Niishi vipi na huyu jamaa yangu

Niishi vipi na huyu jamaa yangu

Ulifanya kosa kubwa sana kuhamia kwa huyo rafiki yako.Wewe ni mtu mzima sasa unatakiwa uishi maisha yako independent uwe na vitu vyako vya ndani na sio kitumia vitu vya marehemu. Ukikaa hapo nakuhakikishia akili yako itadumaa,pia mtaanza kukwazana na huyo jamaa au mke wake,nakushauri kwa nia njema kuwa wewe kama mtoto wa kiume unahitaji kujijenga,unahitaji kuwa na privacy yako,unahitaji kuwa na samani mbalimbali na kwa kumalizia unatakiwa kujitegemea. Mambo ya kukaa wanaume wawili kubebana yameshapitwa na wakati. Grow up brother.
Hama. kuanzia hii wiki tafuta ustaarabu wa kuhama fasta. yaani isiwe ombi na hauhitaji kuburgain na rafki yako. Wewe ni mtu mzima una haki ya kufanya maamuzi sahihi wakati sahihi ambao ndio huu.

Thanks bro, thus why naipenda sana jf., ubarikiwe sana kwa ushauri wako mzuri
 
kizazi cha wanaume kinazidi kuteketea...... hili umeshindwa kuamua mpaka ulete jamvini.....
 
Nadhani unge muliza swali lake ana maana gani huenda ukamuelewa vibaya kumbe sio maana yake,na vile vile huyo nibinadamu hata kama una leta huenda anahisi anakufanyia mengi labda kusafisha nyumba kupika na mengine,na hata wewe huna uhuru wakufanya yako au hata kama una rafiki yako hawezi kuja au hamuwezi kukaa late night,chamsingi hama kama hali yako ina ruhusu..
 
Bila shaka mu bukheri wa afya,

Kuna jamaa yangu ameniomba sana niishi nae ktka nyumba ya kupanga ambayo anaishi yeye na mkewe na mtoto wao mmoja.

Kisa kiko hivi, hiyo nyumba alikuwa anaishi na mwenye nyumba ambae amefariki kama wiki mbili hivi. kwa kuwa nyumba ni kubwa jamaa yangu kanimba nichukue na mimi chumba hapo kisa yeye anaogopa kuishi hapo peke yake na et nkikataa hata yeye atahama.

kwa kuwa hata mimi nilikuwa ninaharakati za kutafuta nyumba nyingine ya kupanga nikaona nimkubalie kwani nyumba yenyewe ina kiwango kizuri.

Tatizo lililonifanya niombe ushauri ni hivi, toka nihamie hapa tumekuwa tukishea chakula means nakontribute then shemeji anapika chakula cha wote. Lakini jana shemeji kanifuta usiku wakati nakula cha chakula cha usiku akaniuliza swali ambalo nilishindwa kumjibu papo kwa hapo, kaniuliza hivi "Shemu tutaendelea kula pamoja au utaanza kujipikia chakula chako?" kwa kweli nilimwambia anipe muda nitafakari! Huku nikiwaza amefikiria nini kuniuliza swali kama lile!!

Kujipikia sio tabu lakini sasa kwa jinsi tunavyoishi na huyu jamaa yangu cjui atanielewaje. Maana tunashea sebule na kila kitu tulichokikuta hapo, mi naingia chumbani kwangu nae anaingia kwake.

ushauri wenu wadau. Ingekuwa ww ndo mimi ungechukua uamuzi gani katika hili!!?
Tafadhali sana,jitegemee haraka sana,laa sivyo yatakukuta yafuatayo:
1.huyo mkewe atakuingiza majaribuni na utamla na mgombane na rafikio
2.huyo jamaa yako atakuomba ma tako
 
Mimi ninavyoona ni kuwa kabla ya wewe kuhamia hapo....huyo jamaa yako na mkewe walikuwa na utaratibu wao wa kupata mlo ambao pengine ulikuwa unampa unafuu huyo mwanmke kuingis jikoni mara kwa mara.....,

Baada ya kuhamia wewe imemlazimu kuingia jikoni kwa kuwa walaji wameongezeka.....

Sasa hiyo hali ya kuingia jikoni mara nyingi tofauti na alivyo zoes ndio imekuwa kero kwake.....

Na hapo amefikisha ujumbe kwa jinsi anavyokwazika na hali hiyo....ni jukumu lako kuchukua hatua.......
 
Kuishi na watu nyumba moja halafu kila mtu awe anajipikia ni hali nisiyoipenda kabisa.

Inaleta awkwardness flani hivi.

Siwezi kabisa kuishi namna hiyo.

Ningekuwa wewe ningehama. Kwanza wala hata nisingehamia.

Ningetafuta sehemu yangu niishi mwenyewe kwa uhuru zaidi.

Mambo ya kuchangia chakula na watu mwishowe huwa yanaishia pabaya tu.

Hapo umeulizwa hivyo usikute wenzio wameshakusoma na kukuona labda unakula mno kuliko unavyochangia.

Kwa hiyo jiongeze mwenyewe hapo.
Well said bradha ngabu
 
pole sana kaka, wewe hama tu, afu mbona kuishi kibachelor tena peke yako ni uhuru zaidi? mzee ulipakua firigisi nini kabla ya rafiki yako wakati wa kula? hapo lazima shem amaindi.
 
Nakushauri kwanza uache kula nao pamoja na umwambie rafiki yako umehamua hivyo na pili utafute nyumba sehemu nyingine na umwambie unahitaji kuwa na privacy zaidi au umwambie ukweli tuu usiogope.

Kwanza nashangaa umekubali vipi kuwa una share chakula au jiko moja na mtu mwenye familia kabisa... Hii wanawake wengi kamwe hawawezi unakuwa kama na wewe umeoa... Bora hata ungekuwa ni ndugu wa huyo jamaa wala asingaliona shida kabisa.

Kiukweli wewe ndio ulitakiwa kuwa wa kwanza kufikiri utakula kwake huyo jamaa mpaka lini na mtu ana familia yake na hata kama una changi? Hukufiri lazima itakuletea matatizo siku moja?

Wanawake wana matatizo sana na huwa ni vyanzo vya ugomvi lakini kwenye hili wewe hukufikiri vyema kabla ya kukubali ombi la rafiki yako.
Acha kula hapo na pia utafute nyumba nyingine...
 
Huyo ni mke wa mwenzio oa wako na ww upikiwe...amechoka kukupikia ndio mana amekuambia live...
 
Kama una mda mfupi uamie,acha kushare chakula..kulee mtaani,usitumie sebule yao.jipe miezi 3 ya kujianda kuhama ili jamaa asikufikirie vibaya..apo tatzo ni mwanamke.
 
acha unafiki mwite rafiki yako akiwa pamoja na mkewe huyo unayemwita shemeji weka hao chini waambie asanteni nami nitaanza kujipikia na kama kweli we ni mwanaume tafuta mwanamke weka kwako ndo ukubwa huo
 
sisi wanawake sijui tuna roho gan chakula tu kinamtoa mtu roho mjib uyo shemeji yako kuanzia leo utajipikia mwenywe uku unatafta ustaarab wa kuhama usije gombana na rafk yako sbbu ya mkewe hama
 
Back
Top Bottom