Nifungue duka la nguo za kike au za kiume?

sheremaya

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
3,321
7,629
Ndugu zangu,

Majibu yenu hapa yatanipa mwanga wa kuweza kuamua nifungue duka lipi kwa ajili ya nguo za wanawake tu au nifungue duka kwa ajili nguo za wanaume au nifanye vyote kwa pamoja kwenye duka moja sitaki kuwamba hela au kuwakopa hela, naomba mawazo yenu ndugu zangu ili niweze kupata hela.
 
Bidhaa za jinsi KE huwa zinauza haraka, iwapo utakuwa makini katika uchaguzi wa bidhaa husika, maana bidhaa zao zina msimu.

ubarikiwe mkuu nimepata nyama kwenye ubongo kwa mana iyo hata navochukua mzigo nisichukue mwingi kwa ajili kwenda na fashion isije ikapita alaf bado nipo na mzigo dukani
 
Wanaume wagumu kweli kununua nguo... Fungua duka la nguo za kike au kama unachanganya weka nguo za kiume kidogo sana

....Ni kweli wanaume wagume kweli kujinunulia nguo zao ila ni wepesi kweli kuwanunulia wanawake nguo zao....halafu wanawake nao kuwanunulia wanaume nguo mmmmh, mpaka watishiwe kwamba kuna nyumba ndogo anahonga....
 
uza zote ila zakike ziwenyingi kuzidi za kiume. Angalizo nguo za kike zinaenda na fashion hivyo hakikisha unakuwa namali mpya kila mara pili nguo zakike zinafaida ndogo kulinganisha na zakiume wakati huo huo za iume zinatoka taratibu ila zinafaida kubwa. pia usisahau kuchanganya na vitu kama saa, mikanda, wallet (kike na kiume), mikufu, hereni, pete miwani, mpesa na tigo pesa. All the best
 
Back
Top Bottom