EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,320
Anukaenyi Bob-Manuel Ogochukwu
Raia mmoja wa Nigeria amekamatwa na kete 66 (kilo 1.115) za heroin alizodai ni za drug lord wa Kitanzania. Anukaenyi Bob-Manuel Ogochukwu (43) amekamatwa na dawa hizo mara baada tuu ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos akitokea Nairobi na Ethiopian Airlines. Kete hizo zilikutwa tumboni mwa Mnigeria huyo.
Katika mahojiano yake na mamlaka husika, Mnigeria huyo amesema kuwa aliamua kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa sababu ni drug lords pekee ndiyo wameonyesha nia ya kumsaidia kifedha kulipia gharama za matibabu ya mtoto wake (4) aliyelazwa hospitali Nairobi akisumbuliwa na ugonjwa unaotishia kuchukua uhai wake.
Mnigeria huyo ambaye ameoa Mkenya, amesema: “Nafundisha kwenye shule ya kompyuta iliypko Onitsha, katika jimbo la Anambra. Hii ni mara yangu ya kwanza kusafirisha dawa za kulevya. Nilisafirisha heroin kumnusuru mwanangu mgonjwa. Daktari amesema kuwa mwanangu ana shimo kwenye moyo wake. Mwanangu yupo hosipitali anapambana kuishi. Nimekutana na watu wengi lakini hakuna aliyekubali kunisadia ispokuwa drug lords. Drug lord aliyenipa heroin anatoka Tanzania na alihaidi kunilipa Dola za Kimarekani 2,000 kwa ajili ya gharama za matibabu ya mwanangu. Nina wasiwasi sana na hali ya mwanangu”.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa mamlaka ya dawa za kulevya Nigeria (NDLEA), Kanali Muhammad Mustapha Abdallah (retd) amesema kuwa mwanae kuwa mgonjwa siyo kigezo cha kusafirisha dawa za kulevya. Amesema “maelezo ya mtuhumiwa siyo kigezo cha kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Usafirishaji wa dawa za kulevya ni kosa la jinai na mtuhumiwa atashtakiwa kwa mujibu wa sheria. Kitendo alichokifanya mtuhumiwa kimefanya hali yake kuwa mbaya zaidi kwa sababu atashtakiwa kwa kosa la jinai wakati mkewe sasa atakuwa na jukumu la matunzo wa mtoto wake mgonjwa.
Mnigeria huyo atashtakiwa kwa kosa la kumiliki na kuingiza nchini Nigeria dawa za kulevya za heroin na adhabu ya kosa hilo ni miaka isiyopungua 15 jela.
Vyanzo:
- NDLEA arrests man with heroin at Lagos airport - Tribune
- I ingested 66 wraps of heroin to save my sick son – Computer instructor
- NDLEA Arrests Heroin Importer at MMIA
- Man Smuggling Heroin Into Nigeria Apprehended at Lagos Airport | Sahara Reporters
- NDLEA arrests man over heroin importation - Nigeria Today