Habari zenu jf
Wakati nasoma chuo nilitokea kupendwa Sana na kijana mmoja darasani Ila sikumkubalia ombi la kuwa naye kwa sababu kiumri tulikuwa tunalingana Na hata hivyo sikuwa nimempenda
Mimi baada ya kumaliza chuo nilipata kazi yeye hakupata Hadi Leo ,basi aliamua kurudi shule ambako anasomeshwa na wazazi na mwezi wa kumi na moja shule inaisha.
Baada ya kumaliza shule nilipata mtu mwingine ambaye nilizaa naye Ila baadaye tulishindwana kila mtu akaendelea na maisha yake.
Kwa sababu nilikuwa Sina ugomvi na yule kijana wa chuo tulikuwaga tunasalimiana Mara moja moja na baadaye mwaka Jana nilimuambia kuwa mahusiano yangu yameenda vibaya alinitia moyo na baadaye alirudi Tena akinisihi nimkubalie na yupo tayari kuwa na Mimi no matter what
Nilimkubalia japo mahusiano yalikuwa ya kitoto Toto Sana(yupo chuo)nipo mtaani kazini ,so ilikuwa hatupo committed kabisa hatuzungumzii future Yani Ni ile umeamkaje umeshindaje hatuonani Wala kutembeleana toka mwaka Jana alipita kwangu once akalala kwa jirani kesho yake nikamtembeza town kidogo akenda zake chuo,(Ndo Mana nilikuwa nimekubali yule "una buku hapo ,Mana nilijua kabisa hapa sioni future mwanaume anaonekana bado hela ya kula anapewa na wazazi Mimi tayari Nina maisha refer uzi ulopita )
Pamoja na hayo Ni mtu anaye jali Sana (Siyo kwa maana ya kunipa vitu hapana coz Hana hela ile emotional tu),like KUPIGA simu,kuuliza mipango yangu inaendeleaje hivyo
Akikupigia utapenda "it's like hellow my precious wife how are you doing ,I miss you mpenzi,Nakupenda Sana malkia wangu Yani ana maneno matamu mnoo (alafu kwa kingereza sasa chezea mhaya wewe),aogopi kuku introduce kwa yeyote , he is innocent ,kind ,humble and very understanding
Kuna siku tukawa tunatembea njia nzima nimeshikwa mkono na mkoba nimesaidiwa(jamani sisi wanawake haya Mambo tunapenda Sana) .
Ila kwa upande mwingine Mimi Simpendi akipiga simu wakati mwingine sipokei ,akinitext Kama mud haipo sijibu Yani vyote hivyo vinaonyesha hayupo moyoni mwangu ,wakati mwingine najikaza tu
Nimeona drama za wanaume wa siku za Leo (Siyo wote ) wengine wanachuna wengine waongo, hawajitambui, hawana upendo wa kweli Ila huyu anaonyesha upendo wa agape hasa,
Baada ya kuwaza Sana Nika come up with conclusion,kwa Nini nisieke nguvu zangu na moyo kwa huyu kijana ambaye IAM sure ananipenda na hawezi kunitenda?
sasa ombi langu kwenu nataka nianze kutengeneza mapenzi na huyu kaka ,nisaidie mbinu ya kufanya nimpende na nimshikilie for future use.
#Je Hali yake ya uchumi ya sasa nifanyeje nimsaidie naye atoboe