Nihurumie mgombea weye wa ........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nihurumie mgombea weye wa ........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by walonge, Aug 29, 2010.

 1. w

  walonge Member

  #1
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kila ninapojaribu kufuatilia mwenendo wa kampeni wa mgombea wa chama kilichokuwa kikitutawala nimekuwa nikitamani kusikia jambo moja kubwa. Kimsingi hali halisi ya maisha hapa Tanzania sio nzuri kwa waliowengi na hili sihitaji ubishi. Ila natakakujua ama kusikia kutoka kwa mgombea huyu aombaye urudi tena madarakani, Je, ni wapi ambapo serikali yake ina kiri mapungufu ya kifikra, kiutendaji na hata ki imani ambapo imepelekea watu kuzidi kuwa masikini? Natamani kujuwa udhaifu wenu na sio kujisifia kwa mafanikio pekee.
   
 2. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,074
  Likes Received: 15,723
  Trophy Points: 280
  that is your intention sio lazima afate unavyotaka wewe
   
 3. w

  walonge Member

  #3
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Je, ina maana kuna sababu ya msingi inayoweza kuwafanya haya yasiwe mambo muhimu kuyasema? kumbuka ukitawala watu wanakupima kwa mambo mawili nayo ni mafanikio yako na mapungufu yako. Sasa unapozungumzia mafanikio pekee na kuyaacha mapungufu yako unatowa picha gani kwa jamii? Kumbuka kila mwenye nafsi ana mapungufu yake ila kilichomuhimu ni kuwa mkweli wakujifunza kutokana na makosa na kuwa muwazi katika kukiri kosa ili tutambuwe nia yako.. Tunataka Rais anayetambuwa pia makosa yake na sisi kumuamini kuwa hatoyarudia tena kwa yeye mwenyewe kukiri hadharani mapungufu hayo. Vinginevyo watu watatumia makosa hayo kumnyima kura kama ambavyo upepo unavoonekana kumuendea vibaya kwa wafanyakazi. Ikiwa wewe ndio unamshauri mgombea asiwe tayari kukiri mapungufu basi juwa unampeleka pabaya kwani makovu hayo hakuna wakumfutia kwalioathirika ni yeye mwenyewe atamke.
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Wanaamini wakiyasema mapungufu watanyimwa kura.
   
 5. w

  walonge Member

  #5
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Sasa wasiposema wao wenyewe huoni kama wanawapa nafasi wabaya wao kuwasemea na hiyo si ndio itawaumiza zaidi? Muhimu hapo ni kukiri ili usamehewe na huo ndio ushauri wangu wa bureeeeeeeeeee!
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ulikuta wapi kwenye politics wakionesha madhaifu? Hata chadema walipoambiwa hawana demokrasia kwa kumnyima Zitto nafasi ya kugombea uenyekiti uliona walikubali kosa? Hata walipoambiwa kuwa imekuwaje wabunge wote wakuteuliwa (isipokuwa mmoja) wametoka Kilimanjaro na hata Tarime kwa chacha wangwe ambako ndo waliongoza kwa kukpata kura nyingi kuliko jimbo lolote la chadema (including Kilimanjaro) walikubali? Chadema walipopata hela kutoka kwa mfadhili halafu Mbowe akasema nimeikopesha chadema walikubali? Namengineyo mengi. So please do not write non sense.
   
Loading...