Nijuzeni kuhusu kodi ya ongezeko la thamani (value addad tax)

Ni aina ya kodi ambayo hutozwa katika kununua na kuuza bidhaa au utoaji wa huduma au ni kodi inayotozwa katika ongezeko la thamani ya bidhaa

Hii kodi inatozwa katika namna kuu tatu kuna standard ambayo ni 18% na 0% na nyngne ambazo hazipo katka sheria ya kodi.
 
Naomba mnieleweshe kuhusu kodi ya ongezeko la thamani (value added tax) na inavyofanya kazi
KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT) ni kodi anayolipa mlaji/mtu wa mwisho katika kununua bidhaa au kulipia huduma ambazo zinakubalika kulipia kodi hii

1. USAJILI WA VAT
Mfanyabiashara anatakiwa kusajili VAT baada ya kuwa na mauzo zaidi ya mil 100 kwa mwaka. Usajili wa huduma za kitaalam zinazostahili kutozwa VAT hufanyika bila kujali mauzo ya huduma kwa mwaka. Vlvl serikali na taasisi zake zinazofanya shughuli za kiuchumi za kujipatia kipato nje ya kazi zao za msingi zinatakiwa kusajili.

2. VIWANGO VYA VAT
Bidhaa, huduma, uingizaji na uagizaji wa bidhaa na huduma toka nje na kuingia Tanzania bara hutozwa 18%
Kuuza bidhaa nje ya Tanzania hakuna gharama za VAT

3. KUWASILISHA RITANI ZA VAT
Mfanyabiashara aliesajiliwa na VAT anatakiwa kutumia mashine ie EFD machine. Pili, anatakiwa kuwasilisha hesabu za ritani siku ya 20 ya mwezi unaofuatia
Kwa kifupi ni hayo
Maelezo zaidi waweza kupitia vyanzo hivi
1. Kitabu kidogo KODI NA USHURU MBALIMBALI 2017/2018 Toleo la Julai 2017
2. Sheria ya kodi ya ongezeko la thamani Sura 148 na sheria ya fedha

Nawasilisha
 
Mleta mada labda ungeuliza swala mahususi ambalo ungetaka kujua kuhusu kodi ya ongezeko la thamani VAT maana ni swala pana kuweza kuli elezea lote humu!
 
Back
Top Bottom