Nifundisheni Kumpenda

Nifundisheni Kumpenda

Angekuwa na pesa usingemsumbua huyo ila shida ni hali yake ya uchumi..... Sisemi umuwezeshe mtaji wanaume muda mwingine wanafanana na kondoo kumbe chui.... Omba mungu ukubali hali yake basi
 
Habari zenu jf
Wakati nasoma chuo nilitokea kupendwa Sana na kijana mmoja darasani Ila sikumkubalia ombi la kuwa naye kwa sababu kiumri tulikuwa tunalingana Na hata hivyo sikuwa nimempenda

Mimi baada ya kumaliza chuo nilipata kazi yeye hakupata Hadi Leo ,basi aliamua kurudi shule ambako anasomeshwa na wazazi na mwezi wa kumi na moja shule inaisha.

Baada ya kumaliza shule nilipata mtu mwingine ambaye nilizaa naye Ila baadaye tulishindwana kila mtu akaendelea na maisha yake.

Kwa sababu nilikuwa Sina ugomvi na yule kijana wa chuo tulikuwaga tunasalimiana Mara moja moja na baadaye mwaka Jana nilimuambia kuwa mahusiano yangu yameenda vibaya alinitia moyo na baadaye alirudi Tena akinisihi nimkubalie na yupo tayari kuwa na Mimi no matter what

Nilimkubalia japo mahusiano yalikuwa ya kitoto Toto Sana(yupo chuo)nipo mtaani kazini ,so ilikuwa hatupo committed kabisa hatuzungumzii future Yani Ni ile umeamkaje umeshindaje hatuonani Wala kutembeleana toka mwaka Jana alipita kwangu once akalala kwa jirani kesho yake nikamtembeza town kidogo akenda zake chuo,(Ndo Mana nilikuwa nimekubali yule "una buku hapo ,Mana nilijua kabisa hapa sioni future mwanaume anaonekana bado hela ya kula anapewa na wazazi Mimi tayari Nina maisha refer uzi ulopita )

Pamoja na hayo Ni mtu anaye jali Sana (Siyo kwa maana ya kunipa vitu hapana coz Hana hela ile emotional tu),like KUPIGA simu,kuuliza mipango yangu inaendeleaje hivyo
Akikupigia utapenda "it's like hellow my precious wife how are you doing ,I miss you mpenzi,Nakupenda Sana malkia wangu Yani ana maneno matamu mnoo (alafu kwa kingereza sasa chezea mhaya wewe),aogopi kuku introduce kwa yeyote , he is innocent ,kind ,humble and very understanding

Kuna siku tukawa tunatembea njia nzima nimeshikwa mkono na mkoba nimesaidiwa(jamani sisi wanawake haya Mambo tunapenda Sana) .

Ila kwa upande mwingine Mimi Simpendi akipiga simu wakati mwingine sipokei ,akinitext Kama mud haipo sijibu Yani vyote hivyo vinaonyesha hayupo moyoni mwangu ,wakati mwingine najikaza tu

Nimeona drama za wanaume wa siku za Leo (Siyo wote ) wengine wanachuna wengine waongo, hawajitambui, hawana upendo wa kweli Ila huyu anaonyesha upendo wa agape hasa,

Baada ya kuwaza Sana Nika come up with conclusion,kwa Nini nisieke nguvu zangu na moyo kwa huyu kijana ambaye IAM sure ananipenda na hawezi kunitenda?

sasa ombi langu kwenu nataka nianze kutengeneza mapenzi na huyu kaka ,nisaidie mbinu ya kufanya nimpende na nimshikilie for future use.

#Je Hali yake ya uchumi ya sasa nifanyeje nimsaidie naye atoboe
1.acha dharau na kumuona kama mtoto mdogo hyo keshakuwa mtu mama
2.weka kwenye akili yko kwamba hyo ndo your future itakusaidia kupunguza sharia
3.weka mipango sawa ili awe na mishe ya Uganda
N.B wasukuma na wahaya huwa wako serious kwenye mahusiano sio kama wanaume wa dar ambao kwao kumuacha mwanamke n suala la dakika
 
Sawa asante nitaufanyia kazi
 
Lady of Destiy1, mimi napenda kukutia moyo kwa yote unatofanya tena ukimshirikisha MUNGU wako. Kwahiyo basi nikujuze jambo moja ambalo wengi bado hawalijua na linasababisha waumizwe sana sana pale wanapoamua kuanzisha mahusiano na wale wanaowapenda zaidi.
Kwenye mahusiano yenye kuzaa familia bora ni pale unapopata mtu anayekupenda na wewe ukajifunza kumpenda , hiyo ni kwa mwanamke au mwanaume. Mara nyingi sana watu wanaoingia kwenye mahusiano na wale waliowapenda wao ni lazima waishie kuumizwa, kwakuwa huyo yeye aliyempenda atamkubalia kwa kumtumia tu kingono au kipesa na uenda hasiwe na mawazo naye ya kujenga familia, ni wachache inatokea kuwa umempenda naye kakupenda sana.
Mtu akitokea kukupenda unatakiwa ujifunze kumpenda na hapo mtatengeneza penzi zuri sana.
Ushauri juu ya unamsaidiaje yule umpendae kama bado hajawa na kipato cha kuendesha maisha yenu, ni kuchagua siku mnatoana "out", na kuongea kwa undani nini cha kufanya kama ni mradi, au kazi, na kama ni mradi , basi ni mradi gani ambao anauweza unasoko zuri na wa mtaji kiasi gani. Pili huo mradi mfanye kama unamuazima huyo mpenzi wako huo mtaji , ili usimamizi wa huo mtaji uwe mzuri , pamoja na kwamba ni mradi wenu wote.
Na ili kupata faida ni lazima muwe mnaweka kumbukumbu za mahitaji, mauzo, matumizi,mtaji na faida , hapo atanyanyuka na kuwa mmeinuka wote maana pesa yake ndiyo pesa yako.
Kama anakupenda nawe jifunze kumpenda mtakuwa na maisha mazuri, "usiangalie sura".
Sawa
 
Asante sana ubarikiwe
 
Bado hatuja jaribu
Unasubiri nn kumpa kitumbua chako?. Da natamani jamaa yako ndiyo angeleta Uzi humu tumshauri aachie ngazi kwako. alianza kukufuata hukumpenda, ukawa na mwingine akakumimba. Jamaa kazingua mmeanza tena mahusiano lakini mpaka sasa hujampa papuchi!! Hapo mkioona unajitafutia tu lawama za michepuko. Na Ninaamini akija mwanaume mwingine tena unaye mfeel unaweza mpa papuchi kabla yake.
 
Katika vitu nimejaribu nimeshindwa ni kuwa kwa mahusiano na mtu anayenipenda halafu mimi simpendi,

I swear nilishashindwa kupretend, kwanza naweza kuwa naye and still nikajiona niko mpweke like I am still missing out something, akituma msg unaona kero, akipiga simu ndo hata hamu huna, akikuita jina zuri hauskii hata mchecheto wowote moyoni.!!

Hicho kifungo huru kitakusumbua sana, usiwe na mtu ambaye wewe mwenyewe moyoni mwako you are not proud of being with him/her..!!

Yeah, uta force kwa muda but as time passes by ukweli utajidhihirisha, utajikuta akifanya kosa kidogo unachefukwa hasaa,

Honestly, sikushauri uwe na mtu kwa kujipa moyo eti utajifunza kumpenda that's a big lie and stop being desperate, Hebu Lea kwanza mwanao kwa huu muda uliopo.!!
 
Umenivunja moyo jamani
Kwa jinsi ninavyoona huyo jamaa tayari unampenda na ameshakuingia moyoni. Inawezekana kabisa kumpenda mtu kama ukijenga mazingira ya kumzoea na urafiki. Mapenzi yanayojengwa kwenye urafiki uwa yanakuwa strong sana na urafiki unaweza kutengenezwa. Mkubali huyo mtu na pokea simu zake na jibu text zake na ikiwezekana mwambie unampenda kila siku na muanze wewe kuwasiliana

Ni bora uishi na mtu anyekupenda kuliko mtu asiyekupenda maana kupenda ni wajibu wa mwanaume na mwanamke wajibu wake mkuu kwenye mahusiano ni kutii. Wazazi wetu walikuwa wanachaguliwa wake au waume ambao walikuwa hata hawawajui lakini walikubali wakatengeneza mazingira ya kumpenda huyo aliyechaguliwa na wakaishi Maisha mazuri tu mpk tukazaliwa sisi.

Kuhusu kipato chake hilo ni suala la muda tu. Kuendelea kwake kusoma Zaidi inaonyesha ana dira nzuri ya Maisha yake kukuzidi hata wewe kwa kuwa ana elimu Zaidi.

Umeshazalishwa, ni ngumu sana kumpata mtu atakayekuoa ukiwa na mtoto (binafsi hata mimi sitakubali mtoto wangu aoe single mother sababu nazijua mwenyewe) hivyo huyo anayekupenda na kukufanya malikia mshike tena mshike haswa. Ni ngumu sana single mother kuolewa dunia ya sasa kama unabisha kuwa utayaona
 
Unasubiri nn kumpa kitumbua chako?. Da natamani jamaa yako ndiyo angeleta Uzi humu tumshauri aachie ngazi kwako. alianza kukufuata hukumpenda, ukawa na mwingine akakumimba. Jamaa kazingua mmeanza tena mahusiano lakini mpaka sasa hujampa papuchi!! Hapo mkioona unajitafutia tu lawama za michepuko. Na Ninaamini akija mwanaume mwingine tena unaye mfeel unaweza mpa papuchi kabla yake.
Bahati mbaya ushauri nataka Mimi
 
Kwa jinsi ninavyoona huyo jamaa tayari unampenda na ameshakuingia moyoni. Inawezekana kabisa kumpenda mtu kama ukijenga mazingira ya kumzoea na urafiki. Mapenzi yanayojengwa kwenye urafiki uwa yanakuwa strong sana na urafiki unaweza kutengenezwa. Mkubali huyo mtu na pokea simu zake na jibu text zake na ikiwezekana mwambie unampenda kila siku na muanze wewe kuwasiliana

Ni bora uishi na mtu anyekupenda kuliko mtu asiyekupenda maana kupenda ni wajibu wa mwanaume na mwanamke wajibu wake mkuu kwenye mahusiano ni kutii. Wazazi wetu walikuwa wanachaguliwa wake au waume ambao walikuwa hata hawawajui lakini walikubali wakatengeneza mazingira ya kumpenda huyo aliyechaguliwa na wakaishi Maisha mazuri tu mpk tukazaliwa sisi.

Kuhusu kipato chake hilo ni suala la muda tu. Kuendelea kwake kusoma Zaidi inaonyesha ana dira nzuri ya Maisha yake kukuzidi hata wewe kwa kuwa ana elimu Zaidi.

Umeshazalishwa, ni ngumu sana kumpata mtu atakayekuoa ukiwa na mtoto (binafsi hata mimi sitakubali mtoto wangu aoe single mother sababu nazijua mwenyewe) hivyo huyo anayekupenda na kukufanya malikia mshike tena mshike haswa. Ni ngumu sana single mother kuolewa dunia ya sasa kama unabisha kuwa utayaona
Ngoja nianze zoezi
 
Hahahaaa bibie.....
Mapenzi hayana harufu wala rangi ili tuweze kukufundisha.
Hivyo tu ulivyojieleza inatosha kabisa kusema ushaanza kupenda
 
Back
Top Bottom