nikadhani tanga nilikwenda kikazi kumbe ni mvutano wa kuifata damu yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nikadhani tanga nilikwenda kikazi kumbe ni mvutano wa kuifata damu yangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Doyi, Jan 10, 2012.

 1. Doyi

  Doyi JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 747
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  habari zenu magreat thinkers wa JF .mbarikiwe saaana kwa kuwa nyie ni sehemu ya maisha yangu maana humu jamvini japo kuna vimbwanga na vituko vya kila leo lakini kwa upande mwingine nimejifunza mengi saaana.shukurani kwa wana JF popote mlipo.
  kisa hiki jamani waungwana nimekichomoa mahali yaani copy and paste so wazeee wa madongo msiniumize sura nimetoa taarifa mapemaaa

  NANUKUU
  mimi ni mfanyakazi wa serikalini katika wizara fulani . kwa kweli bado sijaoa(nina mtoto) ila ndo hvo kimjinimjini ukikutana na mrembo mnamalizana maisha yanaendelea...hyo imekuwa ndo staili ya maisha yangu.Siku 1 nikasafiri kikazi kwenda bagamoyo kwenye semina kama ya wiki mbili hivi.......aaah kwani hata huko bagamoyo nilipitwa basii...kama unaamini hvo ni sawa na kuamini gavana wetu mstaafu balali alikufaga wakati.........mmm tuyaache hayo..ishu ni kuwa nikapata mwanamke hukohuko kwenye semina tukajivinjari sana ,tukala tundi kwa sana na ful KUPIGA PICHA za mikao ya kimahaba na zingine za kawaida.......ila wakati tunakula tundi muda fulani nakumbuka yule mwanamke aliniambia yupo kwenye sku za hatari so aidha nifanye kwa kinga au kama ninaweza yale mambo yetu yale niyamwagie nje.mmmh kinga skutaka kwa kuwa nilisha onja ile kitu yetu ilomzubaisha baba yetu adam na akaingia mkenge matokeo yake ndo haya dunia leo ipo kama ilivo pia kumwaga nje kwa kweli nahisi mtu akiniuliza mimi ni mwanaume..? naweza nikababaika kujibu kwa kutokuwa na uakika lakini akiniuliza unaweza kupiiiz nje? nina uhakika wa 900% kuwa SIWEZI...basi mzee mzima nikaserebuka nae mwanamke wa watu kavukavu.
  baada ya wiki kadhaa semina ikaisha (yeye alikuja bagamoyo pia kikazi kutoka kigoma na mimi kutoka dar).kila mtu akarudi katika mkoa wake na ahadi nyiiiingi za kuendeleza mapenzi.kama ujuavyo ndugu yangu mapenzi ya mbali kwa BAADHI yetu hatuyawezi tukaanza kupotezeana mpaka tukawa hatutaftani na huyo mwanamke tena. na nafkiri akabadili namba ya simu sjui maana nikawa simpati.nikamsahau maisha yakaendelea...
  ikapita kama miaka 15 hivi bado nikiwa mfanyakazi wa serikalini nikapangiwa kwenda mkoani tanga kikazi kama wiki 3. nikaenda huko tanga ila nikafkia kwa jamaa yangu ili niokoe ela ya hoteli nifanyie mambo mengine.jamaa yangu akanikaribisha vizuri alikuwa akiishi yeye na mkewe na kisichana cha kazi kwa umri kama miaka 14 au 15 kwa kadirio langu
  kwa kweli walikuwa wanakatesa sana haka kabinti mana walikuwa wanakatumikisha kama mbwa,bila hata mshahara, kalikuwa hakalali mpaka kamemaliza kazi zoote so kakawa kanalala muda mbovu kama saa 7 au 8 ucku kila siku kwenye stoo ya vyakula au jikoni na hapo jikon penyewe hata mbwa hastahili kulala sasa skuambiii binadamu.kalikuwa kamechakaa kwa mateso ya mule ndani.kila nkikaangalia nakaonea huruma lakini sina la kufanya naona naingilia maisha ya watu.ilikuwa ni kawaida kupitisha hata sku mbili hakajala kwa kuwa wao mara nying walikuwa watu wa kula makazini kwao au hotelini.sku 1wakakaambia kawapikie wali kwa kuwa watakula nyambani kakapika wali kakaunguuza ukawa hauliki na ilitokea hvo kwa kuwa kalisinzia wakati kanapika(nafkir kwa sababu ya uchovu wa kulala masaa machache).weeeee ilikuwa kosaa kalipewa kibano mpaka kakavunjwa mkono. kalilia saana mpaka usku wa manane na chumba changu kilikuwa na hapo anapolala yeye.nikaamka nkamwambia mwenyej wangu aamke tukapeleke hospitali kwa kuwa wamekajeruhi katoto ka watu. si jamaa wala mkewe hakuna aliyejali wala hawakukubali kukapeleka kupata matibabu.niliskia uchungu sana.kesho yake nikawa kuna kazi namalizia pale ndani ili niwah kazini nikiwa nimekaa sebuleni( wenyej wangu walikuwa pia wametoka kwenye mihangaiko yao ya kila siku) nikakaita ..kakaja kwa upole nikaanza kukahoji jina,mahali kalipotokea na kaliletwa na nani hapo..."hapa nililetwa na dada mmoja jirani yetu alinichukua kutoka kwetu kigoma kuja nifanye kazi ,mama yangu alifariki kwa hyo nikawa sina mtu wa kunilea ndo nimekuja huku tanga kutafta maisha" kakanijibu hivyo ....niliskia huruma sana ila nikashangaa kidogo maana kalikuwa kananiangalia kwa jicho kama la kunichunguza au kuniangalia kwa makini.nikaakauliza sababu ya kuniangalia hvo kwa makini kakajibu ... unajua anko nilikuwa cjapata nafasi ya kukuangalia kwa karibu na kwa umakini ila nahisi umefanana na mtu alipiga picha na mama kabla hajafariki.........ah nikaona haka kamechanganyikiwa na kile kipigo na maumivu ya mkono.....akilini mwangu nikachukue nikapeleke hospitali hata kama wenyej wangu watachukia potelea pote....nikakaambia haya kavae twende hospitali na uje na hyo picha unayosema kakaenda kuvaa fresh kakarudi kameshka picha mkononi...haa haaaaaa mwana JF hebu kisia nilichoona kwenye hyo picha....kisia basiii ili stori inogee..aisee nilihisi kuishiwa nguvu nikakaa chini kama nataka kupoteza fahamu...pale kwenye picha nipo mimi na yule mwanamke tuliekutana nae bagamoyooo miaka 15 ilopita.yani ni mimi kabsaaaa na yule mwanamke.na nikakumbuka tulivokuwa tunapga picha nilimwambia picha zile kesho yake mpiga picha akileta ampe yeye huyo mwanamke kwa kuwa mimi si mtu wa kutunza mapicha picha(nafkiri wanaume tulio wengi hatuna desturi hii kwa mawazo yangu).kumbe mwanamke wa watu nilimpa ujauzito akajifungua akalea kiumbe na akachukua picha na kumwambia mwanae " huyu kwenye picha ndo baba yako ila yupo dar sku ya sku huenda MUNGU akawakutahisha".baadae kabisa mwanamke wa watu akafariki mwanae akaja tanga kufata mateso na siyo kazi......nilitoka kwenda hospitali na huyo mwanangu kisha nikapitia kazini kuomba ruhusa kwa maana akili yangu haikuwa sawa mda huo....aisee naomba nikatishe hiii stori ila kwa kifupi ili kujiridhisha baada ya miezi kadhaa nilienda kwa wataalamu wa afya kupima vinasaba(DNA) na kweli nikakuta ni mwanangu halali(of coz hata kama ingekuwa syo mwanangu ngeish nae kwa kuwa ile coincidence ilinitisha sana) kwa sasa naish nae na anasoma kidato cha sita na nina mpango wa kusaka mke mwema atakaenilielea mwanangu kwa upendo kwa kuwa nikikumbuka niliokuwa nayaona sitaki yamrudie........MWISHO WA KUNUKUU

  jamani nafkiri hilo ni angalizo kuwa kwa wale wazee wa kupga kazi za nje bila kinga kila mnapoenda semina mjaribu kufatilia usikute mna watoto wenu wanahenyeka na dunia wakijua hawana baba kumbe nyie mpo na VISHTOBE vingine au wake zenu mnakula raha kumbe damu zenu zinateseka.....asanteni wana jf kwa usikivu na poleni kwa urefu wa kisa...cheers
   
 2. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ahsante ndugu naamini somo limeeleweka vizuri,
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Umeicopy and paste kutoka wapi? Ila duh km ni kweli imeniumiza sana
   
 4. m

  mbweta JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Miaka kumi na tano bado hujaoa anyway story inasikitisha sana.
   
 5. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  inasikitisha ,hapo wote baba na mama mnamakosa.
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  sasa uoe nini?
  Wakati bunduki inaanguka yenyewe kama kanga.

  We lea wanao, washakua hao.
   
 7. D

  Derimto JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nimejaribu kukaa nafasi yako nimeshindwa ila mkuu pole kwa kisa hicho.
   
 8. CPU

  CPU JF Gold Member

  #8
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  :shock: . . . . . :rant::rant:
   
 9. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Watoto wengi wa mtaani na wanaoomba barabarani ni matokeo ya wazembe kama wewe...ila nakusamehe kwa sababu hukujua kuwa umezaa.

  Ila sasa ndiyo haujaoa mpaka leo? Una hatari. Na usiendekeze ngono zembe tena.

  Mwisho, pole sana.
   
 10. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhh! Nawachukia sana binandamu wanaowatesa wenzao! Lakini pia sisi tujifunze kutokuwa sababu ya kuzaliwa watoto watakaoteswa maana dhambi hii itaanza kwetu!
   
 11. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kwakweli wenye tabia kama yako waache, kwani watoto wa mtaani wanateseka sana wkt kuna wazazi waliowazaa. Pole sana ndugu yangu. Mtu wa form six huitaji kuoa sasa, kwani huna uzoefu wa ndoa na kutokana na umri wako ulivyo si rahisi kuishi na mke, kwani uvumilivu utakosa.
   
 12. g

  georgelupembe Member

  #12
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa tabia zako ulizozieleza, isije kuwa nako ulikalamba !
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkuu Doyi hukujibu swali la DA hapo juu.
  N akwa kadiri ya maelezo yako, isipokuwa hii hadithi uwe umeikopi humu humu JF, inaonesha ni kisa chako mwenyewe. Kuna msemo wa kizungu unasema "wasiosema kweli wanapaswa wawe na kumbukumbu nzuri". Kosa lako hun akumbukumbu kuwa ulituambia uliikopi pahali kumbe huu mkasa umekutokea wewe. Angalia chini hapo kwenye nyekundu ulivyojichanganya.

  Anyway, ni kisa cha kusisimua na chenye ukweli wa vipi tunaishi. Bahati yako hcho kisichana kilkuwa na picha ya mama yake na katika maisha ya tabu, kama ingekuwa katika mazingira mengine na mtu mwenhgine angeweza hata kukichakachua hali ya kuwa ni mwanawe. Na hilo ndilo funzo kubwa tunalolipata kwenye kisa hiki.

  Hongera kwa kukutana na damu yako. Ushauri, mtafutie mama huyo msichana.

   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kuna watu wenye uzoefu wa ndoa kabla ya kuingia kufunga ndoa?
   
 15. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Sasa usitafute dogodogo maana kama binti amemaliza form 6 then atakuwa ana miaka si chini ya 20...ukitafuta dogodogo hawataheshimiana humo ndani. Tafuta mkubwa mwenzio mwenye busara zake na sio shangingi...
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Sina cha kusema,nafunga bakuli langu!
   
 17. Doyi

  Doyi JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 747
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Wakuu hcho kisa kipo na hakinihusu mimi...Kisa chenyewe kiliandikwa kwa luga ya kistaarabu sana ila mie nimeongezea vijimaneno vya kimtaani ili kunogesha.Ndugu Dena amsi nafkir ndo kilichovuruga unadhan nadanganya.anyway labda ni uandish wangu mbovu ila kuhusu kuwa na kumbukumbu ndogo may be ni maon yako.Nioe vp jaman wakat mi ni kijana mdogo namalizia masomo na cna hata mtoto wala cjawah kuzaa waungwana....Ni uandish tu huo kunogesha jamvi.Haya nakaribisha madongo mengne bandugu
   
 18. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  daaaah story inasikitisha hongera kwa kukutana na mtoto wako
   
 19. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Dah hii coincidence ni balaa. Kwa kweli naanza kuamini Mungu yupo aisee, hii haiwezekani itokee hivi hivi , Mungu yupo aisee dah!
   
 20. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Acha ngono zembe mkuu, bahati yako umepata mtoto na sio ukimwi. Jaribu kufuatilia semina zote ulizokuwa unaenda unaweza kuta wapo wengine. Ila hongera sana kwa kumuokoa mwanao kutoka kwenye mikono ya wanyang'anyi.
   
Loading...