Niishije na shemeji yenu

ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
4,324
4,034
Niliwahi kuoa nikamuacha mke wangu wa kwanza na kwa sasa niliamua kuishi tu na mtu kama mke na mume, kwa bahati nzuri amepata ujauzito, tupo karibu kimazungumzo kama mtu na mdogo wake yaani nikitoka kazini saa 12 natembea nae mazoezi au kuangalia movies bandika bandua mpaka saa tano.

Nahisi nakosea kwani hata mke wa kwanza ilikuwa hivi na nilikuja mchoka na kumuacha. Kuna kijiwe rafiki yangu fulani hivi mtu mzima nilimkuta nilishangaa na kumuuliza kwanini upo kijiweni alinijibi "nikikaa nyumbani mama yako nitakwaruzana naye si unajua wanawake walivyo akikuona upo upo lazima akutibue".

Sasa na mimi kwa huyu nilienae nimemuona sometimes yupo hivyo si nimeanza kutafuta vijiwe vya kukaa ili nibadili sura ya kushinda nyumbani jioni mpaka usiku je itasaidia na ki ukweli kijiwe sikiwezi kabisa.

Nishaurini wakuu
 
Mkuu maisha ya ndoa hayana fomula kwamba ukifanya hivi au vile basi mambo yatakua sawa.
Kila mtu ana njia yake ya kuendesha familia yake.
Ndio maana hata ukichukua sampo ya watu wanaoendesha familia zao kwa mtindo mmoja unaweza kukuta kati yao zipo zenye shida na zenye amani.
Fanya mambo yatakayo kupa furaha wewe na familia yako lakini kumbuka kuwa na mipaka na kuheshimiana kati yenu.
 
Ndo maana wazee hawanielewi, na mi nawaangalia tu. Sio lazima kuoa, nitaoa nitakapokuwa tayari...
 
Mkuu kaa vijiweni vinasaidia pia kwa namna moja au nyingine

Pia uyo mzee wa makamo amesema point kukaa kaa ovyo nyumban kunaibua vi ugomvi vya ap na pale

Kaa kijiweni ukirudi unapiga msosi kujulian hali alf unajilia vyako

Alaf usiseme uwezi unaweza sana sema ujaamuwa
 
Ukikaa na mtu sana unamchoka fasta . .fuata ushauri wa mzee hapo
 
Back
Top Bottom