Nigeria: Mchungaji apigwa risasi 40 bila hata moja kupenya mwilini mwake

Dmfnh8eXoAIXGDm.jpg



Kama ametoka salama hatakiwi kusikitikia chochote zaidi ya kumshukuru Mungu
 
Kuna dini flan inasema kuwa; Mnyazi Mungu Subhanah taalah ni kun faya kun. Yaani husema likawepo lisokuwepo. Kwa nini unasema ati kuwa alikuwa katumia juju?? Hapana, hiyo ni kazi ya Mnyazi Mungu kukinga mja wake. Ka siku yake haikuwa hiyo, kinga ya Mungu ni kuu. Ili zisisemwe kuwa hazikuwa risasi ndo matobo hayo yakatokea. Hukumbuki za TL 38 zote zikaingia mwilini lakini hakuna ya kumuua?? Wahitaji risasi 1 tu mumuangusha tembo wala sio 40. Acheni Mungu aitwe Mungu tu. Na nyiye mnaotaka kuua wenzenu, mtaaibika saana tu miaka hii kwani risasi sasa ndo zinakuwa "maji maji".

Haya yoteeeee unaandika nini.. unajua tofauti ya kuingia na kutokuingia.. na hizo 38 uliziona zikimwingia.. acha uongo na kuanduka upupwu.. kuniletea ya siasa zeny kwenye uzi huu.. eeeeh ukiona vipeee jipige vibao ulie..
 
Wakati ulimwengu ukibuni njia ya kuweza kubuni mavazi ambayo yatazuia risasi kutokupenya kiurahisi kwenye mwili wa binadamu, hii ni tofauti kwa Mchungaji wa Kanisa la Grace and Power Prophetic Ministry International, David Elijah kutoka Nigeria ambaye wiki iliyopita amenusurika kifo kwa kushambuliwa kwa risasi akiwa njiani kuelekea kanisani.

Mchungaji David siku ya Ijumaa Septemba 7, 2018 akiwa mjini Awka, Anambra huko Nigeria alikuwa anaenda kanisani kwake akiwa kwenye gari alivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto na kuanza kumfyatulia risasi.

Gari hilo lilitobolewa karibia lote kwa risasi lakini mpaka maaskari wanafika eneo la tukio, walimkuta mchungaji David Fulana yake ikiwa yenye matundu ya risasi huku mwili wake ukiwa haujajeruhiwa hata kidogo.

Hata hivyo, maaskari hao walimkamata kwa mahojiano zaidi huku wakitahamaki tukio hilo kwamba amewezaje kupona kwenye shambulizi hilo.

Tayari Jeshi la Polisi katika jimbo la Anambra limemuachia Mchungaji huyo siku ya Jumamosi baada ya kujiridhisha kuwa mtu huyo alikuwa salama na ni raia mwema.

Mchungaji David anatajwa kuwa moja ya wachungaji vijana wenye utajiri Mkubwa nchini Nigeria. Baada ya tukio hilo la kushambuliwa jana David alionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameshika maburungutu ya fedha huku akiweka Captions kuwa yupo nchini Malaysia kikazi.

Maoni mengi ya wadau mitandaoni nchini Nigeria yanaonekana kushangazwa na tukio hilo, huku wengi wao wakidai kuwa Mchungaji huyo anatumia nguvu za giza.
September 7,why???
 
Hii habari niliisikia
Hapo akarudi kanisani kutumia kuhubiri waumini wamuamini eeeh

Kwa kweli hii ni biashara kubwa ya udanganyifu kwa wengi inasikitisha kutumika katika jina la Mwenyezi Mungu.. wengine uenda mbali kutumia kinga za juju risasi zisiwaingie hata majambazi.
@cocochanel alifanyaje fanyaje mpaka ikaonekana kama ni kweli,Kumbe udanganyi???
 
ACHENI KUDANGANYWA!!!!
kilichotokea hapo,
1. Pasta anachana shati lake matobo sehemu tofauti kwa msumari na kuyatanua au mkasi pia ukiwemo
(tazameni hayo matundu sio ya risasi kwa anayejua risasi)
2.Pasta baada ya kuchana hayo matundu anakwenda sehemu ya mbali iliyojificha na kulishambulia gari lake kwa risasi ili liwe na matundu.
3. Anatembea kwa mwendo wa kasi ili watu wasi note yale matundu mpaka sehemu anataka a create ile scene, anapiga sisasi za maana na wanatoa taarifa polisi(zinapigwa juu tu, ili watu wasikie), ( bunduki yaweza kua yake au ya rafiki au mtuvameajiriwa)
4. skendo ya yeye kutojeruhiwa na risasi inazagaa
na WAJINGA WENGI WANAANZA KWENDA KANISANI KWAKE NA KUMPA MICHANGO KUAMINI YEYE NI WAAJABU, Ila ukweli nikwamba akikutana na wale wasiojulikana zinamtoboa na anapotea.

FUNGUENI AKILI ZENU JAMAA ANATAFUTA PESA HAPO HAKUNA JIPYA.

I'm out!
Duuh aisee cocochanel huyu amekujibia swali langu kwako.
 
Kwa sauti kubwa... hii ni mbinu ya kibiashara nayo kama matangazo ya biko. Hapo subiri kondoo watakavyo mwagika kanisani kwake
 
Mungu angalia akiokoa watu wake. Kama aliwaokoa akina Daniel katika tundu la simba hili pia aweza Fanya.
 
Nasikia kafanya igizo ili ajaze nyomi kwenye kanisa lake alipigwa kama mchezo wa kuigiza na blankoo bulet
 
Back
Top Bottom