI MPYA KWA KILA GARI LISILO LA ABIRIA LINALOPITA KATIKA BARABARA ZETU ZA LAMI KATIKA MIJI YA MWANZA, DAR ES SALAAM NA ARUSHA. KODI HII INAPENDEKEZWA IWE SHILINGI 25,000 KWA SIKU KWA KILA GARI LA AINA HIYO. Kodi hii italipwa katika vituo maalumu pale tu ambapo gari husika litakuwa nimeingia katika barabara zetu za lami katika miji ya Arusha Mwanza na Dar es Salaam. Kupitia kodi hii Serikali itakuwa na uhakika wa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 250 kila mwezi. Na fedha hizi zote itabidi zitumike katika kuboresha Elimu yetu katika ngazi ya Msingi na Sekondari.